Chuma ulete zipo za mitindo mingi tu, kuna ambao wanakuja na kipande tu cha karatasi ila wewe itaiona kama noti ya tsh 10,000/=, kwa hiyo hapa atakuwa amechukua bidhaa bure na chenji ya bure, pia kuna wengine wanachukua bidhaa bila ya kununua, yaani mchawi yule anapita ktk biashara yako anachagua chagua kisha hanunui anaacha, kumbe wakati ule anashika shika ndio anabeba bidhaa wewe hujui, na pia kuna wengine wanatumia mandondocha kuja kukusanya ushuru katika kila biashara ila wewe huwaoni, hizo ni baadhi tu ya njia wanazotumia. Ila ukiwasikiliza hao wakimbizi watakwambia hakuna kitu kama hicho