Mtu ukijitambua vizuri inakuwa rahisi kujithaminisha, na unavoweza kujithaminisha na jamii inayokuzunguka itakuthamini, being yourself haiwzi kuwa tu njia ya kuthaminiwa, unaweza kuongezea vitu vya ziada ili hata wengine wakuthamini, unaangalia uko na nani na unaongea nini, unaenda wapi na unaonekana vipi, personallity yako pia inaweza kukufanya uthaminiwe mahala fulani, na pia thamini wenzako ili na ww uthaminiweGaga asante kwa hayo
Ila inaanzia kwako kwanza yaani wewe unajitambua, unatambua thamani yako, unatambua nafasi yako, unatambua umuhimu wako na ukajiweka katika nafasi ya kuthamini hilo. Then muonekano wako nao unachangia na maongezi yako na sio mtu wa kukurupuka kufikia kutoa ushauri au unapoambiwa jambo then ukawa msikizu sio mtu wa kujikweza then jamii itakuelewa. Hapo hutumii elimu yako wala cheo chako wala nafasi yako katika jamii. Jamii inakuona wewe kama wewe na sio kwa ile title au class au cheo ulicho nacho.
Hiyo ya kutoa complement ya umependeza hata kwa mwenzi wako wengi huwa tunajisahau kusema ukweli. Kuna wale ambao wanafanya kusudi kuishusha thamani ya mwenzake kwa maneno na visa vya kukukatisha tamaa sasa hapa inakuwaje?
Maneno kama....unajifanya unajua, ni hivyo videgree vyako ambavyo any tdh can have it....LOL
Mbu, usipojithaminisha mwenyewe ni vigumu mtu mwingine kukuthamini, kujithamini kuanzia ndani ya roho na mwili wako na hadhi yako kama binadamu kamili, hapo hata wengine wanaweza kukuthamini
Mr Rocky za siku nyingi? Gud to have you back!
Eti eh! Ah kweli binadamu tupo wa aina nyingi! Mwenzako hiyo ndo anaiona hoja baab kubwa!
Mbu kuhusu kuchukua hatua pale unapohisi kutumiwa kwa faida ya wengine mh kweli wengine tunahitaji therapy.....huwa tuna ile ya namwachia Mungu ...sasa sijui hatujiamini au kujithamini!?
Kweli kabisa Tulizo, ila sie waafrica hapo bold huwa ngumu sana, wengi wetu kujishusha ili tupate faida fulani hatuwezi, natokeo yake kila mtu kichwa juu hata kwenye jambo anaona kabisa anatakiwa aje chini lakini hakunaNi kweli kujithamini au kuthamini wengine kunatokana na kujitambua wewe binafsi. Na hili kujitambua wewe binafsi inabidi ujue tamaduni za jamii inayokuzunguka iwe kazini, familia au hata Pub. Kwa kujua hilo ndio utaweza kushusha au kupandisha vigezo kutokana na maisha ya jamii hiyo.
Mara nyingi ukijishusha kwa kiasi fulani utakuwa na uwezo mzuri wa kujitambua na kujichaganya na kukubalika na jamii sehemu yeyote hile..hata pale nyumbani kwako jaribu kujishusha na kuthamini kazi za House girl au Houseboy wako..jaribu kumfanya kama mdogo wako na uone matokeo yake.... Pia tukumbuke hakuna kipimo cha thamani..sio cheo, wala hela, wala mavazi, wala mikogo..wala kutoa misaada..vyote hivyo havisaidii kupandisha thamani yako ..Thamani ni kukubalika..na kuheshimika kwa kujishusha kwako albeit ilibidi uwe juu... Hata walevi wanathamani na kuthaminiwa wakikutana kwenye jamii za walevi wenzao..ni utamaduni na vigezo vyao. Hapo utaona thamani inakuja yenyewe na wala sio wewe unayeiweka au kuilazimisha... kikubwa.. Jitambue..jishushe ili wale wanaokuzunguka ndio wakupandishe..