Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Its never too late. You still have an option to check in depth nature of your family. There some things you can still change while you are in. Remember the emphasis is to raise a good life and good family!
nakumbuka kaka yangu wa kwanza kuzaliwa wakatim anatarajia kuoa, baada ya kumweleza baba, baba alifanya udadisi kujua alipotoka huyo mwanamnke, baada ya kujua atokapo huyo mwanamke, kisha akamwambia kaka asubiri atamjibu.Alisafiri kwa siri hadi huko kijijini na kufanya ushu-shushu wake na baada ya kurudi akamwambia kaka aende kule kijijini akamuone mzee fulani yeye ndiye atakayekuwa baba yake wa kumsaidia kuposa na kumfungisha ndoa.
Kumbe alishaongea na huyo mzee na kukubaliana naye amsdaidie kusimamia ndoa ya kaka yetu kwa kuwa huko kaka alipotarajia kuoa ni mbali na alipo na yeye alikuwa ni mtumishi asingeweza kusafiri kwenda huko.
Na utaratibu huo aliufanya hata kwetu sisi kufanya ushu-shushu kabla ya kutoa go ahead ya kuoa.
Ni jambo zuri sana kuijua familia unayooa au kuolewa, wazee walikuwa na maana zao kutukataza kuto-oa koo fulani.
Tausi Mzalendo, mzee alikuwa anaangalia vitu kama Ulozi, Kifafa na magonjwa mengine ya kurithi na pia tabia ya familia kwa ujumla, wizi wizi na udhulumaji.............Pamoja na kukubaliana nawe, zama zimebadilika.Mfano wa kaka yako ni typical kwa watu waliozaliwa na kukulia vijijini.Chukulia kuwa huyo kaka yako angepata mchumba aliyezaliwa na kukulia nje ya mkoa, au nchi mnayoishi.Baba yako angefanya nini? Wakati mwingine ni vigumu kufanya upelelezi.Binti labda kasomea shule za bweni miaka yote.Kijijini hajakaa au hata kwenda ni mara moja moja.Huwezi kumhukumu kwa tabia za "wanafamilia".Tabia pia huchangiwa na mazingira.Chukulia kwa mfano, familia ina tabia ya uchapa kazi na heshima z kupiga magoti. Binti kakulia mbali na familia, hajui hata mila na desturi, hajawahi kushika jembe, hajafundishwa kufanya kazi - anachojua yeye ni kupata kila anachokitaka na ziada. Atarithi tabia za familia?
Dunia imekuwa kijiji.Watu/watoto hufunzwa na dunia zaidi ya wanavyofunzwa na mama siku hizi.
Kupata mwenza atakayekidhi vigezo, viwango, matamanio na matarajio itategemea:
- Mhusika/Mtafutaji yeye mwenyewe ana tabia gani.Kama ana tabia mbaya basi huenda atakutana na mtu mwenye tabia mbaya kam zake
- Mazingira ya kufahamiana na muda utakaochukua kumfahamu mwenzio na kufanya maamuzi
- Kudra ya mwenyezi Mungu!
Pamoja na kukubaliana nawe, zama zimebadilika.Mfano wa kaka yako ni typical kwa watu waliozaliwa na kukulia vijijini.Chukulia kuwa huyo kaka yako angepata mchumba aliyezaliwa na kukulia nje ya mkoa, au nchi mnayoishi.Baba yako angefanya nini? Wakati mwingine ni vigumu kufanya upelelezi.Binti labda kasomea shule za bweni miaka yote.Kijijini hajakaa au hata kwenda ni mara moja moja.Huwezi kumhukumu kwa tabia za "wanafamilia".Tabia pia huchangiwa na mazingira.Chukulia kwa mfano, familia ina tabia ya uchapa kazi na heshima z kupiga magoti. Binti kakulia mbali na familia, hajui hata mila na desturi, hajawahi kushika jembe, hajafundishwa kufanya kazi - anachojua yeye ni kupata kila anachokitaka na ziada. Atarithi tabia za familia?
Dunia imekuwa kijiji.Watu/watoto hufunzwa na dunia zaidi ya wanavyofunzwa na mama siku hizi.
Kupata mwenza atakayekidhi vigezo, viwango, matamanio na matarajio itategemea:
- Mhusika/Mtafutaji yeye mwenyewe ana tabia gani.Kama ana tabia mbaya basi huenda atakutana na mtu mwenye tabia mbaya kam zake
- Mazingira ya kufahamiana na muda utakaochukua kumfahamu mwenzio na kufanya maamuzi
- Kudra ya mwenyezi Mungu!
Ninavyofahamu tabia ya mtu haifutiki kwa kubadili mazingira. Inaweza ikafunikwa kwa muda tuu. Halafu kwenye familia huangalii tabia tuu, kuna mambo kama magonjwa nk nk" sasa vyema ukafahamu ili ujipange vyema uendapo huko
Mimi sista aliolewa na raia wa kenya wanaishi bongo,sista akuwafahamu ndugu wa mmewe kwa undani kumbe alikuwa anamkutanisha na marafiki anazuga kuwa ni wadogo au kaka zake ,akawa anajifanya mambo safi.familia aikupenda sista aolewe na huyu bwana lakni dada alpolazmisha familia ilikubali kuepusha lawama kwa dada.sasa hivi amekuja gundua wazazi wa mme wake ni waganga wa kienyeji uko kwao mombasa na amekuwa akiaribu mimba,mwanaume pesa yake aijulikani inapokwenda dada ndio analipa kodi na kumlea jamaa ukikutana na jamaa kitambi kikubwa.familia ilimpa dada kiwanja jamaa kakiuza kinyemela akanunua gari. Dada/kaka kuweni makini mtakapo kuowa au kuolewa