Unahitaji miaka mingapi ili ufanikiwe kupitia kazi yako?

Unahitaji miaka mingapi ili ufanikiwe kupitia kazi yako?

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Haya nimejifunza mimi kupitia shughuli zangu na kuwaona pia wengine kwenye shughuli zao. Mafanikio ni mchakato na kila kazi ina njia zake kuna kazi zinamafanikio ya haraka na hata kupotea huja kwa haraka sana kupitia kazi zangu tatu ninazofanya nimejifunza haya.

1. Biashara, hii ni kazi ngumu sana itabaki ni option na njia ya mafanikio kwa wachache sana , biashara inakanuni nyingi sana za wazi na kanuni ZA SIRINI, NIMEKUTANA NA SIRI nyingi na mambo ya ajabu sana,kwenye biashara mtu anafika mahali hawezi kueleza amefanikiwaje na hata akiporomoka hajui ilikuwaje, kinachosemwa muda mwingine sio kinachoendelea kwenye biashara, ili ufanikiwe kupitia biashara unahitaji miaka kumi na kuendelea huku ukiwa mvumilivu sana, nje ya hapo umekwama.

2. Kilimo na ufugaji (hapa sio pagumu sana ila pana matokeo ya kushangaza sana, unaweka pesa nyingi unapata hasara ama faida kidogo, unaweka pesa kidogo faida kubwa, kilimo hakitaki mazoea unaishi msimu kwa msimu , bei ya soko inabadilika wakati umeishaweka pesa zako humo, unahitaji miaka kama saba kuanZa kuhisi mafanikio kwenye ufugaji unahitaji miaka kama kumi na tano kufanikiwa kupitia kilimo

3. Ajira, nimeajiriwa kama mwalimu nilichojifunza ualimu unaweza usifanikiwe hadi unastafu otherwise unatumia akili nyingi, unatakiwa uibe muda na ufanye kazi zako na utumie salary na mikopo kuanzisha kazi zako binafsi, otherwise ajira kama ualimu inakuacha maskini milele.

Tuambie kazi unazofanya zinahitaji muda gani ufanikiwe na je kuanguka kwake kupoje.
 
Mafanikio ni yapi? Hakuna mafanikio zaidi ya kuridhika, mpaka unakufa utaona bado hujfanikiwa.

Watu wanaweza kukuona umefanikiwa ila wewe binafsi unaona bado ..
 
Kuanza kuhisi Amani unapofanya kazi zako ndio kufanikiwa kwenyewe, huumizi kichwa kuhusu kazi iwe kuitanua au kuanzisha mradi mahali.
 
Ndio hivyo yaani kuhisi amani ni kuridhika pia, unakuta hauna cha kufanya.

Ishu ya mafanikio ni utapeli kwa kuangalia wengine huwezi kuelewa maana ya Mafanikio, wapo waliokuzidi ila sio mafanikio.

Mafanikio yanatokana na wewe binafsi kutumia vyema nafasi yako katika kufanikisha mambo yako. Mambo ya tajiri fulani hayakuhusu, yeye mfanyabiashara wewe mwajiriwa mna level tofauti za mafanikio.

Mwingine awe na familia ,tamaa za kujifananisha ni mda mdogo tu ukifika miaka 60 utaona kawaida hata kuishi kijijini utaona sawa. Hakuna tafsiri ya mafanikio achana na motivational speakers.
 
li ufanikiwe kupitia biashara unahitaji miaka kumi na kuendelea huku ukiwa mvumilivu sana, nje ya hapo umekwama.
hapa nimekuelewa zaidi.
 
Back
Top Bottom