Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Waandishi wa filamu walikuwa na vionjo vyao katika maisha ya mateso ambayo mtazamaji anaweza jikuta anamwaga machozi wakati anaangalia filamu.
Hali hii ilikuwepo hata Tanzania kipindi filamu zinafanya vizuri kuliko sasa, filamu kama Dunia Hadaa, Safari, nk zilikuwa na vionjo vya kuteka hisia za mtazamaji.
Baadae wanaijeria wakatushinda kwenye filamu za sampuli hiyo, wakawa wanaandika stori ambazo kweli ukiangalia inakuonyesha ubaya wa watu, ziko filamu kama Orphan, Afro, nk.
Wahindi na wazungu nao wanazakwao ambazo ukiangalia unatekwa kihisia kiasi cha kuona mchozi unaweza kukaribia kutoka. Na wengine walikuwa wanalia moja kwa moja kwa kuguswa tu na stori ya filamu husika.
Je una filamu ipi unayoikumbuka imewahi kujaribu kuudondosha mchozi wako?