Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
well said, labda niongezee tu unakuwa kwako uko free kuleta ndugu ambao watafikia badala ya kuwapangishia gesti ikiwa nyumba ya kupanga ndogo, ninaweza kufuga, kulima bustani kwa matumizi yangu na biashara, kufundisha tuition, kufanya consultancy etc, ninaweza kuweka fremu nikafanya biashara duka au chochote bila kulipa kodi.Ndugu yangu nyumba ni investment yenye profit kubwa tu. Nikupe mfano mimi nimenunua kiwanja 2007 sh 1.5m, Makongo Juu Dsm leo kiwanja katika eneo nilipo ni zaidi ya milioni 30. Sasa nime simamisha na mjengo hii inamaana kiwanja changu pamoja na mjengo vinaweza kuniingizia zaidi ya milioni 90 hivi. Lakini bado ninafaidi ya pesa niliyokuwa nikilipa kodi kila mwaka Sinza ambayo ni milioni 1.5, sasa hivi silipi tena nipo kwangu.
Mawazo ya mtoa mada ni ya kijasiriamali zaidi. Na wajasiriamli ni wachache sana kwenye ulimwengu wa leo. Ndiyo maana wengi wao wanampinga. Ni mara chache sana unaweza kumwambia mtu aache kazi ajiajiri mwenyewe akubaliane na wewe. Wengi wao watakujibu niache kazi nile nini? Familia yangu ile nini? Nitaishije? Maswali chungu nzima. Ndo maana hata hapa utakutana na maswali kama, si afadhali kuishi kwenye nyumba yako..., si afadhali kuachana na kero za kupanga? Wao maisha ni kutatua kero moja leo na kuendelea kuishi kwenye utumwa mwingine miaka nenda rudi.
SO MTAZAMO WANGU NI HUU;
1. Kama aliyechukua mkopo siyo mjasiriamali, ni afadhali akajenga nyumba ya kuishi maana hela yote itaishia kwenye starehe na kubakia kuwa omba omba maana mshahara ndo hivyo tena anagawana mdai wake.
2. Kama aliyechukua mkopo ana ndoto ya kuwa mjasiriamali na amebanwa sana kazini, na hataweza kufuatilia biashara yoyote namshauri ajenge nyumba kwa ajili ya biashara, atakusanya hela ya kodi, value ya nyumba na kiwanja vitakuwa vinaongezeka kila siku, mwisho wa siku kama atakuwa anataka kuacha kazi anaweza kuuza nyumba, changanya na hela ya kodi ni mtaji tosha wa kufanyia biashara na kuachana na utumwa wa kufanyia kazi watu wengine.
3. Kama aliyechukua mkopo ni mjasiriamali muajiriwa ambaye hajabanwa kazini, basi fungua biashara ambayo umeifanyia utafiti wa kutosha na kuridhika kuwa ukingiza mtaji wako hela yako itakuwa inazunguka vizuri na kupata faida ya kuweza kufanya hayo mambo mengine kama kujenga makazi ya kuishi n.k.
Huu ni mtazamo wangu tu kama mjasiriamali.
nikikumbuka hii post huwa nacheka sanachama2chawa idea yako ime kaa kishirikina shirikina hivi
Usifikiri kama unaweza kuingia kwenye kichwa cha mtu kiasi hichohata ukiniita red hindu lakini huo ndo ukweli tatizo lako wewe ni muoga wa maisha.
Kuna mawazo huwezi kuyatekeleza ukiwa nyumba ya kupanga au kwa shemeji,uko sahihi,lakini mimi nazungumzia kijana bachela mwenye kazi ya kawaida,mimi ambacho sikubaliani ni ile kujenga nyumba ya kuishi yeye mwenyewe yaweza kuwa ya vyumba 2 ambayo ni vigumu kupangisha.Nakama atajenga nyumba na akapangisha is okey ndo hapo tunasema kaingia kwenye ujasiriamali hiyo itakuwa safi sana.