Unaikumbuka timu hii ya Taifa ya Uholanzi

Hawa ndo vijana wa zamani. Wazee wa jf.
 
Ni fainali ambayo Brazil alikuja kukutana na France katika Final, ambapo Zinadine Zidane "alijitwisha mtu kwa kichwa"
 
Edgar Davies
Yeye Aaron winter na crelence seedorf wazaliwa wa Paramaribo hawa walikuwa chachu ya soka bora la club ya ajax japo timu yao ya taifa walikuwa wakienda sana nusu fainali isipokuwa kaka zao kina guilt ndio walibahatika kuonyesha kwapa mwaka wa 1988. Winston bogade kina Michael raizger ilikuwa unatizama the orange kweli.
 
seedorf kaondoka na utamu wake ac milan nilikuwa namuona umri umeenda lakin anapiga mpira wa maana
 
seedorf kaondoka na utamu wake ac milan nilikuwa namuona umri umeenda lakin anapiga mpira wa maana
Ndio wale maaskari wanakufa na bunduki zao mzaliwa wa Suriname huyu ilipo huko amerika ya kusini lakini ni koloni la wadachi sera ya kuwachukua na kuwapeleka udachini ndio ilisaidia kuokoa vipaji vya magwiji hawa. Seedorf alikuwa ana tabasamu tu akiwa uwanjani na ukiangalia kwa umakini utauona mpira ukifika kwake nao unatabasamu na kutii sheria.
 
Katika kitu kinaniboa kwenye soka ni majeruhi.. marco van basten aliuacha mpira mapema kisa majeruhi..

Marco reus tunakosa kuona ubora wake, jack wilshere n.k(japo ni nje ya mada)
Mchezaji akishakuwa prone to injury, huwa ndio mwisho wa kipaji mara nyingi, too bad [emoji22]
 
mkuu asante umenikumbusha mbali sana
1998 semi final moja kali sana wakicheza na brazil ni kama namuona de lima anamvyomtoka frank de boer na kufunga moja ya magoli mazuri kabisa ambayo nimepata kuyaona
Fenomeno.. chief huyu kiumbe ni nux, dunia ya sasa tunakosa striker kama hii, mpira mguuni ulikuwepo wa kutosha udambwi udambwi na umate wake ulikuwemo, hebu fikiria mtu aujue mpira kama neymar au gaucho kisha alijue goli kama lewandowski au cr7, ndio de lima mmoja, pamoja na kufunga jamaa alikuwa na skills si mchezo, ana rekod ya mabao 88 kumchukua mpaka kipa..

Nje ya mada, nisameheni bure tuu.
 
Seedorf alikuwa anaujua mpira hasa, sijui nimlinganishe na nani sasa, alikuwa anaisukuma tim juu vizur mnoo, anafukia mashimo, anadrible mpira maridadi huku akilamba vyenga lain, mzuri kwa pasi..
 



Pia hiki kikosi kilikuwa kizuri sana including Marco Van Basten, Ruud Gullit, Ronald Koeman, Danny Blind, Aaron Winter, Frank Rijkaard, Vanenburg, Wouters and Johnny Bosman. Coached by the legendary coach Rinus Michels.
Kwangu mimi hiki kilikuwa kikosi bora kuliko kile cha akina Davids, de Boer, Cluivert nk
 
Kwangu mimi hiki kilikuwa kikosi bora kuliko kile cha akina Davids, de Boer, Cluivert nk
Waweza kuwa sahihi kwani kilifika kilele cha mafanikio ukiachilia mbali world cup ya mwaka 1974 ya akina Johan cruffy ambao waliishia final na kufungwa mbili moja na ujerumani magharibi kisha world cup iliyofuatia mwaka 78 pia wakatinga final na kupigwa 3 -1na wenyeji Argentina basi una haki zote za kukiita hiki kikosi kilikuwa bora kwa maana ya mafanikio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…