Unaifahamu vipi CocaCola?

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Posts
23,372
Reaction score
54,943
Jamii forum ni sehemu yenye watu wa kila aina ,(wadukuzi wa mambo) vipo vitu vingi ambavyo vimepata majibu na pia wengi wamefahamu mengi sana kupitia jamii forum (hongereni wote wanaoshiriki kikamilifu kutoa taarifa mbalimbali hapa JF)

Ila leo ninahitaji tusaidiane katika hili,kuhusu kampuni ya coca cola ambayo ina miaka 130 tangu kuanzishwa kwake (may 08,1886)

Kampuni hii licha ya kuuza kuliko kampuni yeyote ile ya vinywaji hapa duniani ina mambo mengine ambayo ni siri sana naomba kwa mwenye ufahamu wake anaweza kutushirikisha.

Inasemekana kampuni hii licha ya kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi na kueneka karibia dunia nzima ni watu wawili tu wanafahamu kuhusu utengenezaji wa vinywaji vya kampuni hii.

Nilipata mshituko kuhusu siri hii kipi kipo nyuma ya pazia ,imebidi nije JF kushirikishana juu ya kampuni hii,(japo sina nia ya kuwatangaza vibaya ila ninahitaji kufahamu).

Ntashukuru kwa wote watakaofanikisha hili na kuweka nondo zenye kuhusu kampuni hii.
 
Cocacola nikinywaji kitam kinarangi nyeusi na kinagesi hakina kilevi kinauzwa sh 400 kwa chupa ndogo sh 500 kwa chupa ya kati 350 ml sh 1000 kwa chupa ya plastic 500ml sh1500 kwa chupa ya plastic saiz ya kai na sh 2500 ml kwa chupa kubwa na kuna chupa mpya ya plastic sh 500. swali jingine pls
 
Wewe lazima utakuwa mwanasheria
 
Kwa taarifa yako tu ni kuwa katika Patent zenye thamani kuliko zote duniani ya coca cola ndio namba moja,

pia ndio inayolindwa kuliko zote, ndio maana hadi leo hiyo ni siri kubwa sana, hao wengine akina pepsi na wenzake wanajaribu kutengeneza lakini hawawezi kutoa kama koka.

hiyo ni siri ya familia, na sio wanafamilia wote wanajua.
akifa baba anamuachia mtoto
 
Yah ,nataka majibu kama haya sio jitu linakuja kutuwekea hapa bei ya soda kama vile hatujui,(asante sana mkuu)
 
Huu ni uzushi tu.

Sasa kama ni wawili tu wanaojua, hawa wa hapa nyerere road wanatumia compounds zip kuipata coca??? Na wakati hawajui??? Au inashushwa na ndege na kujazwa ktk vyupa???
Tulia tu utajua.
 
Huu ni uzushi tu.

Sasa kama ni wawili tu wanaojua, hawa wa hapa nyerere road wanatumia compounds zip kuipata coca??? Na wakati hawajui??? Au inashushwa na ndege na kujazwa ktk vyupa???
Mkuu hawa wa huku kwetu huwa wanapewa ingredients au simplified recipe na maelezo ya jinsi kuchanganya na kupata soda, ni kama vile ambavyo tulikuwa tukitengeneza "juice cola" majumbani kwetu, unafuata tu maelezo rahisi kwenye label.
hiyo ambayo wanaijua hao watu wawili tu ni product formula. Ni very confidential na ina worth multi billions dollar hivyo siri hiyo haiwezi kutolewa kwa mtu mwengine yeyote kwani ni sawa na kugawa utajiri au kuuza soko lako kwa mtu mwingine.
Na kwa nyongeza tu ni kuwa watu hao hawaruhusiwi hata kupanda ndege moja kwa pamoja ili kuepuka kuwapoteza wote kwa pamoja endapo ikatokea bahati mbaya wakapata ajali.
Nadhani nimesaidia kidogo.
 
Heshima kwako mkuu, hii story niliwahi kuisikia nikiwa bado mdogo ila sikutilia maanani labda kwa sababu ya umri.

Ngoja tuendelee kusubiri wajuzi wa mambo!
 
mbona Pepsi INA Bonge LA ladha ukilinganisha na coca cola?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…