Nestory Semeni
Member
- Jul 8, 2024
- 24
- 47
Ndani ya biblia kuna mtu anaitwa Samson
Ni jamaa ambaye tangu utoto wake hakuwahi kunyolewa nywele na ilikuwa ndio siri yake kubwa ya nguvu kubwa,
Tena za ajabu,
Kila jambo ambalo lilifanyika dhidi yake ili kumshinda halikufanikiwa,
Lakini,
Siku ambapo chanzo cha nguvu zake kilipojulikana,
Na akanyolewa nywele,
Alikuwa dhaifu hatari
Mpaka ana kamatwa na kutobolewa macho,
Sasa sikia hiki,
Leo hii ni muhimu kwako kujua chanzo cha nguvu zako ni kipi sasa,
Yaani ni nini hasa ambacho wewe huwa unaona kinakufanya upate hamasa, ile useme na wewe ni binadamu,
Na hata unakuwa huru kushirikiana na watu wengine,
Hapa kuna mtego ambao wengi huwa unatukuta,
Nguvu kupata kwenye vitu, watu na hata "hali fulani"
Kupata kwenye vitu ni kama hivi,
Unajiona ni wa maana sana na hata mwenye nguvu na imara hasa pale ambapo una miliki vitu fulani,
Nyumba,
Simu kali,
Gari ya kiboss,
Saa inayoendana na mishahara ya wengi,
Hatari ya kupata nguvu hapa ni hii
Siku ambayo vitu hivyo vitapotea au kuibiwa utajikuta unahisi kukata tamaa kabisa na maisha,
Yani ni bora hata ukope ili upate hivyo vitu mbaya zaidi ni pale hata huwezi kukopa
Kuna hili jingine,
Kupata nguvu zako kwa watu,
Yani ni hao ambao unawaita marafiki,
Ndugu,
Au vyovyote vile,
Sasa hivi unaona kweli wanakujali na kukuthamini sana,
Na wanakuhakikishia "hatutokuacha"
"Yani mimi na wewe ni dam dam'
Ujue nini,
Kesho na kesho kutwa wanabadilika na wewe uliona kuwa nao ndio furaha yako,
Wanakua maadui na hata ujui ufanyeje,
Lakini huenda isifike huko ikatokea tu bahati mbaya naye "amefariki"
Utafanyeje? Au utamfuata huko huko?
Umeona ilivyo mbaya? Haimaanishi usishirikiane na watu ila ni lazima ujue unapata nguvu zako toka wapi hasa?
Yaani chemichemi ni ipi?
Na hii naona ni bora zaidi kukiko hizo mbili,
Kutegemea "Kanuni" Kama Chanzo cha nguvu.
Yani mambo ambayo ukifanya lazima utapata matokeo mazuri tu, na madhara kidogo yanayovumilika,
Ni sheria za asili ambazo zipo tu hivyo hakuna ambaye anaweza kuzibadilisha ili yeye anufaike nazo,
Ngoja tuelewane kanuni ipoje,
Ukipanda juu ya ghorofa na kujirusha utaanguka? Au utabaki hapo hapo?
Je wewe kama ni "boss" utaanguka? Au utabaki hapo hapo?
Vipi kama ni mchungaji? Au raisi wa nchi? Au ni kichanga cha kuonewa huruma?
Utagundua tu ni kwamba "hakuna ubaguzi hapo" kila kitu kitaanguka tu,
Hakuna kusema kuna kuganda sehemu fulani, yote ni kwamba pale ambapo hakuna msaada wa nje.
Sasa maisha ya kutegemea kanuni yapoje,
Yani ni wewe kuwa na nguvu zaidi au amani au furaha kwa sababu "unazijua kanuni za maisha" (Sheria za asili)
Yani,
Unajua mambo ambayo ukifanya au ukifuata ni lazima tu "utoboe"
Ni lazima tu upige hatua,
Ni kama vile kujua kutembea,
Kwa hiyo unapopitia jambo gumu ni kwamba unajiuliza kanuni zipi za kufuata,
Mfano:
Unapata mauzo mabovu? Badala ya kujikatia tamaa kwamba "huwezi biashara"
Unajiuliza "ni mambo yapi ukiyafanya ni lazima kwako kupata mauzo ya kutosha?"
Unapitia wakati mgumu kwenye ndoa?
Badala ya kufikiria "huwezi tena, ndio unakaribia kuachika jiulize" , "Ni mambo yapi ukifanya au kubadilisha ni lazima tu ndoa kurudi kama zamani?"
Afya yako inakuwa mbaya? Lazima kujiuliza tena "ni mambo ukifuata ni lazima kurudi kuwa vizuri kiafya?"
Kumbuka,
Kushindwa kwako hapa inakuwa ni kwa sababu haujui kanuni za kukuongoza katika hali uliyopo
Na hivyo kama unakosa majibu ndio muda wa kujifunza,
Kujua kwa undani kanuni au sheria za asili kuhusu hilo tatizo lako zipoje.
Nakubali kufuata kanuni hakutakuwa rahisi lakini ndiko kubakufanya uwe huru
Na mtu ambaye huwezi kata tamaa kirahisi.
Je una swali lolote karibu.