Mawazo ya mtoa mada ni ya kijasiriamali zaidi. Na wajasiriamli ni wachache sana kwenye ulimwengu wa leo. Ndiyo maana wengi wao wanampinga. Ni mara chache sana unaweza kumwambia mtu aache kazi ajiajiri mwenyewe akubaliane na wewe. Wengi wao watakujibu niache kazi nile nini? Familia yangu ile nini? Nitaishije? Maswali chungu nzima. Ndo maana hata hapa utakutana na maswali kama, si afadhali kuishi kwenye nyumba yako..., si afadhali kuachana na kero za kupanga? Wao maisha ni kutatua kero moja leo na kuendelea kuishi kwenye utumwa mwingine miaka nenda rudi.
SO MTAZAMO WANGU NI HUU;
1. Kama aliyechukua mkopo siyo mjasiriamali, ni afadhali akajenga nyumba ya kuishi maana hela yote itaishia kwenye starehe na kubakia kuwa omba omba maana mshahara ndo hivyo tena anagawana mdai wake.
2. Kama aliyechukua mkopo ana ndoto ya kuwa mjasiriamali na amebanwa sana kazini, na hataweza kufuatilia biashara yoyote namshauri ajenge nyumba kwa ajili ya biashara, atakusanya hela ya kodi, value ya nyumba na kiwanja vitakuwa vinaongezeka kila siku, mwisho wa siku kama atakuwa anataka kuacha kazi anaweza kuuza nyumba, changanya na hela ya kodi ni mtaji tosha wa kufanyia biashara na kuachana na utumwa wa kufanyia kazi watu wengine.
3. Kama aliyechukua mkopo ni mjasiriamali muajiriwa ambaye hajabanwa kazini, basi fungua biashara ambayo umeifanyia utafiti wa kutosha na kuridhika kuwa ukingiza mtaji wako hela yako itakuwa inazunguka vizuri na kupata faida ya kuweza kufanya hayo mambo mengine kama kujenga makazi ya kuishi n.k.
Huu ni mtazamo wangu tu kama mjasiriamali.