Unajenga nyumba utakula hiyo nyumba!?

Unajenga nyumba utakula hiyo nyumba!?

x - mas

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
931
Reaction score
612
amani iwe nanyi ndugu zangu,kuna hii kitu inanishangaza sana utakuta kijana mfanya kazi za kawaida sana tukiachana na kazi zenye mishahara mikubwa kama ubunge hapa nazungumzia kwa mwanajeshi, mwalimu,askari,bibi/bwana shamba au nesi halafu ni bachela hana mke wala familia amepata pesa labda kwa mkopo,sasa huyu mtu badala ya kufungua mradi aongeze kipato ana kimbilia kununua kiwanja na kujenga nyumba ya kuishi na sio ya biashara utafikiri kaambiwa kuwa viwanja vitaisha kesho ndugu yangu nakwambia viwanja haviishi leo Tanzania hii utazeeka na kufa wewe viwanja vitaendelea kupatakana labda kwa baadae sana ndo tutasema viwanja vimeisha kwani hata marekani pamoja na kuwa na majengo mengi hukitaka kuwa na nyumba yako leo hii utapata hela yako tu..naomba uniwieradhi kama nimekuvunja moyo ila ndo ukwali huo ongeza kipato chako kwanza ndo ujenge nyumba.
 
Wazo lako halitilii maanani kwamba kujenga nyumba pia ni kuwekeza. Nyumba huleta pesa kwa kupangishwa, na hata ukiishi mwenyewe ndani ya nyumba uliyojenga bado unaokoa fedha ya kupanga. Bila kusahau kwamba thamani ya viwanja na nyumba siku zote huongezeka.
 
Mfano umepanga nyumba unalipa kodi ya laki 2 kwa mwezi na unauwezo wa kukopa mil 20 ukajenga vyumba vyako viwili au vitatu ukahamia na marejesho yako kwa mwezi yakawa ni hiyo laki 2 au hata zaidi kidogo, hauoni kwa kufanya hivyo unapata faida? kwanza utaishi confortable kwenye nyumba yako bila kusumbuliwa na mwenye nyumba, pia utakuwa unamiliki nyumba ambayo ni rasimali muhimu na ukuimaliza huo mkopo unaweza kuitumia kupata mkopo mkubwa zaidi wa biashara, inakupa assurance kidogo ya ahueni ya maisha pale utakapokuwa hauna kazi ya uhakika, n.k, n.k..
Kwahiyo kila mtu ana calculation zake na hata hao wanaokopa kwa ajili ya kujenga nyumba wamekuwa wamefanya calculation zao ipasavyo. Kama wewe kukopa ni kwa ajili ya biashara tu hiyo ni hesabu yako siyo lazima kila mtu awe kama wewe.
 
amani iwe nanyi ndugu zangu,kuna hii kitu inanishangaza sana utakuta kijana mfanya kazi za kawaida sana tukiachana na kazi zenye mishahara mikubwa kama ubunge hapa nazungumzia kwa mwanajeshi, mwalimu,askari,bibi/bwana shamba au nesi halafu ni bachela hana mke wala familia amepata pesa labda kwa mkopo,sasa huyu mtu badala ya kufungua mradi aongeze kipato ana kimbilia kununua kiwanja na kujenga nyumba ya kuishi na sio ya biashara utafikiri kaambiwa kuwa viwanja vitaisha kesho ndugu yangu nakwambia viwanja haviishi leo Tanzania hii utazeeka na kufa wewe viwanja vitaendelea kupatakana labda kwa baadae sana ndo tutasema viwanja vimeisha kwani hata marekani pamoja na kuwa na majengo mengi hukitaka kuwa na nyumba yako leo hii utapata hela yako tu..naomba uniwieradhi kama nimekuvunja moyo ila ndo ukwali huo ongeza kipato chako kwanza ndo ujenge nyumba.
Kwa kuwa bado unaishi na wazazi wako na adha ya kodi ya nyumba kwa hapa bongo huijui, tunakusamehe.
 
chama2chawa, jifunze upya...uoni wako ni mfupi au unatia mashaka! Si watu wote wenye kutaka biashara unayotaka wewe!Kuna baadhi mambo ya biashara ni kushoto kabisa lakini kwa 'biashara' hii ya nyumba inawasaidia katika maisha!

pmwasyoke, Lusa Nise..majibu mazuri wakuu.
 
Last edited by a moderator:
amani iwe nanyi ndugu zangu,kuna hii kitu inanishangaza sana utakuta kijana mfanya kazi za kawaida sana tukiachana na kazi zenye mishahara mikubwa kama ubunge hapa nazungumzia kwa mwanajeshi, mwalimu,askari,bibi/bwana shamba au nesi halafu ni bachela hana mke wala familia amepata pesa labda kwa mkopo,sasa huyu mtu badala ya kufungua mradi aongeze kipato ana kimbilia kununua kiwanja na kujenga nyumba ya kuishi na sio ya biashara utafikiri kaambiwa kuwa viwanja vitaisha kesho ndugu yangu nakwambia viwanja haviishi leo Tanzania hii utazeeka na kufa wewe viwanja vitaendelea kupatakana labda kwa baadae sana ndo tutasema viwanja vimeisha kwani hata marekani pamoja na kuwa na majengo mengi hukitaka kuwa na nyumba yako leo hii utapata hela yako tu..naomba uniwieradhi kama nimekuvunja moyo ila ndo ukwali huo ongeza kipato chako kwanza ndo ujenge nyumba.

Hahahaa, kopa ununue FUSO!!!
Labda haujaishi kwingi ujue mengi, kwa mfanyakazi nyumba ni kitu cha muhimu sana kumpunguzia gharama za kupanga, na pia ni njia ya kuwekeza, na pia baadaye akishakuwa na idea za kijasiriamali na keshaijua biashara anaweza kuitumia nyumba kama dhamana katika mkopo wa kibiashara. Amini nakwambia, kwa mfanyakazzi ambaye hajajaribu biashara kujenga nyumba ni safe zaidi kuliko kukopa halafu uanzishe biashara. Wazo zuri ni kwa waajiriwa kujifunza ujasiriamali mapema, wakishaona biashara inalipa ndipo tu wanaweza kutumia kazi kama dhamana ya mkopo wa kuendeleza biashara, japo kikawaida kazi si sahihi kuwa dhamana ya mkopo wa biashara, kwani biashara na kazi yako ni vitu viwili tofauti!
Sijawahi kuwa mtumishi, lakini kwa uzoefu wa miaka mingi naona wafanyakazi wengi wakikopa na kuanzisha biashara mara nyingi huambulia hasara, bishara inataka usimamizi wa karibu mno, halikadhalika kazi inakugharimu masaa mengi kwa siku hivyo kushindwa kusimamia vizuri biashara!
 
Wewe unawivu ndiyo unaokusumbua na sijui umepanga au bado unaishi kwa walezi/wazazi wako..ebu waulize hapo unapoishi walijengaje?Hakuna kitu cha thamani duniani kama nyumba hata ukiwa VX 100 kama huana kwako ni bure.

Nilitarajia ungewatia moyo wenzako kumbe wewe ndiyo mmoja wa warudisha maendeleo..ebu kajifunze habari za basic needs of humans beings
 
Nadhani jinsi ya kutumia pesa ni maamuzi binafsi ya mtu. Hata hiyo biashara inaweza kukata ukaishia kuadhirika. Nadhani jambo la msingi hapa si kujenga nyumba au kufanya biashara bali kuweza kutumia kulingana na uwezo wa mtu huku akitafuta kila mbinu ya kuhakikisha anakuwa na uwezo endelevu. Simpo.
 
hizo ni bange tuu:majani7:

Yaan huamini kama nyumba ni investment??
 
Tatizo lako hujui tofauti kati ya mradi na uchuuzi. Anza kwa kujifunza vizuri maaan ya maneno haya.
 
Watu wanamsakama Mtoa Maada Bure, Ni kweli kabisa kiuchumi ni makosa kujenga nyumba kwa cash yako mwenyewe hasa Mshahara na Nchi zilizo endelea Haiuruhusiwa kabisa kujenga kwa pesa yako, ni razima uchukua mkopo Benki na Marejesho yake ni kidokidogo na unaweza rejesha mpaka ukafa na watoto wakamalizia, na ni marejesho yasiyo umiza si kama huku Bongo kukomoana

Isipo kuwa kwa watu wenye pesa kama wasanii na wafanya biashara wakubwa, tena hao hutakiwa kununua,

Na that is why, Mikopo ya Kujenga Nyumba Hurejeshwa kwa Muda Mrefu sana, Lakini huku Bongo mtu anakopa mkopo na anajenga nyumba na inatakiwa Aurejeshe ndani ya Mwaka mmoja au Miwili, Hii kiuchumi haipo na inapatikana Bongo pekee,

Mara Nyinyi nyumba Huchukua Muda Mrefu sana Kuja kufanya Return hata hayo Magorofa Unayo yaona Inawachukua miaka Mingi sana kuja ku break even

Ingawa some time Mazingira ya huku anaforce watu kujenga Nyumba na hii ni kutokana na kwamba Ujenzi huku Africa hasa Bongo ni Rahisi sana na hakuna Sheria kabisa, Thati is why unakuta Mtu kajenga Gorofa si Gorofa yaani nyumba haileweki, Lakini kwa Wenzetu hakuna kitu kama hicho Sheria za Ujenzi ni kari sana na Kuna makampuni yanayo husika na kazi za Ujenzi na si mtu kuanza kukusanya Misumari, Nondo na kuanza kujenga, Na hilo ndo linalo tufeza huku Tanzania,

Na ndo maana hata serikali inajaribu kuja na vitu kama Mikopo ya Nyumba kwa sababu wanafahamu kabisa nyumba inahitaji Marejesho ya Muda Mrefu sana na wazungu some time hata hawajengi wanaishi kwenye Nyumba za Kupanga mwazo mwisho kutokana na mambo kama haya
 
amani iwe nanyi ndugu zangu,kuna hii kitu inanishangaza sana utakuta kijana mfanya kazi za kawaida sana tukiachana na kazi zenye mishahara mikubwa kama ubunge hapa nazungumzia kwa mwanajeshi, mwalimu,askari,bibi/bwana shamba au nesi halafu ni bachela hana mke wala familia amepata pesa labda kwa mkopo,sasa huyu mtu badala ya kufungua mradi aongeze kipato ana kimbilia kununua kiwanja na kujenga nyumba ya kuishi na sio ya biashara utafikiri kaambiwa kuwa viwanja vitaisha kesho ndugu yangu nakwambia viwanja haviishi leo Tanzania hii utazeeka na kufa wewe viwanja vitaendelea kupatakana labda kwa baadae sana ndo tutasema viwanja vimeisha kwani hata marekani pamoja na kuwa na majengo mengi hukitaka kuwa na nyumba yako leo hii utapata hela yako tu..naomba uniwieradhi kama nimekuvunja moyo ila ndo ukwali huo ongeza kipato chako kwanza ndo ujenge nyumba.

Baada ya miaka 15 hivi njoo tena utueleze maneno hayo kwenye bold, btw sijui una umri gani?
 
Baada ya miaka 15 hivi njoo tena utueleze maneno hayo kwenye bold, btw sijui una umri gani?

Mkuu kikubwa ni Pesa na wala si kingine, Ukiwa na Pesa hata Mlima unaweza kuuhamisha, Viwanja mpaka sasa kwa masikini kama sisi havipatikani ila kwa wenye pesa ni mashamba kabisa, Mbona USA ilianza miaka ya Elfu miasa lakini kuna viwanja na kila kukicha wanajena nyumba? na wako Milioni karibia 400? ishu si maeneo ishu ni pesa ukiwa na pesa huwezi kosa sehemu ya Kujenga kamwe
 
Aliyeleta huu uzi ni Muha tu, kwani kigoma wivu ndio nyumbani kwao. Umenikera kweli, unataka akaishi kichakani au akanunue toyo/prado ndio uridhike?
 
ndo mana nikaomba radhi najua wengi mmetumbukia kwenye hili janga la kujenga nyumba kwa pesa ya mkopo mwisho wa siku unakuwa na nyumba kubwa hafu unalala njaa,unaanza kuchukia wageni kwa kuwa huna cha kuwalisha au unashindwa kusomesha wengene walikopa mara ya pili wakashindwa kulipa wakaamua kuuza nyumba baada ya kuona maji ya shingo.TATIZO LETU WABONGO TUNAISHI KWA KUKARIRI hatupendi kufanya vitu vya tofauti yaani ndo ile mtu akinunua toyo basi wote ndo style utaona kila mtu kanunua toyo wakati kunaaina nyingi za pikipiki.
amani iwe nanyi ndugu
zangu,kuna hii kitu inanishangaza sana utakuta kijana mfanya kazi za
kawaida sana tukiachana na kazi zenye mishahara mikubwa kama ubunge hapa
nazungumzia kwa mwanajeshi, mwalimu,askari,bibi/bwana shamba au nesi
halafu ni bachela hana mke wala familia amepata pesa labda kwa
mkopo,sasa huyu mtu badala ya kufungua mradi aongeze kipato ana kimbilia
kununua kiwanja na kujenga nyumba ya kuishi na sio ya biashara
utafikiri kaambiwa kuwa viwanja vitaisha kesho ndugu yangu nakwambia
viwanja haviishi leo Tanzania hii utazeeka na kufa wewe viwanja
vitaendelea kupatakana labda kwa baadae sana ndo tutasema viwanja
vimeisha kwani hata marekani pamoja na kuwa na majengo mengi hukitaka
kuwa na nyumba yako leo hii utapata hela yako tu..naomba uniwieradhi
kama nimekuvunja moyo ila ndo ukwali huo ongeza kipato chako kwanza ndo
ujenge nyumba.
 
Back
Top Bottom