UNAIDS: 87% ya wanaoishi na VVU nchini wanatumia dawa

UNAIDS: 87% ya wanaoishi na VVU nchini wanatumia dawa

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Tanzania imetajwa kuwa nchi ya mfano katika udhibiti wa maambukizi ya Ukimwi na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa Ukimwi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Ukimwi (UNAIDS), Winnie Byanyima amesema, sababu ya uzinduzi wa ripoti hiyo kufanyika nchini ni kutokana na mafanikio ya Tanzania katika kudhibiti ugonjwa huo.

"Sababu ya kuja kufanya uzinduzi wa ripoti hii hapa nchini ni kutokana na juhudi kubwa ambazo Tanzania imekuwa ikichukua kudhibiti maambukizi ya ukimwi,” amesema

“Mwaka 2010, kwa miaka 10 mfufulizo imefanikiwa kupunguza maambukizi na vifo vitokanavyo na ukimwi kwa asilimia 50, Tanzania imekuwa nchi ya mfano duniania katika udhibiti wa ugonjwa huu," amesema.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema, uzinduzi wa ripoti hiyo nchini ni heshima kwa Tanzania kutokana na juhudi ambazo Serikali imekuwa ikiweka kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.

Mwenyekiti wa Baraza la watu wanaoishi na ukimwi Tanzania (Nacopha) Leticia Kapala amesema, kwa sasa Serikali imekuwa ikichukua juhudi za kuyafikia makundi yote yaliyo katika hatari ya kupata mambukizi ya ukimwi pamoja na kutoa elimu kutokomeza unyanyapaaa.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom