UNAIDS: Maambukizi ya UKIMWI yanaweza kuongezeka mara 6 kufikia mwaka 2029

Hivi TZGOV ikiamua itashindwa kweli kutenga fungu kwa ajili ya hizo dawa !!?? Mambo mengine I feel yako ndani ya uwezo wetu !!
Kile kikopo gharama yake ni USD 500 sawa na zaidi ya TZS 1,000,000 na kinatumika kwa mwezi mmoja.
Watumiaji wapo zaidi ya milioni 1.2.
Sidhani kama wanaweza kwa akili hizi hizi tunazozijua.
 
Kivipi mkuu?
EU na USA Wakisitisha misaada moja kwa moja ya Arv sidhani kama Africa itaweza kuhudumia watu wake, UKIMWI ule utishao kama upo sasa utaonekana kwa macho matumizi ya condom yatazidi, watu wataiogopa ngono.
 
Wakuu,

Hivi si tuliambiwa kuwa ARV ziko za kutosha?

Na kwamba tusihofu Marekani kusitisha misaada kwa sababu serikali ina ARV zinazotosha? Sasa inakuaje tunapewa onyo kuwa maambukizi ya UKIMWI yataongezeka?

Au ndo yaleyale tuliambiwa Rais yuko fit alafu baada ya siku kadhaa tukatangaziwa msiba wa taifa?

=========================================================

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na Ukimwi (UNAIDS), Winnie Byanyima, ameonya kuwa idadi ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI (HIV) huenda ikaongezeka mara sita zaidi ifikapo mwaka 2029, endapo Marekani itasitisha ufadhili wake kwa mpango wa kukabiliana na ugonjwa huo.

Byanyima amesema kuwa kusitishwa kwa msaada huo kunaweza kusababisha vifo vya mamilioni ya watu, pamoja na uwezekano wa kuibuka kwa aina mpya na sugu ya virusi vya HIV.

Soma pia: Wizara ya Afya: ARV zipo za kutosha

Katika mahojiano na Shirika la Habari la AP, akiwa nchini Uganda, Byanyima amesema kuwa, licha ya kupungua kwa maambukizi katika miaka ya hivi karibuni, hatua yoyote ya kusitisha msaada wa kimataifa inaweza kurudisha nyuma mafanikio hayo.

Mwaka 2023, maambukizi mapya ya HIV yalirekodiwa kuwa milioni 1.3- punguzo la 60% tangu kiwango cha juu zaidi kiliporekodiwa mwaka 1995. Hata hivyo, Byanyima ameonya kuwa, endapo msaada wa Marekani utasitishwa, ifikapo 2029, dunia inaweza kushuhudia maambukizi mapya milioni 8.7, vifo vinavyohusiana na UKIMWI milioni 6.3, na watoto yatima milioni 3.4

Tishio hilo linatokana na tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump, kwamba Marekani itasitisha misaada yote ya kigeni ndani ya siku 90. Hatua hii imeibua wasiwasi mkubwa, kwani Marekani ni mfadhili mkuu wa mipango ya afya duniani, ikiwemo PEPFAR- mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na UKIMWI.

Hamna lolote wao na madawa yao ndio wanaufanya uzidi kuwepo kwa kasi.
Waondoe misaada yao hatuitaki
 
Hivi si tuliambiwa kuwa ARV ziko za kutosha?
Lini Sirikali ilisema Ukweli? Tuliambiwa Mwendokasi ya Mbagala itaanza Dec 2024 mpaka leo bado haujaanza.

Wakasema elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi form 6 lakini mwanafunzi akichaguliwa lazima uwe na mpunga si chini ya laki 3.

Hospital wazee ,watoto matibabiu ni bure lakini ukienda unadaiwa fedha.

Kwahiyo usiamini Sirikali hata kidogo.
 
Kile kikopo gharama yake ni USD 500 sawa na zaidi ya TZS 1,000,000 na kinatumika kwa mwezi mmoja.
Watumiaji wapo zaidi ya milioni 1.2.
Sidhani kama wanaweza kwa akili hizi hizi tunazozijua.
Haifiki huko !!Mfano kikopo cha vidonge 30 za FDC (Tenofovir+Lamivudine+Dolutegravir) ni USD 7.00 - 10.00.
 
Mkuuu usichukulie simple hiyo USD 10 kwa mwezi , kumbuka siku hizi Ukimwi walionao wengi ni Choka Mbaya! Kila mwezi imtoke elfu 25.
 
Nlikuwa naangalia zaidi issue ya Ufadhili wa Nje vs Vyanzo vya ndani !!! Kwa mgonjwa ni kweli wengi hawatoweza hujinunulia !!
 
Sirikali haiwajali wananchi wake hata siku moja ,wao watatumia fedha za ndani kununua mavieite tu ,kujijengea majumba ya wastaafu na kulipana wenza wa viongozi ila kuweka ruzuku kwenye ARV sahahu.

Vijana waliochoka wanajilipua kununua "Mal.@.ya wa Buku buku , vijana wanajilupua kula mishngazi yenye fedha na kuambukizwa ,bodaboda wanajiokotea mizigo tu na kumalizana nao kavu kavu ,means wenye ngoma siku hizi ni chokambaya.....Ukimwi huu bila ARVs kutoboa hata mwaka ngumu labda uwe carrier.
 
Haifiki huko !!Mfano kikopo cha vidonge 30 za FDC (Tenofovir+Lamivudine+Dolutegravir) ni USD 7.00 - 10.00.
Uko sahihi, nimesoma nimeona uko sawa.
Nilidhani kati ya hizo na PEP bei ni sawa kumbe ñi tafauti kabisa.
Bei ya PEP ndio ipo huko USD 600+, hizi nilishawahi kutumia mara 2 katika kipindi tofauti.
Screenshot_20250212-090441_Chrome.jpg
 
Hatari
Wakuu,

Hivi si tuliambiwa kuwa ARV ziko za kutosha?

Na kwamba tusihofu Marekani kusitisha misaada kwa sababu serikali ina ARV zinazotosha? Sasa inakuaje tunapewa onyo kuwa maambukizi ya UKIMWI yataongezeka?

Au ndo yaleyale tuliambiwa Rais yuko fit alafu baada ya siku kadhaa tukatangaziwa msiba wa taifa?

=========================================================

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na Ukimwi (UNAIDS), Winnie Byanyima, ameonya kuwa idadi ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI (HIV) huenda ikaongezeka mara sita zaidi ifikapo mwaka 2029, endapo Marekani itasitisha ufadhili wake kwa mpango wa kukabiliana na ugonjwa huo.

Byanyima amesema kuwa kusitishwa kwa msaada huo kunaweza kusababisha vifo vya mamilioni ya watu, pamoja na uwezekano wa kuibuka kwa aina mpya na sugu ya virusi vya HIV.

Soma pia: Wizara ya Afya: ARV zipo za kutosha

Katika mahojiano na Shirika la Habari la AP, akiwa nchini Uganda, Byanyima amesema kuwa, licha ya kupungua kwa maambukizi katika miaka ya hivi karibuni, hatua yoyote ya kusitisha msaada wa kimataifa inaweza kurudisha nyuma mafanikio hayo.

Mwaka 2023, maambukizi mapya ya HIV yalirekodiwa kuwa milioni 1.3- punguzo la 60% tangu kiwango cha juu zaidi kiliporekodiwa mwaka 1995. Hata hivyo, Byanyima ameonya kuwa, endapo msaada wa Marekani utasitishwa, ifikapo 2029, dunia inaweza kushuhudia maambukizi mapya milioni 8.7, vifo vinavyohusiana na UKIMWI milioni 6.3, na watoto yatima milioni 3.4

Tishio hilo linatokana na tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump, kwamba Marekani itasitisha misaada yote ya kigeni ndani ya siku 90. Hatua hii imeibua wasiwasi mkubwa, kwani Marekani ni mfadhili mkuu wa mipango ya afya duniani, ikiwemo PEPFAR- mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na UKIMWI.

Wakuu,

Hivi si tuliambiwa kuwa ARV ziko za kutosha?

Na kwamba tusihofu Marekani kusitisha misaada kwa sababu serikali ina ARV zinazotosha? Sasa inakuaje tunapewa onyo kuwa maambukizi ya UKIMWI yataongezeka?

Au ndo yaleyale tuliambiwa Rais yuko fit alafu baada ya siku kadhaa tukatangaziwa msiba wa taifa?

=========================================================

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na Ukimwi (UNAIDS), Winnie Byanyima, ameonya kuwa idadi ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI (HIV) huenda ikaongezeka mara sita zaidi ifikapo mwaka 2029, endapo Marekani itasitisha ufadhili wake kwa mpango wa kukabiliana na ugonjwa huo.

Byanyima amesema kuwa kusitishwa kwa msaada huo kunaweza kusababisha vifo vya mamilioni ya watu, pamoja na uwezekano wa kuibuka kwa aina mpya na sugu ya virusi vya HIV.

Soma pia: Wizara ya Afya: ARV zipo za kutosha

Katika mahojiano na Shirika la Habari la AP, akiwa nchini Uganda, Byanyima amesema kuwa, licha ya kupungua kwa maambukizi katika miaka ya hivi karibuni, hatua yoyote ya kusitisha msaada wa kimataifa inaweza kurudisha nyuma mafanikio hayo.

Mwaka 2023, maambukizi mapya ya HIV yalirekodiwa kuwa milioni 1.3- punguzo la 60% tangu kiwango cha juu zaidi kiliporekodiwa mwaka 1995. Hata hivyo, Byanyima ameonya kuwa, endapo msaada wa Marekani utasitishwa, ifikapo 2029, dunia inaweza kushuhudia maambukizi mapya milioni 8.7, vifo vinavyohusiana na UKIMWI milioni 6.3, na watoto yatima milioni 3.4

Tishio hilo linatokana na tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump, kwamba Marekani itasitisha misaada yote ya kigeni ndani ya siku 90. Hatua hii imeibua wasiwasi mkubwa, kwani Marekani ni mfadhili mkuu wa mipango ya afya duniani, ikiwemo PEPFAR- mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na UKIMWI.

Kwa nini kulia lia na Hela za wamarekani ambao wanachapa kazi usiku na mchana!

Trump ni mshirika muhimu sana wa maendeleo barani Afrika.
 
Zinatosha, maana yake ukienda leo kesho utazikuta ijapokuwa walitia jibu la juu juu, maana walipaswa zatisha mpaka lini. Ila hazitoshi mpaka 2029.
 
Ni wakati sasa kuishi kwa tahadhari, hakuna haja ya kuwa na michepuko.
 
Back
Top Bottom