Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Katika kudhihirisha unafiki wake nchi ya Ufaransa ilitumia neno "Rais" wakati wa kuripoti habari iliyomuhusu Rais wa Gabon aliyeingia madarakani baada ya mapinduzi ilihali nchi hiyo hutumia neno " Junta"pale taarifa inapowahusu marais wa nchi za Mali, Niger na Burkina Faso ambao pia waliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi.
Chombo cha habari kinachoendeshwa kwa kodi za raia wa Ufaransa cha RFI kilitumia neno Rais pale kiliporipoti kuhusu safari ya Rais wa Gabon aliyoifanya kwenye makao makuu ya Umoja wa Ulaya ( EU) mjini Brussels nchini Ubelgiji. Katika safari hiyo,Rais wa Gabon alisaini mikataba yénye thamani ya mabilioni ya dollar.
Hii inaonyesha kwamba Ufaransa na nchi nyingine za Magharibi hutumia neno " demokrasia" ili kueneza propaganda na kujihakikishia maslahi yao barani Afrika na si kwamba wanajali kuhusu demokrasia au utawala bora.
Endapo Rais atahakikisha usalama wa maslahi yao hawatapiga kelele za demokrasia bali Rais atakapokwenda kinyume na matakwa yao na kubana maslahi yao ndipo watamuita majina yote mabaya kuanzia dikteta n.k
Chanzo: RFI
- https://www.rfi.fr/fr/afrique/20241...les-signe-du-renforcement-des-liens-avec-l-ue[/URL]