Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Majamaa waliingia nyumbani kwa Diddy na wakachukua kila kitu, ikiwemo hard disk za kamera za siri ambazo Diddy alikuwa ameweka kwa ajili ya kurekodi kila kitu kilichokuwa kinaendelea.
Kamera za siri? Yaani alikuwa anarekodi kila kitu, hadi kitendo cha Diamond kuingia kwenye jumba lile, kilirekodiwa.
Hii ni kawaida sana hasa kwa watu maarufu. Wale TISS ya Marekani sasa wanajua kila kitu: nani alifanywa na Diddy, nani hakufanywa, nani alisalimika, na nani aliwahiwa.
Wasanii wengi wapo kimya kwa sababu wanajua kuwa majamaa wana ushahidi wa kila kitu. Wanachofanya ni kuvujisha taarifa moja baada ya nyingine, si kwa bahati mbaya, bali makusudi kabisa.
Jay Z kimyaaaa. Dj Khaled, Beyonce, na Lebron James pia wapo kimyaaaa. Unadhani zile sauti za Burna Boy zinatolewa bure? Ni kwa makusudi.
Mademu wengi wamemalizwa humo, ikiwemo mastaa wa Afrika walioshinda Grammy. Jiulize, kwa nini Davido hasemwi kwenye hili?
Ukizaliwa kwenye pesa na ukakua kwenye pesa, kuna ulimbukeni fulani huna. Tofauti na aliyekuwa choka akipata pesa, huwa tunakosa nidhamu. Hii ni changamoto kubwa kwa watu weusi. Washajua hilo, hivyo inakuwa rahisi kutudhibiti.
Hawakushindwa? Wanamtumia mkeo; anaomba talaka, unatozwa pesa nyingi. Hakuna mtu mweusi aliye salama kwa sababu ya ulimbukeni wa pesa tulionao.
Wakipata pesa, maslay queen wote wanataka kula, washikaji wanakula bata klabu, na mbaya zaidi, washauri wetu huwa ni watu weusi. Angalia wale walio na washauri wa kizungu huko US, kuna tofauti kubwa.
Mpaka sasa, hakuna staa aliye salama, hasa kwa Diddy. Diddy hawezi kuchomoka hili, ama atafungwa au mtu atatumwa aondoe roho yake.
Ukiua kwa upanga, utakufa kwa upanga. Huwezi kumuua 2pac ukabaki salama. Huwezi kumdedisha BIG na kumdhulumu mkewe Faith Evans ukabaki salama. Huwezi kumdhulumu Mase, akaangua kilio kanisani halafu ukabaki salama.
Mara nyingine, tunatengeneza hatima yetu hapa duniani. Umeua kwa upanga, utakufa kwa upanga.
