Unaishiwa Cha Kuongea Na Mazungumzo Yanakua Mafupi Ukiwa Na Mwanamke? Fuata Muongozo Huu...

Unaishiwa Cha Kuongea Na Mazungumzo Yanakua Mafupi Ukiwa Na Mwanamke? Fuata Muongozo Huu...

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Aidha unaongea na mwanamke kwa mara ya kwanza au tayari upo na mwanamke lakini mazungumzo yenu yanakua kama mahojiano ya kutafuta kazi/ polisi hakuna hisia zozote, hakuna kuchombezana na we mwenyewe unaona haufurahii mazungumzo. Hivi ndivyo unaweza na kuyabadilisha kuwa mazungumzo yenye raha.

Yaongoze mazungumzo. Usije ukakaa na mwanamke ukasubiri ye ndo awe kiongozi. Muvi nyingi zinaonesha ivo lakini haifanyi kazi kwenye maisha halisi. Wewe ndo uongoze mazungumzo kuelekea utakako, mazungumzo utakayo wewe. Wanawake wanapenda kuwa na watu wanaowaongoza. Ukiamuachia mwanamke hili jukumu yeye atakuongoza kwenye urafiki, na atakuweka wewe kama rafiki yake tu (sio lengo lako hili).

Jibu maswali kwa stori badala ya jibu la moja kwa moja. Wanawake wanapenda taarifa hasa ikiwa na vitu vingi. Ukisimulia stori unakua unaweka mada tofauti tofauti hivyo inakua rahisi kwa mwanamke kuuliza maswali zaidi na kupata mazungumzo marefu kuliko kumuacha ayaongoze mazungumzo yeye. Mfano, unaulizwa unapenda chakula gani, badala ya kusema pilau na kubaki hakuna kitu, toa stori.

Mfano, kuna siku nilikua safarini kwenda Tanga, kuna shughuli tulikua tunaenda kufanya, kuna hoteli tulisimama wenzangu wakaenda kula ila mi nikawasindikiza tu, yule mhudumu alipoona sili akaniuliza na nikamuambia naogopa vyakula vya njiani, akaanza kunishawishi, akanishauri pilau na akaniambia kiasi cha kula mpaka nikashawishika, aisee sikuwahi kula pilau kama hilo na sikuumwa tumbo safari nzima, tangu siku hiyo nina hamu na pilau tu. Apo umetoa mada tofauti za kuendeleza mazungumzo, umeenda Tanga, ulikutana tena na huyo mhudumu?, mara ya mwisho umekula pilau lini tena, mlienda kwa shughuli gani. Lakini ungesema tu pilau kusingekua na chochote cha kuchochea mazungumzo.

Kuwa mcheshi. Sio lazima uwe kama MC Pilipili ila utengeneze hali ya kumfanya afurahi na kutabasamu. Njia rahisi ni kutoa stori yako ya utotoni ambayo we mwenyewe ukiikumbuka unacheka na pia anayoweza kuielewa kwa kuwa ni vitu vinavyojulikana sana. Mfano, labda uliwahi kumdanganya mzazi wako siku ya wajinga alafu ukaishia kuchapwa, au jinsi ulivojikojolea kwa kuogopa kuchapwa na mwalimu.

Tengeneza hali ya sisi (wewe na mwanamke). Tumia maneno yenye, tuna…, tuta… sana zaidi ya mimi na wewe. Hii inamfanya ajione yupo katika maisha yako hivyo inakua rahisi na yeye pia kuchangia.

Ongelea mambo ya baadaye. kama we ni mdogo au hauna maisha ya kuvutia sana au hauna hela ya kuishi maisha ya kukuvutia we mwenyewe hilo lisiwe kikwazo. Cha muhimu uwe na malengo. Unaweza zungumzia vitu unavotaka kuvifanya, sehemu unayotaka kwenda, unataka uwe nani lakini hauna haja ya kudanganya, au kumdanganya utampeleka Dubai. Ubaya wa uongo ni kutengeneza sumu ya kwenye mahusiano.
Toa stori ya kwanini unataka ivo, au kinachokusukuma (motisha).

Epuka kuuliza maswali yanayohitaji jibu la ndio/ hapana. Mfano, unapenda kusafiri? Aidha utajibiwa ndio au hapana. Njia ni nzuri ya kuuliza maswali yanayohitaji jibu la kuelezea. Mfano, sehemu gani ushawahi kusafiri ikakuvutia? Kwanini?. Njia nzuri zaidi ni kuanza kutoa wewe stori ya sehemu uliyosafiri na ukaifurahia alafu muulize na yeye ilikuaje stori yake. Hapa unakua kiongozi na kumuongoza kile mnachotaka kukizungumzia na jinsi ya kuzungumzia.

Ongea kwa kujiamini na ukiwa na tabasamu. Mara nyingi haijalishi unasema nini, kwa mwanamke inajalisha zaidi jinsi unavyokisema. Pia unapuliza uliza kwa kujiamini. Wanawake wanapenda kuwa na watu wanaojiamini, achana na zile muvi za Hollywood zinazoonyesha mwanaume anaongea kwa kujing’atang’ata.

Ndio maana katika kundi la infinite kiumeni ndio sehemu pekee utakayojifunza na wanaume wengine ili kuwa bora na kujiamini zaidi katika mahusiano na mapenzi na mwanamke unayehitaji kujenga naye maisha.
 
Wanawake hawana formula mkuu, wapo ambao hawapendi swali lenye jibu fupi liwe na maelezo mengiiii...wanaona ni mtu unayejifanya mjuaji, haupo focused n.k

Muhimu ni kujua upo na mwanamke yupi na uongee vipi...
 
Ongea ukweli wako “honesty” pasipo kuogopa na kwa sentesi iliyonyooka. Muache yeye afanye maamuzi.

Usije jaribu kuingia kwenye kichwa chake ukajipa maamuzi, like naona naelekea kitomba kumbe yeye ana changamsha genge tuu. Unafanya kitu fulani unashangaa zero response.

Weka hofu pembeni, ongea, zungumza, uliza
 
[emoji848]
1358609189.jpg
 
Na hawa wanawake wanaojibu wa ok au sawa hata uwaongeleshe na kuwapigisha story hawacheck wala kuchangia zaidi ya ok au sawa . Hawa ni jamii ya viumbe gani
 
Wanawake hawana formula mkuu, wapo ambao hawapendi swali lenye jibu fupi liwe na maelezo mengiiii...wanaona ni mtu unayejifanya mjuaji, haupo focused n.k

Muhimu ni kujua upo na mwanamke yupi na uongee vipi...
Ndugu Mwandishi anatafuta formula na wakati kutongoza sio sayansi ni sanaa 😂
 
Wanawake hawana formula mkuu, wapo ambao hawapendi swali lenye jibu fupi liwe na maelezo mengiiii...wanaona ni mtu unayejifanya mjuaji, haupo focused n.k

Muhimu ni kujua upo na mwanamke yupi na uongee vipi...
Mimi ni mtu wa story nyingi hicho ulichosema ni true
 
Yote haya ili iweje mdogo wangu?

Bagosha!

Na kama una hela yeye mwenyewe ndo atakuwa anaanzisha topiki. Hata vita vya Ukraine mtavichambua kwa kina tu kabla hamjahamia kwenye tozo za Mwigulu na plea bargaining ya jaji Biswalo [emoji16][emoji16][emoji16]
Teh 😂😂 teh teh teh teh 😂😂😂 dah!...nyie jamaa mna vituko
 
Back
Top Bottom