GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Leo nilipokuwa ninaperuzi mtandao wa Quora, nilikutana na mada moja inayohusiana na mighahawa ya KFC na McDonald barani Afrika.
Mmoja wa wachangiaji alieleza kuwa Afrika Kusini na Misri ndizo nchi zinazoongoza kwa kuwa na hiyo mighahawa barani Afrika. Hata hivyo, baadhi ya matawi ya KFC Afrika Kusini zilifutiwa leseni na KFC baada ya kushindwa kukidhi vigezo vya usafi vya KFC.
Sikushangazwa na hiyo comment maadam ni Afrika. Nafikiri unanielewa nikisema hivyo. Niliamini kuwa kwa vyovyote msimamizi wa huo mgahawa atakuwa ni mtu mweusi.
Nilipoendelea kuperuzi, nilikutana na swali lililokuwa likiuliza nchi inayoongoza kwa uchafu duniani. Majibu yaliyofuatiwa yalinitia moyo.
Tanzania haikuwemo, wala Burundi, wala Uganda, wala Kenya. Hakuna nchi toka barani Afrika iloyotajwa, pamoja na kwamba wengi wa wachangiaji walidai kuwa wameshafika nchi mbalimbali duniani katika kila bara.
Nchi iloyotajwa na watu wengi kuwa inaongoza kwa uchafu ni India. Wanadai ni kuchafu sana hakuna mfano.
Sifurahii nchi ya India kuwa chafu, lakini mimi ambaye ni Mwafrika, nimefurahi kwa nchi yangu na bara langu kutokutajwa kama kinara wa uchafu duniani.
Wewe unajisikiaje kufahamu hilo?