Unaionaje Gen Z ya Tanzania?

Unaionaje Gen Z ya Tanzania?

Maana ya Gen Z.
Kwa mujibu vyanzo vya mtandaoni, Gen Z ni vijana waliozaliwa kuanzia mwishoni mwa miaka 1990. Pia wanafahamika kama kizazi cha kidijitali kwa sababu walizaliwa wakati mtandao ndio umeanza kuchipukia.

Hiki ndicho kizazi kinachosadikika kukuza mtandao ndio maana kimepewa jina Gen Z ambalo lina maana ya: Gen=Generation. Z=Zoomer. Hivyo, kijana aliyezaliwa katika hicho anaweza kuwa na miaka 26-28

Gen Z ya Tanzania!

Tumeona au kusikia huko Kenya Gen Z yao imeandaa maandamano bila kujali ukabila dhidi ya mswaada wa kodi na wamefanikiwa kwa sababu rais hajasaini na ameurudisha bungeni. Gen Z ya Kenya imekuwa kitu kimoja kupigania mustakabali wao.

Mimi nawauliza wajumbe kila mmoja atathmini kwa kurejea Gen Z ya Tanzania iliyopo mtaani na mtandaoni;

1. Je, Gen Z ya Tanzania ina uwezo wa kupigania haki zao?

2. Je, Gen Z ya Tanzania inafuatilia mambo yanayohusu nchi yao?

3. Je, Gen Z ya Tanzania inauwezo wa kujisimamia katika maisha na kufika mbali au ni mpaka wapewe mwongozo na wazazi au walezi?

4. Je, Gen Z ya Tanzania inatumia muda mwingi kufanya nini katika maisha yao ya kila siku?

5. Je, Gen Z ya Tanzania inaweza kupewa madaraka mbalimbali na wakafanya vizuri?

6.Je, Gen Z ya Tanzania ni ya moto au imepoa? Kama imepoa, ni nini kimesababisha kuwa hivi?

Ikumbukwe, Gen Z ndio baadae wanakuwa watu wazima. Je, Gen Z ya Tanzania inaandaliwaje baadae kuwa watu wazima na kuongoza nchi baada ya wale wazee wajamaa wote kuisha?
Kabla ya kujadili hoja yako, lazima uelewe kuwa Tz hakuna Gen-Z, bali kuna Gen-C(Generation chawa) mithili ya mazombie yasiyojitambua.

Watawala wanavyocheza na mali za Taifa kwa manufaa ya matumbo yao, ulitegemea kukapatikana mtu akashadadia ama kushabikia utawala huu na vijana wengine kukaa kimya?

Kukaa kimya huwa ni kuunga mkono!

Kuna mtu hata kwa kejeli angeliweza kusema mi5 tena na vijana wakanyamaza?

Kuna mtu angelisema habari za kuupiga mwingi na vijana wote, nchi nzima wakanyamaza gwaaa!

Vijana wa Tz ni generation dhaifu sana iliyojaa vijana wabinafsi na waoga.

Generarion-Z, ni nembo ya vijana wanaojielewa na kujitambua kwa sababu wanajua kuwa kesho ya taifa lao ipo mikononi mwao na ndiyo maisha yao dhahiri.

Sasa akijitokeza kiongozi asiyefaa kwa ulaghai na uzabizabina, gen Z wanauwezo wa kumwajibisha kuokoa future zao, si hawa wa kwetu, thubutuu!

Tofauti na Generation-C ambayo ni ya vijana wanaopenda kubet, kushabikia mipira na kula bata bilsbkutaka kufanya kazi, hauwezi hata siku moja kuwafananisha na generation -Z wenye malengo na maono tofauti.
 
Maana ya Gen Z.
Kwa mujibu vyanzo vya mtandaoni, Gen Z ni vijana waliozaliwa kuanzia mwishoni mwa miaka 1990. Pia wanafahamika kama kizazi cha kidijitali kwa sababu walizaliwa wakati mtandao ndio umeanza kuchipukia.

Hiki ndicho kizazi kinachosadikika kukuza mtandao ndio maana kimepewa jina Gen Z ambalo lina maana ya: Gen=Generation. Z=Zoomer. Hivyo, kijana aliyezaliwa katika hicho anaweza kuwa na miaka 26-28

Gen Z ya Tanzania!

Tumeona au kusikia huko Kenya Gen Z yao imeandaa maandamano bila kujali ukabila dhidi ya mswaada wa kodi na wamefanikiwa kwa sababu rais hajasaini na ameurudisha bungeni. Gen Z ya Kenya imekuwa kitu kimoja kupigania mustakabali wao.

Pia soma: Kule Kenya Gen Z wanadili na Wakusanya Kodi wa Kenya, Tanzania tunadili na Mbowe ambaye hakusanyi kodi

Mimi nawauliza wajumbe kila mmoja atathmini kwa kurejea Gen Z ya Tanzania iliyopo mtaani na mtandaoni;

1. Je, Gen Z ya Tanzania ina uwezo wa kupigania haki zao?

2. Je, Gen Z ya Tanzania inafuatilia mambo yanayohusu nchi yao?

3. Je, Gen Z ya Tanzania inauwezo wa kujisimamia katika maisha na kufika mbali au ni mpaka wapewe mwongozo na wazazi au walezi?

4. Je, Gen Z ya Tanzania inatumia muda mwingi kufanya nini katika maisha yao ya kila siku?

5. Je, Gen Z ya Tanzania inaweza kupewa madaraka mbalimbali na wakafanya vizuri?

6.Je, Gen Z ya Tanzania ni ya moto au imepoa? Kama imepoa, ni nini kimesababisha kuwa hivi?

Ikumbukwe, Gen Z ndio baadae wanakuwa watu wazima. Je, Gen Z ya Tanzania inaandaliwaje baadae kuwa watu wazima na kuongoza nchi baada ya wale wazee wajamaa wote kuisha?
GenZ yetu ni zao letu

Keyboard warriors
 
Back
Top Bottom