Unaifahamu vipi CocaCola?

Unaifahamu vipi CocaCola?

Mkuu hawa wa huku kwetu huwa wanapewa ingredients au simplified recipe na maelezo ya jinsi kuchanganya na kupata soda, ni kama vile ambavyo tulikuwa tukitengeneza "juice cola" majumbani kwetu, unafuata tu maelezo rahisi kwenye label.
hiyo ambayo wanaijua hao watu wawili tu ni product formula. Ni very confidential na ina worth multi billions dollar hivyo siri hiyo haiwezi kutolewa kwa mtu mwengine yeyote kwani ni sawa na kugawa utajiri au kuuza soko lako kwa mtu mwingine.
Na kwa nyongeza tu ni kuwa watu hao hawaruhusiwi hata kupanda ndege moja kwa pamoja ili kuepuka kuwapoteza wote kwa pamoja endapo ikatokea bahati mbaya wakapata ajali.
Nadhani nimesaidia kidogo.
Safi sana nikitaka watu kama nyie wa kuhirikishana mawazo,asante sana kaka haya mambo hakuna mtu anaeyajua yote ,na pia hii ya kupanda ndege ndio nimeipata tena kwako mkuu.
 
Formula ya kutengeneza syrup ya Coca cola ni SIRI KUU duniani.
Kila wakati wanatakiwa waifahamu wafanyakazi wawili tu, ambao hulindwa usiku na mchana, maisha yao yote.

Hawa washirika wengine[eg.Mzee Mengi] wao wanaletewa Coca cola ikiwa imeshatengenezwa na kupewa maagizo ya namna ya kuichanganya.

Kuna wakati serikali ya India ilitaka kupatiwa hiyo siri lakini Coca cola walikataa na kutishia kutokuuza vinywaji vyao India hadi serikali ilipotii.

Kuna mengi sana ya siri juu ya Coca cola lakini usitegemee kupata hizo siri popote.
 
Huu ni uzushi tu.

Sasa kama ni wawili tu wanaojua, hawa wa hapa nyerere road wanatumia compounds zip kuipata coca??? Na wakati hawajui??? Au inashushwa na ndege na kujazwa ktk vyupa???

Mkuu hao wanaletewa concentrates kutoka Merikani, jamaa wa Nyerere Rd. wao wachanganya maji na kujaza gesi ya carbondioxide na ku-bottle resultant homogenous solution, basi - hawajui siri ya formula inayo tengeneza concentrates.Ila rangi yake inatokana na sukari iliyo kaangwa lakini cha ziadi kilichopo kwenye mchanganyiko maalum no one knows save CocaCola family.
 
Mkuu hawa wa huku kwetu huwa wanapewa ingredients au simplified recipe na maelezo ya jinsi kuchanganya na kupata soda, ni kama vile ambavyo tulikuwa tukitengeneza "juice cola" majumbani kwetu, unafuata tu maelezo rahisi kwenye label.
hiyo ambayo wanaijua hao watu wawili tu ni product formula. Ni very confidential na ina worth multi billions dollar hivyo siri hiyo haiwezi kutolewa kwa mtu mwengine yeyote kwani ni sawa na kugawa utajiri au kuuza soko lako kwa mtu mwingine.
Na kwa nyongeza tu ni kuwa watu hao hawaruhusiwi hata kupanda ndege moja kwa pamoja ili kuepuka kuwapoteza wote kwa pamoja endapo ikatokea bahati mbaya wakapata ajali.
Nadhani nimesaidia kidogo.
Heeeh!!..Majina majina yao ni akina nani vile???
 
1. "Coca cola" ndio neno (jina) la tatu linalofahamika sana duniani baada maneno "Mungu" na "Helo" katika lugha zozote duniani

2. Kama njia ya marketing, wakati wa 2nd world war coca cola Atlanta walikuwa wanatoa soda bure askari wa front line (ikumbukwe hakuwa mshirika wa pande yoyote ya vita)
 
Kwa taarifa yako tu ni kuwa katika Patent zenye thamani kuliko zote duniani ya coca cola ndio namba moja,

pia ndio inayolindwa kuliko zote, ndio maana hadi leo hiyo ni siri kubwa sana, hao wengine akina pepsi na wenzake wanajaribu kutengeneza lakini hawawezi kutoa kama koka.

hiyo ni siri ya familia, na sio wanafamilia wote wanajua.
akifa baba anamuachia mtoto
Kuliko kuruka ruka mwambieni tu mwenye swali lake hamna jibu basi inatosha. Naona kila mja ansjizungusha zungusha wakati hoja yenyewe mkiikwepa, wabongo bwana!
 
Coca-Cola niijuayo mimi ilianzia huko Marekani kwenye jimbo la Georgia, hususan katika miji ya Columbus na Atlanta.

Mvumbuzi wake alikuwa ni Kanali John Pemberton, aliyekuwa mwanajeshi katika majeshi ya Confederate kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyowahi kutokea Marekani.

Na mpaka leo hii makao yake makuu yapo jijini Atlanta.

1481034045650.jpg

Pichani hapo ndo makao yake makuu.

Na kusema ukweli wazawa wa Atlanta na Georgia kwa ujumla, wanaipenda sana Coke. Kukuta wanakunywa vinywaji vya aina nyingine ni nadra.

Hata migahawa mingi Atlanta huwa wanauza bidhaa za Coca-Cola zaidi kuliko bidhaa za makampuni mengine.

World of Coca-Cola ni moja ya vivutio vikubwa katika jiji la Atlanta. Hapo ndo sehemu unayoweza kuonja kila aina ya kinywaji hicho iliyowahi kutengenezwa.

Kwa atakayeweza kutembelea Atlanta napendekeza apatembelee hapo world of Coca-Cola. Panavutia sana na panafundisha mengi kuhusu hicho kinywaji kilichoenea kwenye kila kona ya hii dunia.

USA baby [emoji631] [emoji631] [emoji631]

1481034132470.jpg
 
Formula ya kutengeneza syrup ya Coca cola ni SIRI KUU duniani.
Kila wakati wanatakiwa waifahamu wafanyakazi wawili tu, ambao hulindwa usiku na mchana, maisha yao yote.

Hawa washirika wengine[eg.Mzee Mengi] wao wanaletewa Coca cola ikiwa imeshatengenezwa na kupewa maagizo ya namna ya kuichanganya.

Kuna wakati serikali ya India ilitaka kupatiwa hiyo siri lakini Coca cola walikataa na kutishia kutokuuza vinywaji vyao India hadi serikali ilipotii.

Kuna mengi sana ya siri juu ya Coca cola lakini usitegemee kupata hizo siri popote.

Kuna mambo mengine yanajulikana lakini awayasemi miaka ya nyuma walikuwa wana adulterate na utomvu au majani wa Coca kutoka Amerika ya Kusini, hii illikuwa inawafanya wateja wapendelee kunywa CocaCola i.e inakufanya uwe na hamu ya kunywa CocaCola tu, nasikia mambo hayo waliachana nayo - lakini nakumbuka taste ya CocaCola ya miaka hiyo tofauti kabisa na CocaCola ya miaka ya hivi karibuni.
 
kutafuta siri za coca cola sio rahisi kiivi, yani kama kuwapekua wajenzi huru (freemanson)
 
Kuna mambo mengine yanajulikana lakini awayasemi miaka ya nyuma walikuwa wana adultate na utomvu au majani wa Coca kutoka Amerika ya Kusini hii illikuwa inawafanya wateja wapendelee kunywa CocaCola i.e inakufanya uwe na hamu ya kunywa CocaCola tu, nasikia mambo hayo waliachana nayo - lakini nakumbuka taste ya CocaCola ya miaka hiyo tofauti kabisa na CocaCola ya miaja ya hivi karibuni.
Ni kweli kabisa Mkuu unachosema.
Coca cola ya 1886 ni tofauti na ya 1920s ambayo ni tofauti na ya 1970s baada ya kufanyiwa marekebisho.

Coca cola wamewahi kutuhumiwa kutumia addictive material kwenye vinywaji vyao ili kuwafanya wanywaji wewe na addiction ya Coca cola, walikubali na baadae[1930s] waliondoa hayo material.
 
Formula ya kutengeneza syrup ya Coca cola ni SIRI KUU duniani.
Kila wakati wanatakiwa waifahamu wafanyakazi wawili tu, ambao hulindwa usiku na mchana, maisha yao yote.

Hawa washirika wengine[eg.Mzee Mengi] wao wanaletewa Coca cola ikiwa imeshatengenezwa na kupewa maagizo ya namna ya kuichanganya.

Kuna wakati serikali ya India ilitaka kupatiwa hiyo siri lakini Coca cola walikataa na kutishia kutokuuza vinywaji vyao India hadi serikali ilipotii.

Kuna mengi sana ya siri juu ya Coca cola lakini usitegemee kupata hizo siri popote.
Dah,hawa watu basi ni wasiri sana kama wanaweza kusitisha huduma yao kisa kutoa formula ya utengenezaji basi ni noma sana !
 
Watu wa maabara wa hivi Viwanda au Makampuni hutumia mchanganyiko Huo kwa taratibu na viwango vilivyowekwa na Coca-Cola na si vinginevyo
 
Kuna mambo mengine yanajulikana lakini awayasemi miaka ya nyuma walikuwa wana adulterate na utomvu au majani wa Coca kutoka Amerika ya Kusini, hii illikuwa inawafanya wateja wapendelee kunywa CocaCola i.e inakufanya uwe na hamu ya kunywa CocaCola tu, nasikia mambo hayo waliachana nayo - lakini nakumbuka taste ya CocaCola ya miaka hiyo tofauti kabisa na CocaCola ya miaka ya hivi karibuni.

Coca-Cola classic bado ipo sokoni....huwa naiona.

http://www.coca-colacompany.com/stories/coke-lore-new-coke
 
kutafuta siri za coca cola sio rahisi kiivi, yani kama kuwapekua wajenzi huru (freemanson)

Kwa watu walio bobea kwenye taaluma ya Kemia kama Dk.Magufuli awawezi kushindwa ku-analyse ingredients zilizotumika kutengeneza kijwaji cha CocaCola we sema labda wanaogopa kufunguliwa mashtaka.

CocaCola walipewaje patent bila ya ku-disclose formula yao? Wanalinda kivipi kitu ambacho hakijulikani kimetengenezwa kivipi - wavumbuzi si wanalinda formula zao au uvumbuzi wao usiwe duplicated na watu wengine bila ya kupata kibari maalumu kutoka kwao, sasa CocaCola wanatumia mbinu gani zaidi ya kutegemea usiri wa one of family member - ingekuwa siri za uchawi au uganga wa kienyeji sawa lakini kitu ambacho ni formula za kemia ambazo siku hizi kuna analyser za kibaini solute particles zenye saizi za nanometer!!

Hapo mimi ndiyo usiri wa masuala ya formula ya CocaCola uniacha na maswali mengi bila kupata majibu!!
 
Waku, suala la usiri wa formula ya coca cola sio conspiracy theory, ni suala halisi kabisa.

Katika ulimwengu wa 'ushushu wa kibiashara' kuna terminology maarufu inaitwa "Trade Secret"..

Trade secret - ni mbinu au namna ya ufanyaji jambo au mchakato au kifaa au formula au taarifa za siri zinazotumiwa na kampuni husika katika uendeshaji wake biashara au utengenezaji wa bidhaa zake na kuiweka kampuni hiyo katika nafasi nzuri ya kuwashinda washindani kibiashara.

Sasa mojawapo ya 'trade secret' zinazolindwa zaidi ulimwenguni ni viungo (ingredients) zinazotumika kuchanganywa kwenye kinywaji cha Coco Cola na kukifanya kuwa na ladha tofauti na vinywaji vingine vyote duniani. Viungo hivi vya siri vinavyo changanywa kwenye coca cola vinajulikana kama '7X'.

Sasa kampuni mama yenyewe ya coca cola huko marekani wao wanatengeza 'concentrate' yenye viungo hivi na kuwauzia 'bottlers' wenye vibali kutoka kwao kila pembe ya dunia ambao wao wanachanganya 'concentrate' hiyo na maji (carbonated water) na kuongeza kiwango cha sukari na kusindika kisha kuuza kwa walaji..

Ndio kusema kwa mfano, Bonite Bottlers ya Bw. Reginald Mengi wao wananunua concentrate kutoka makao makuu marekani na kuchanganya na maji na sukari na kuuza kwa walaji.
Mfumo huko hivyo Dunia nzima kila unapoiona coca cola.

Wapo 'majasusi' wa kibiashara kwa kushirikiana na wanasayansi wamefanikiwa kucrack hii ingredient lakini bado kitendawili kinabaki kuhusu viwango na namna ya uchanganyaji wa viuongo hivyo.

Ni wafanyakazi wachache sana (wengi husema watu wawili tu) kwa muda husika ndio hupewa siri ya ingredient ya '7X' inayotumika kutengeneza concentrate inayoipa coca cola ladha yake ambayo ni tofauti kabisa na vinywaji vingine vyote na siri hii inabakiwa kuwa moja ya 'Trade secret' inayolindwa zaidi.

The Bold.

Cc: minji, Nifah, kbosho, Adolph Hitler Jr
 
Waku, suala la usiri wa formula ya coca cola sio conspiracy theory, ni suala halisi kabisa.

Katika ulimwengu wa 'ushushu wa kibiashara' kuna terminology maarufu inaitwa "Trade Secret"..

Trade secret - ni mbinu au namna ya ufanyaji jambo au mchakato au kifaa au formula au taarifa za siri zinazotumiwa na kampuni husika katika uendeshaji wake biashara au utengenezaji wa bidhaa zake na kuiweka kampuni hiyo katika nafasi nzuri ya kuwashinda washindani kibiashara.

Sasa mojawapo ya 'trade secret' zinazolindwa zaidi ulimwenguni ni viungo (ingredients) zinazotumika kuchanganywa kwenye kinywaji cha Coco Cola na kukifanywa kuwa na ladha tofauti na vinywaji vingine vyote duniani. Viungo hivi vya siri vinavyo changanywa kwenye coca cola vinajulikana kama '7X'.

Sasa kampuni mama yenyewe ya coca cola huko marekani wao wanatengeza 'concentrate' yenye viungo hivi na kuwauzia 'bottlers' wenye vibali kutoka kwao kila pembe ya dunia ambao wao wanachanganya 'concentrate' hiyo na maji (carbonated water) na kuongeza kiwango cha sukari na kusindika kisha kuuza kwa walaji..

Ndio kusema kwa mfano, Bonite Bottlers ya Bw. Reginald Mengi wao wananunua concentrate kutoka makao makuu marekani na kuchanganya na maji na sukari na kuuza kwa walaji.
Mfumo huko hivyo Dunia nzima kila unapoiona coca cola.

Wapo 'majasusi' wa kibiashara kwa kushirikiana na wanasayansi wamefanikiwa kucrack hii ingredient lakini bado kitendawili kinabaki kuhusu viwango na namna ya uchanganyaji wa viuongo hivyo.

Ni wafanyakazi wachache sana (wengi husema watu wawili tu) kwa muda husika ndio hupewa siri ya ingredient ya '7X' inayotumika kutengeneza concentrate inayoipa coca cola ladha yake ambayo ni tofauti kabisa na vinywaji vingine vyote na siri hii inabakiwa kuwa moja ya 'Trade secret' inayolindwa zaidi.

The Bold.

Cc: minji, Nifah, kbosho, Adolph Hitler Jr
Kiukweli jamii forum ni darasa na pia ni chuo kisicho na mwanafunzi wote ni waalimu wanafunzana ,the bold (JF MASTER) asante kwa kunisogeza mbele na nimefahamu tena kingine hapa (7x)......
 
Back
Top Bottom