Unaifahamu vipi CocaCola?

Unaifahamu vipi CocaCola?

Kwa taarifa yako tu ni kuwa katika Patent zenye thamani kuliko zote duniani ya coca cola ndio namba moja,

pia ndio inayolindwa kuliko zote, ndio maana hadi leo hiyo ni siri kubwa sana, hao wengine akina pepsi na wenzake wanajaribu kutengeneza lakini hawawezi kutoa kama koka.

hiyo ni siri ya familia, na sio wanafamilia wote wanajua.
akifa baba anamuachia mtoto
Baba ndiye huchanganya?
 
ina alosto iyo noma,.nkiikosa sina ata raha
Arosto yake usipime,nilikuwa nakunywa tatu hadi nne kwa siku,niliteseka sana kuacha kuinywa,nilikuwa rafiki sana na wenye viosk(maduka ya mtaani),
 
Waku, suala la usiri wa formula ya coca cola sio conspiracy theory, ni suala halisi kabisa.


Katika ulimwengu wa 'ushushu wa kibiashara' kuna terminology maarufu inaitwa "Trade Secret"..

Trade secret - ni mbinu au namna ya ufanyaji jambo au mchakato au kifaa au formula au taarifa za siri zinazotumiwa na kampuni husika katika uendeshaji wake biashara au utengenezaji wa bidhaa zake na kuiweka kampuni hiyo katika nafasi nzuri ya kuwashinda washindani kibiashara.

Sasa mojawapo ya 'trade secret' zinazolindwa zaidi ulimwenguni ni viungo (ingredients) zinazotumika kuchanganywa kwenye kinywaji cha Coco Cola na kukifanya kuwa na ladha tofauti na vinywaji vingine vyote duniani. Viungo hivi vya siri vinavyo changanywa kwenye coca cola vinajulikana kama '7X'.

Sasa kampuni mama yenyewe ya coca cola huko marekani wao wanatengeza 'concentrate' yenye viungo hivi na kuwauzia 'bottlers' wenye vibali kutoka kwao kila pembe ya dunia ambao wao wanachanganya 'concentrate' hiyo na maji (carbonated water) na kuongeza kiwango cha sukari na kusindika kisha kuuza kwa walaji..

Ndio kusema kwa mfano, Bonite Bottlers ya Bw. Reginald Mengi wao wananunua concentrate kutoka makao makuu marekani na kuchanganya na maji na sukari na kuuza kwa walaji.
Mfumo huko hivyo Dunia nzima kila unapoiona coca cola.

Wapo 'majasusi' wa kibiashara kwa kushirikiana na wanasayansi wamefanikiwa kucrack hii ingredient lakini bado kitendawili kinabaki kuhusu viwango na namna ya uchanganyaji wa viuongo hivyo.

Ni wafanyakazi wachache sana (wengi husema watu wawili tu) kwa muda husika ndio hupewa siri ya ingredient ya '7X' inayotumika kutengeneza concentrate inayoipa coca cola ladha yake ambayo ni tofauti kabisa na vinywaji vingine vyote na siri hii inabakiwa kuwa moja ya 'Trade secret' inayolindwa zaidi.

The Bold.


Cc: minji, Nifah, kbosho, Adolph Hitler Jr
wajenzi huru mkuu sidhani kama mikono yao imekosekana hapo....
shukrani bhana....
 
Huu ni uzushi tu.

Sasa kama ni wawili tu wanaojua, hawa wa hapa nyerere road wanatumia compounds zip kuipata coca??? Na wakati hawajui??? Au inashushwa na ndege na kujazwa ktk vyupa???
Wanaamanisaha ile.flavour mkuu
 
Unachosema ni kweli kabisa.

Coca-Cola za Atlanta ni tofauti kabisa na Coke za Bonite bottlers.

Hata Fanta orange za bongo ziko tofauti na zilizopo huko zilipoanzia.

Huenda labda hao bottlers huwa wana leeway flani kuendana na soko wanalohudumia.
Yeah, nakumbuka mwalimu wangu wa sekondari alikua mzungu mmarekani alipenda sana coke ya Tanzania nilivomuuliza kuwa zinatofauti? alinijibu kuwa hii ya huku hutumia real sugar ila kwao hutumia corn sugar
 
Hiyo habali y sili yawatu wawili niuongo uliokomaa kabisa
 
Ndio hii ambayo Baba Latifa huwa anasemaga hakamatiki akionja msisimko?
 
Ni kweli kabisa Mkuu unachosema.
Coca cola ya 1886 ni tofauti na ya 1920s ambayo ni tofauti na ya 1970s baada ya kufanyiwa marekebisho.

Coca cola wamewahi kutuhumiwa kutumia addictive material kwenye vinywaji vyao ili kuwafanya wanywaji wewe na addiction ya Coca cola, walikubali na baadae[1930s] waliondoa hayo material.
Duh!
nani amethibitisha kua ya mwaka 1886 huko nitofauti na ya mwaka 1870s halafu na ya 200s nitofauti naamini hata huyo mtu ange kuwepo mate yake yasinge kumbuka hiyo ladha tena
 
Duh!
nani amethibitisha kua ya mwaka 1886 huko nitofauti na ya mwaka 1870s halafu na ya 200s nitofauti naamini hata huyo mtu ange kuwepo mate yake yasinge kumbuka hiyo ladha tena
Coca cola wenyewe walieleza kwamba miaka hiyo walibadilisha ingredients zenye kuathiri ladha ya Coca cola.
 
Mkuu hawa wa huku kwetu huwa wanapewa ingredients au simplified recipe na maelezo ya jinsi kuchanganya na kupata soda, ni kama vile ambavyo tulikuwa tukitengeneza "juice cola" majumbani kwetu, unafuata tu maelezo rahisi kwenye label.
hiyo ambayo wanaijua hao watu wawili tu ni product formula. Ni very confidential na ina worth multi billions dollar hivyo siri hiyo haiwezi kutolewa kwa mtu mwengine yeyote kwani ni sawa na kugawa utajiri au kuuza soko lako kwa mtu mwingine.
Na kwa nyongeza tu ni kuwa watu hao hawaruhusiwi hata kupanda ndege moja kwa pamoja ili kuepuka kuwapoteza wote kwa pamoja endapo ikatokea bahati mbaya wakapata ajali.
Nadhani nimesaidia kidogo.
Ni watu gani hao
 
Coca-Cola ni kinywaji ambacho sio rafiki kabisa kwa afya zetu,hii sio siri tena.Wanaoendelea kunywa Coca-Cola,Pepsi na vinywaji vinavyofanana na hivyo ni wale wasiojua contents zake au wenye msimamo wa kwamba inzi kufia kwenye kidonda ni sawa.

Kama unataka kujua contents za Coca-Cola tafadhali google hapa,"What chemicals are really in Coca-Cola's Coke Soda.?"
Ulipo anza kusema COCA SIO KINYWAJI RAFIKI KWA AFYA ZETU nikajua unaleta sababu ili kutu saidia jibu na kutuokoa afya zetu wewe unasema tuende google. google?!
 
Diamond Platnumz-Taste The Feeling Anthem(Coca-Cola).
22a2d88e14f7ed96df39a602f90a2f70.jpg

Nasikia furaha
Moyo wangu unapoanza tukiwa wawili
Ninayempenda sikatai ni wewe
Na hili joto la Dar
Tupate ya baridi Coca-cola tupozeshe na miili
Tuzidi furahi milele
Tena iwe hivi pamoja
Wewe na mi milele
Tuwe free
Wajue kwamba....
Sikamatiki nikionja msisimko
Hakuna cha kunishusha down
Sikamatiki nikionja msisimko
Oh!tena furaha
Namshukuru Mola we kunipata Mimi
Tujivinjari ukiwa name kwa ufukwe
Oh! tena bahari imejaa
Niongezew Coca-cola Nipige mbizi hadi chini
Tafadhali moyo wangu usiutupe
Tena iwe hivi pamoja
We nami milele
Tuwe free
Wajue kwamba....
Sikamatiki nikionja msisimko
Hakuna wakunishusha down
Sikamatiki nikionja msisimko
Hakuna wakunishusha down
Jua linapozama
Nyota zinazagaa
Shika nikushike mama
Tuzidi fika mbali
Tupate raha ya milele
Pamoja,Mimi na wewe
Tupate raha ya milele
Pamoja,Mimi na wewe
Sikamatiki nikionja msisimko
Hakuna wa kunishusha down
Sikamatiki nikionja msisimko
Hakuna wakunishusha down
Sikamatiki nikionja msisimko
Hakuna wa kunishusha down
Sikamatiki nikionja msisimko
Hakuna wa kunishusha down.
 
Aisee coke, ukipata baada ya kula msosi Wa moto...hutajutia
 
siri ya mpishi ni ngumu kuijua , sababu kuna mama anapika chakula huku kwetu watu wanakula sana na wanajaa sana, sasa kila mtu analake la kusema kuhusu siri za huyu mama lakini ukweli anaujua mwenyewe
 
Yaani mkuu unataka utafuniwe kila kitu,hapana, that is too much.Acha uvivu mkuu.Ni lazima WaTZ tujenge tabia ya kusoma.Or else tutaendelea kuwa mbumbu na jamaa wataendelea kufanya vitu vyao bila sisi kujua.
Ulipo anza kusema COCA SIO KINYWAJI RAFIKI KWA AFYA ZETU nikajua unaleta sababu ili kutu saidia jibu na kutuokoa afya zetu wewe unasema tuende google. google?!
 
Back
Top Bottom