Unajipaka mafuta gani mwilini?

Napaka mafuta ya nazi minara naogea sabuni ya ozona vimenisaidia uso angalau kua vizuri. Nina wiki mbili toka nianze kuvitumia
tengeneza mwenyewe ndo utafaidi hayo ya mombasa ovyo tu
 
Duuh! Una "aleji" kama mimi nini?

Me pia natumia sabuni hizo kama nikibadili ni dettol, kinyume na hapo ni majanga.

Mafuta ya nazi (nitangeneza mwenyewe, naweka na karafuu+mdalasini+hiliki)
waooh!hongera
 
nakogea sabuni ninayotengenza mwenyewe yenye mchamganyiko wa nazi+asali.na papai
napaka mafuta ninayotengeneza mwenyewe anbayo nimeyapa jina DN ni mchanganyiko wa lavenda+mdalasini mbichi+mchaichai ni mazuri sana kwa jinsia zote tunapaka familia nzima na yana harufu nzuri sana
 
mafuta ya nazi huwa unayawekeaje hvo vikorobwezo dear? mimi nayatumia tu hivohivo
jinsi ya kuweka kikolombwezo chochote ktk mafuta yako-:
CHUKUA MAFUTA YA NAZI KIASI UPENDACHO,
WEKA KATIKA JAGI LA CHUPA AMBALO LINAMFUNIKO,
CHAGUA VIKOLOMBWEZO UNAVYO VIPENDA,
TUMBUKIZA NDANI YA JAGI LENYE MAFUTA YA NAZI FUNGA VIZURI,
ACHA VILALE HUMO USIKU MZIMA,ASUBUHI TOA VIKOLOMBWEZO TAYARI UTAKUWA UMETENGENEZA MAFUTA YAKO UNIQUE NA MAZURI!
 

nifundishe best
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…