Unajenga nyumba utakula hiyo nyumba!?

Aliyeleta huu uzi ni
Muha tu, kwani kigoma wivu ndio nyumbani kwao. Umenikera kweli, unataka
akaishi kichakani au akanunue toyo/prado ndio uridhike?

hata ukiniita red hindu lakini huo ndo ukweli tatizo lako wewe ni muoga wa maisha.
 
Mi ninachojua kwa sasa naitwa Baba mwenye nyumba.

Sent from my LT26i using Tapatalk 2
 
duuh! mtoa mada atakuwa alisoma la saba B

JIPANGE MKUBWA, MTU AMBAYE HANA KWAKE NI MTUMWA,!
 
Haina haja ya kulumbana sana, kama mleta sred anaamini ana uwezo wa kufanya biashara halali ya kumzalishia fedha ya kutosha sioni kwa nini aangaike kujenga sasa hivi wakati akiwa na pesa ya kutosha atajenga hata masaki.

Mfano wa watu aliowatolea, ni wa watu wenye vipato vya kawaida, na kutokana na adha za kupanga watu wanaona bora ajenge kwanza kuwa na mali isiyoshuka thamani. Sio kila mtu anaweza biashara.

Mwisho wa siku inategemea vipaumbele vya mtu mmoja mmoja, mwingine yuko radhi afe kwenye nyumba ya kupanga lakini ana gari anayoitaka. Ila kila unachokifanya sasa hivi kitagusa maisha yako ya baadae kwa uzuri au ubaya.

Kama hauko vizuri kwenye biashara, nunua kiwanja sasa hivi itafika kipindi hata sio mabwepande wala bagamoyo, hapatakamatika.

Hapa kwetu mikopo ya nyumba kwa watu wa kawaida ni vigumu sana kupata kutokana na vigezo vyake.

Mtazamo wangu binafsi, nyumba inaleta utulivu wa akili kujipanga na mambo mengine ya maendeleo.
 

Mbona mnaigeuza JF kijiwe cha uongo? Nchi gani iliyoendela ambayo watu wake wanakatazwa kujenga kwa pesa zao?
 

Unapata wapi kuzungumza mambo usiyoyajua kabisa. Jifunze kufanya utafiti angalau kidogo kabla ya kufungua mdomo wako mbele ya watu wazima...
 
Mbona mnaigeuza JF kijiwe cha uongo? Nchi gani iliyoendela ambayo watu wake wanakatazwa kujenga kwa pesa zao?

Wewe ndo umegeuza kijiwe cha Kahawa na sijui umetoea wapi, Ni Nchi nyingi za Ulaya na hata Marekani, Uliza Wachumi wakusaidie na sio kutaka kuaply CIVICS kwenye mambo ya Uchumi.
 

Wakati wewe unaumiza kichwa juu ya kodi ya nyumba, Mm niko kwenye projects nyingine kabisa mkuu. I

Sent from my LT26i using Tapatalk 2
 
Wewe ndo umegeuza kijiwe cha Kahawa na sijui umetoea wapi, Ni Nchi nyingi za Ulaya na hata Marekani, Uliza Wachumi wakusaidie na sio kutaka kuaply CIVICS kwenye mambo ya Uchumi.

Kweli JF imevamiwa. Watu kama wewew mara nyingi huwa mashabiki wa CHADEMA. Unaongea tu mradi mdomo wako umefunguka!!!
 
Mi ninachojua kwa sasa naitwa Baba mwenye nyumba.

Sent from my LT26i using Tapatalk 2
Baba mwenye nyumba haina maana lazima uwe na nyumba,baba mwenye nyumba maana yake kuwa na mke.Mbona mimi naitwa baba mwenye nyumba wakati nimepanga?
 

Sawa mkuu,

sasa nikishapata huo mkopo nikaamua kuanza biashara ili niongeze kipato, wakati huo mimi nitakuwa nakaa wapi? wazo lako linawalenga Watz walioko hatua ya pili ( wale ambao familia zao zimeshajijenga tayari), wale walioingia mjini na kufikia kwa mtu au homeboy hawezi kukuelewa unapomshauri aanze b/ness wakati hana pa kukaa. Kumbuka utegemezi kwetu bado haujaondoka,wengi wetu baada ya kuanza vibarua tunapiga picha home tulikotoka na tunachokiona ndio kinatufanya tujenge kwanza biashara ambalo si chaguo la kila mtu huja baadae baada ya kupata utulivu wa akili.

Nakupa changamoto hii,
Mama mzazi atoke kijijini kwenu aje kukutembelea mjini, akute uko kwenye chumba cha kupanga ili hali una mabiashara makubwa makubwa, sijui kama atakuelewa ( nazungumzia kiafrica zaidi, mlio na mawazo ya Uk hii not applicable). Kwetu sisi heshima ya mtu awe na kwake ( nyumba kwanza) na mengine yafuate. Samahani niko Kiafrika zaidi.
 
heshima pesa ubaba mwenye nyumba chanzo cha shikamoo ambazo ni kelele tu

Nashindwa kuelewa unachofikiria... huyu anayeitwa baba mwenye nyumba maana yake anatengeneza hela kupitia nyumba yake, hivi unajua thamani ya nyumba wewe? Nenda kule mikocheni, Oysterbay, Masaki, Kijitonyama, Mwenge, Sinza na sehemu zinazofanana na hizo utajua watu wanatengeneza shs ngapi kwa kupangisha nyumba zao. Au pesa kwako ni ile inayotokana na biashara tofauti na nyumba?
 



uko sahihi,lakini mimi nazungumzia kijana bachela mwenye kazi ya kawaida,mimi ambacho sikubaliani ni ile kujenga nyumba ya kuishi yeye mwenyewe yaweza kuwa ya vyumba 2 ambayo ni vigumu kupangisha.Nakama atajenga nyumba na akapangisha is okey ndo hapo tunasema kaingia kwenye ujasiriamali hiyo itakuwa safi sana.
 
Ndugu yangu nyumba ni investment yenye profit kubwa tu. Nikupe mfano mimi nimenunua kiwanja 2007 sh 1.5m, Makongo Juu Dsm leo kiwanja katika eneo nilipo ni zaidi ya milioni 30. Sasa nime simamisha na mjengo hii inamaana kiwanja changu pamoja na mjengo vinaweza kuniingizia zaidi ya milioni 90 hivi. Lakini bado ninafaidi ya pesa niliyokuwa nikilipa kodi kila mwaka Sinza ambayo ni milioni 1.5, sasa hivi silipi tena nipo kwangu.
 

Nimekupata,
Wewe unazungumzia wanaotaka kuwa wajasiriamali. Kumbuka ktk dunia hii wajasiriamali ni wachache sana na pia sio kila mtu anataka kuhangaisha bongo yake kwa biashara. Kuna watu na ni wengi wao malipo ya mshahara kwao yanatosha na hahitaji biashara zaidi, kama ambavyo watu wote hawawezi kucheza mpira na wakalipwa mihela kama Messi.

Ushauri wako uko sahihi kwa watu wachache sana kama nilivyokwisha sema kuwa ni kwa familia zilizo ktk hatua ya pili, nyumba ni ulinzi na heshima.
 

I totally support you, nimekuwa nikibishana na marafiki zangu wengi wenye mawazo mgando kama ya wana jf wengi waliorespond kwa hii thread. yeyote anayejidai ana nyumba muulize maswali yafuatayo:

Nyumba yako iko plot No. ngapi?, block no. ngapi? offer yako namba ngapi, je una lease?

Ukimuuliza hayo maswali nina uhakika majibu mengi ni hapana. Kwa maana nyingine ameweka ardhini wazungu wanachoita white elephant. Hiyo "nyumba" utakuta amejenga kwa mfuga mbwa hapaeleweki wala hapatambuliki na hawezi kwenda kukopea. I urge people to forget the conventional way of thinking and start thinking like the person of 21 st century.

To most people i know their homes are not assets rather they are liabilities. Na hizo wanazoita nyumba si nyumba ni vibanda, mtu eti amejenga nyumba choo chenyewe cha nje hajui kama yuko vulnerable muda wowote aweza katwa mapanga usiku, anaoga kwa kujimwagia na kopo! Mswaki asubuhi anapigia kwenye maua au migomba iliyo karibu na hiyo"nyumba".

Give me break; we should think like great thinkers.
 
Unaishi kwa nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…