Unajiamini kupita kiasi mpaka unatia hasara na hasira kwa wenzio

Unajiamini kupita kiasi mpaka unatia hasara na hasira kwa wenzio

OgaBoy

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
1,531
Reaction score
2,140
Kuna watu wa ajabu sio siri ni wasumbufu. Jamaa flani huwa na tabia ya ajabu yaani yeye akienda garage na gari yake, anauliza kutatua tatizo fulani ni shingapi anaambiwa basi anasema okay fanyeni marekebisho alafu jamaa anakaa pembeni anaagiza bia na ile pesa ya ufundi kinachobaki ndo anawapa mafundi wakati walikubaliana bei tofauti.

Mafundi wakigoma anawatisha kuondoka na hiyo hela na gari wala haongezi anasema si mnakataa hii hela bana mi naenda yaani kirahisi.

Mfano tatizo ni kuziba pancha au kukaza na kubadili taili. Labda kaambiwa ni 20k anakunywa bia pale kinachobaki hapo ndo anawapa mafundi. Tabia mbaya.

Wengi wanaopata hasara na hasira ni wale wanaotoa huduma za malipo baada ya kazi hapa ukikutana na watu wa hivi ni tabu tu!

Inabidi muwe na mifumo mizuri ya malipo kwanza ndo huduma ifuate ikishindikana kutatua tatizo mnarudisha pesa kuliko kuisubiri.
 
Juzi nilipanda gari ya abiria na mtu wa aina hiyo anae jiamin kupita kiasi hadi akaanza kunikera.

Alipandishwa abiria mtoto wa Kama miaka 14 maelekezo kapewa kondakta jamaa akaanza kumuhoji mtoto kwa sauti huku anamuuliza mtoto kwanini unasafiri mwenyewe? Mama yako anaakili kweli? Yuko wapi? Akasimama kwenye siti akaanza kuwasukuma watu waliokaa siti za dirishani bila ustaarabu anawafokea sogea sogea ili amuone mama wa mtoto ila hakumuona kwakua gari lilishaanza kuondoka.

Akakaa kama dakika 20 mwendo ni wa kawaida tu akaanza kupiga kelele kumwambia dereva asimamishe gari eti mwendo ni mkali sana, kufika kwa trafik akamuita trafik akamwambia dereva anakimbiza sana gari mpige faini, wakati trafik anaenda kwa dereva abiria wakamwambia Askari kuwa gari inaenda mwendo wa kawaida tu haikimbii kama jamaa anavyodai.

Yule msela alivyosikia abiria wanasema hivyo akasimama kwa hasira huku anatukana huyo ms*nge anaesema gari haikimbii ni Nani? Aseme mbele yangu nimuone.

Daah ooyaaah jamaa alinikera kishenzi yule mshamba sijui ni wa wapi angeendelea na makelele yake ningemtia vitasa ila baada ya kutukana aliletewa noma na abiria karibu wote baada ya hapo akatuliza wenge.
 
Huyo mwamba nae hujilipa kwe fungu la utawala.

Huyo mpigeni lile la kufumulia tairi aje awasumbue polisi kupeleleza.

Akija tena alete ujinga, kamateni muingizen kwenye gari yake au gari yoyote mmshikishe adabu. Ili wengine wajifunze.
 
Unamzungumzia kujiamini au mtu mwenye mental illiness .
Kuna tofauti ndogo sana ya kujiamini na kuwa mshamba huyo jamaa Hana tatizo lolote la akili ila inaonekana kuna kanafasi flan alipata ikamfanya ajiamini hadi akawa mjinga akaona anayo mamlaka mbele ya kila anaekutana nae kumbe haiko hivyo
 
Juzi nilipanda gari ya abiria na mtu wa aina hiyo anae jiamin kupita kiasi hadi akaanza kunikera

Alipandishwa abiria mtoto wa Kama miaka 14 maelekezo kapewa kondakta jamaa akaanza kumuhoji mtoto kwa sauti huku anamuuliza mtoto kwanini unasafiri mwenyewe? Mama yako anaakili kweli? Yuko wapi? Akasimama kwenye siti
Wanakera sana watu wa aina hiyo, ni walimbukeni
 
Kuna tofauti ndogo sana ya kujiamini na kuwa mshamba huyo jamaa Hana tatizo lolote la akili ila inaonekana kuna kanafasi flan alipata ikamfanya ajiamini hadi akawa mjinga akaona anayo mamlaka mbele ya kila anaekutana nae kumbe haiko hivyo
Basi ukute hakutegemea kama angepata hako kanafasi.
 
Back
Top Bottom