Unahisi nani alinywea hapa?

Hapana chezea gattuso tetesi zinasema Ronaldo anajiandaa kuandika kitabu kuhusu huyu gattuso[emoji3][emoji3]

Na hata pia Puyol.

Nakumbuka baada ya ile fainali ya ligi ya mabingwa ambayo man utd alikufa 2-0 dhidi ya barca, Ronaldo alisikika akisema hakuna siku aliyopata shida katika maisha yake ya soka uwanjani kama siku ile na aliyempa hiyo shida ni Carles Puyol
 
Juzi niliangalia kidogo baadhi ya mechi za ligi ya Brazil kwa kweli nilikumbuka zile mechi za miaka ishirini iliyopita kwanza spidi ,ufundi,pia niligundua marefa wa Brazil hawana ule Utu wa kirefarii yaani kosa moja kadi nyekundu,hakuna mazungumzo hapa ndio kidogo nilichoka,Lizarazu juzi nilivyomuona mnyama eto's niliumia sana navuta picha miamba ya cameroun vs Ghana eeehe halafu eti AFRICON hakuna mashabiki jamaniii kizazi hiki kimekuwaje?duu masikitiko !!!Mungu rudisha drogba,regorbert song,yekini,babayaro,bila kusahau mwanza ,chikwalakwala,pale zambia ,dunia inakimbia sana
 
Gattuso alikuwa hatari sana, Apumzike kwa amani!
 

Mkuu tukiongelea America ya kusini hasa Brazil, hapo haungelei mpira tena bali unaongelea sanaa katika mpira(The art in football), yaani mpira uliotawaliwa na ufundi wa hali ya juu usiochosha kabisa kuutizama.

Vilabu vya brazil vinacheza mpira wa kuvutia haswa kuliko hata timu yao ya taifa(selecao) maana kule wachezaji wengi wanatoka mule mule brazil ambako mpira ni sanaa/tamaduni.

Kwenye football academies za brazil wanamjenga mchezaji zaidi kwanza kwenye skills(dribbling,controls,passes) halafu baadae ndio linakuja suala la teamwork. Tofauti na academy za ulaya ambako wanafundisha zaidi jinsi ya kucheza kitimu mwanzo mwisho.

Wachezaji wengi wa kibrazil huwa wanabadirika wakienda ulaya, wakifika huko nao wanaanza kucheza direct football so ule udambwi udambwi wote unawekwa kando. Na ndio maana hata timu yao ya taifa siku hizi haina lile soka la kuvutia sana maana wachezaji wengi wanaoitwa ni wale wanaocheza ligi za ulaya.

Soka la ulaya ni la kutafuta ushindi zaidi, Niliwahi kuskia kuwa wakati Adriano Ribeiro ametoka Flamengo na kusajiliwa Inter mwaka 2001 alipokutana na kaka yake Ronaldo Delima pale sansiro, Ronaldo alimwambia kwamba “hawa mashabiki wa ulaya wanahitaji magoli tu, na hili uweze kuteka mioyo yao yakupasa ufunge mara kwa mara sio lazima wakuone ukipiga chenga, kama unataka chenga subiri tutaenda kuzipiga tukiwa na timu yetu ya taifa”.

Hapo kwa marefa sio kwa brazil tu, marefa wa amerika ya kusini karibia wote tu huwa ni mabandindu na huwa wana watesa sana Messi na Neymar. Tumezoea kuona messi akiskilizwa sana uwanjani na marefa anapokuwa spain, lakini akirudi huko kwao anapuuzwa vibaya mno na marefa mpaka anakuwa mkali.

Afcon ya sasa hivi imepoteza mvuto sababu hata wachezaji tulionao hawako skillful kiviiiile kama ilivyokuwa zamani, wengi tulionao ni wakawaida tu sema ni overpriced sababu wamekuzwa ulaya, na pia hawana profile kubwa hata kwenye vilabu wanavyochezea kama ilivyo kwa akina Drogba,eto’o,kanu etc
 
Hii mechi naikumbuka, ghatuso akili zake anazijua mwenyewe
 
Asante kaka nacheka tu hapa kila nikikumbuka....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…