Unaikumbuka timu hii ya Taifa ya Uholanzi

Goli bora kuwahi kufungwa ndani ya miaka 25 ya EPL.
Touch Turn and Finish.
Arsenal halali yenu kupata tabu sasa hivi mlisha pata raha sana zamani.
 
LVG ni father of modern FOOTBALL, style yake sio kama ya kina Rinus na cryuff, japo wengi wanawafananisha. Angalia interview nyingi za Cryuff ana mcriticise LVG kwa style yake na anasema haipendi. Pia LVG aliondoka Barcelona sababu alitaka kuanzisha culture yake na walikuwa wakimpinga sana, kama mfumo wake ni sawa na uliozoeleka barca wasingempinga
Louis van Gaal - Wikipedia

LVG ana hadi long balls (Fellaini)

LVG yeye ni Tactical zaidi sio pasi tu, kipindi cha man U tuliona 3-5-2, kisha baadae ikaja 4-4-2 diamond, alivyomdrop di maria ikaja 4-1-4-1 kisha msimu wa mwisho 4-2-3-1, mzee wa philosophy kila timu ana mfumo wake.

huyu jamaa hata timu iwe mbovu vipi na wachezaji wamekaa muda mfupi anaweza fanya wonders, uholanzi hii ilioshindwa fuzu Euro na world cup jamaa aliwapeleka nusu, beki martin Indi, na vlaar. msimu wa mwisho Man U alikuwa anaokota tu academy, kina CBJ, Rashford, Mc Nair, TFM, etc na walikuwa wanafanya vizuri kuliko watu wazima.

wakati mifumo ya kina Cryuff na pep inataka wachezaji wazuri wanaoweza ku adapt mfumo,
 
Huwezi kuiweka kando club ya ajax Amsterdam na mafanikio ya timu au kung'ara kwa the orange maana vipaji lukuki vimepita hapo toka mkongwe johan cruffy mpaka blind baba na mwana Kluivert mwanae Justin yupo pale mapacha familia ya de Boer aah pana mdachi ila mkongo kwa kuzaliwa kizito "kiki "musampa wamepita hapo achilia mbali wanaigeria watatu George finidi nwanko kanu na tijan babangida wamepata kikiwakilisha kikosi cha ajax. Pana waqt huwaza miongoni mwa timu bora miaka ya nyuma the orange ilikuwa inatamba ila sijui walikuwa na gundu (jokes )hawa kina suarez ibrahomavic walikuta zama za ajax kama zimekwisha vile.
 
Asante kwa mchango murua kabisa
 
Tupac je?
 
Mkuu jamaa walikuwa na kikosi kizuri hawakuwa na bahati.

Rejea Brazil ya kombe la dunia mwaka 1982, ni moja kati ya vikosi bora vya wakati wote lakini hawakutwaa taji lolote licha kutandaza soka la hali ya juu!

Yes. Mpira ni bahati pia. Hawa jamaa walikua fit karibu kila mwaka lakini 'mungu wa bahati' hakuwa kwenye ardhi yao
 
Mimi nasemaga Uhalanzi ni Brazil ya ulaya, haijawahi kukaukiwa vipaji tangu soka linaanzishwa!

Huwa wanatoaga majembe kila zama, tangu enzi za Cryfu,Rud guilt, van basteen,Denis Berkamp,Overmars,Kluivert,Robben.

Sema nayo ni ill-fate timu haijawahi kuwa na bahati na Hizi zama za akina Depay ndio wamefulia kabisa wamekosa mpaka EURO iliyokuwa na timu za ajabu kama New Zealand
 
genious ni Huyu


kakitengeneza yeye hicho kikosi,

alivyotoka hapo akaenda kutengeneza spain,

alivyotoka hapo akatengeneza kidogo kwao kisha akamalizia kutengeneza ujerumani.
Huyu Mzee heshima yake ilichafuka alivyokubali kuifundisha man u halafu akaanza kulazimisha mpira wa kidutch
 
Kwa kipindi hicho ulicho ainisha kuanzia johan cruffy mpaka kina Kluivert naweza kukuunga mkono ila baada ya hapo wamekuwa wakipata watu wawili watatu tu mfano kipindi cha kina van perse akawepo na wisley pamoja na van da vart basi sasa kwa mtiririko huo huwezi kusema kuwa wana gundu au nuksi lakini kipindi kile unakuta pana wachezaji zaidi ya saba watamu Kluivert pale seedorf hapa davida kule raizger pale winter kule blind hapo winston bogade yaani ilikuwa una uhakika wa kufika mwisho na wakotolewa ndio unasema wana nuksi.
 
Huyu Mzee heshima yake ilichafuka alivyokubali kuifundisha man u halafu akaanza kulazimisha mpira wa kidutch
hata Man U mkuu alikuwa akidrop mastaa Timu inashinda. Nakumbuka msimu wa kwanza mwishoni aliwadrop kina Falcao, RVP, Di maria na wengineo timu akawaeka kina young, Fellaini, Herrera na wengine wasio na Ego watu wakasema Timu haiendi hata UEFA mechi zimebaki kama 8 na ratiba kuna spurs, liverpool na Man city mfulululizo. lakini akawapiga wote tena goli 3 kupanda,

Hata mwisho wa Career yake walipoanza kucheza kina Rashford, Lingard alivyopona, martial na watoto wengine timu ilikuwa inacheza vizuri kuliko wakicheza watu wazima kina Rooney.
 

Unajua ni vigumu sana kumbadilisha watu kama falcao au dimaria kucheza mpira aliokuwa ameuzoea na kumpeleka kwenye mpira wa kidutch! Hao akina Lingard na Herrera ilikuwa ni rahisi kucheza kwa kufuata maelekezo ya Van gal sababu ya uchanga na upendeleo wa ghafla aliowapa na ndio maana wakafanya vizuri. Pamoja na hivyo alivyotoka nje ya falsafa ya soka LA man u ndio kulimfanya asidumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…