Unajithamanishaje? ...Unathaminiwa?

Unajithamanishaje? ...Unathaminiwa?

Voiceofreason umeongea kweli kabisa nakuunga mkono. Try to be yourself and the rest will take care of itself and never try to be somebody as u will end up not been somebody but nobody.
 
Mtu ukijitambua vizuri inakuwa rahisi kujithaminisha, na unavoweza kujithaminisha na jamii inayokuzunguka itakuthamini, being yourself haiwzi kuwa tu njia ya kuthaminiwa, unaweza kuongezea vitu vya ziada ili hata wengine wakuthamini, unaangalia uko na nani na unaongea nini, unaenda wapi na unaonekana vipi, personallity yako pia inaweza kukufanya uthaminiwe mahala fulani, na pia thamini wenzako ili na ww uthaminiwe
 
Gaga asante kwa hayo
Ila inaanzia kwako kwanza yaani wewe unajitambua, unatambua thamani yako, unatambua nafasi yako, unatambua umuhimu wako na ukajiweka katika nafasi ya kuthamini hilo. Then muonekano wako nao unachangia na maongezi yako na sio mtu wa kukurupuka kufikia kutoa ushauri au unapoambiwa jambo then ukawa msikizu sio mtu wa kujikweza then jamii itakuelewa. Hapo hutumii elimu yako wala cheo chako wala nafasi yako katika jamii. Jamii inakuona wewe kama wewe na sio kwa ile title au class au cheo ulicho nacho.
 
Hahahaha Mbu eti Unanidharau sana wewe!! Lakini haiwezitoka kwa anayejithamini? LOL
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Thank You Mbu for this useful post........
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mtu ukijitambua vizuri inakuwa rahisi kujithaminisha, na unavoweza kujithaminisha na jamii inayokuzunguka itakuthamini, being yourself haiwzi kuwa tu njia ya kuthaminiwa, unaweza kuongezea vitu vya ziada ili hata wengine wakuthamini, unaangalia uko na nani na unaongea nini, unaenda wapi na unaonekana vipi, personallity yako pia inaweza kukufanya uthaminiwe mahala fulani, na pia thamini wenzako ili na ww uthaminiwe
Gaga asante kwa hayo
Ila inaanzia kwako kwanza yaani wewe unajitambua, unatambua thamani yako, unatambua nafasi yako, unatambua umuhimu wako na ukajiweka katika nafasi ya kuthamini hilo. Then muonekano wako nao unachangia na maongezi yako na sio mtu wa kukurupuka kufikia kutoa ushauri au unapoambiwa jambo then ukawa msikizu sio mtu wa kujikweza then jamii itakuelewa. Hapo hutumii elimu yako wala cheo chako wala nafasi yako katika jamii. Jamii inakuona wewe kama wewe na sio kwa ile title au class au cheo ulicho nacho.

Ama Gaga na Mr Rocky kama mlikuwa mawazoni mwangu.

Japo sidhani kuna ubaya kujaribu/kujitahidi ufanane na fulani (in terms of achievements Only!) kujibadilisha muonekano, sauti, miondoko, nk ndiko kunako fanyisha mtu aonekane kutoko vile vile. Kwenye mapenzi, utakuta mtu anakuwa msanii weeee...siku ya siku 'sinema' ikiisha ndio hapo utaposikia, "jitihada zangu zote umeziona bure!"...ama?

Kujithaminisha kunaanzia kwenye basics jamani. Kunaiz mtu anapoamaka, kutandika kitanda chake kwa shuka na foronya safi, kupiga mswaki na kukoga. Kuvaa nguo safi, na utanashati wake...kama manukato/unyunyu upo ruksa kuepusha harufu ya mwili...kuwahi kazini/chuo nk...

Pia katika hayo, yamo kuongea vizuri na watu, ...kuwa msikivu, kuzuia hasira na maamuzi ya haraka. Uvumilivu,...kula kwa nidhamu, mazoezi kumaintain afya ya mwili na akili nk nk nk... Kwa muonekano wa nje utaonekana vizuri, nawe binafsi sina shaka utajiskia vizuri.
Viji compliments vya hapa na pale mfano "umependeza, u mstaarabu,...upo fit, nk" havitakosekana.

Sasa imagine mtu ni kibonge hasa, tumbo kule, au kakondeana afya mgogoro, mlevi, mmgomvi, mzinifu, madharau almuradi...yupo yupo tu,...lakini kwakuwa una pesa,..unalazimishwa uitwe alwatan...sijui pedesheee! Kina dada nao ndio kutaka waonekane 'Bongo Celebrity',...kila skendeli ahusishwe,...what a Crap!
 
Mbu hilo ndio limekamata wengi kwa sasa. Yaani badala ya kujithaminisha wenyewe thamani ianzie kwao wanataka yale wanayoyafanya ndio yawafanye wathaminike. Mtu anakuwa mtoa msaada kwa jamii fulani au kushiriki kwenye matukio ya kila aina kwenye jamii ili ile jamii imtambue ni nani. Akiwa kwenye matukio anajitambulisha kwa cheo chake au kazi yake au nafasi yake kwenye jamii au utajiri au elimu aliyo nayo. Bila kujua kuwa hivyo vyote ukiwa na thamani yako ukiwa unathaminiwa vinajionyesha vyenyewe bila hata kufanya kazi ya kuvitambulisha.
Huna haja ya kuwa mwanamtindo au celebrity au mwanamuziki ili utambiliwe. Haiba yako, heshima yako, mchango wako kwa jamii, busara zako , namna unavyoshirikiana na watu, namna unavyotoa ushauri vinakufanya utambulike na uthaminiwe kwenye jamii husika.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Hiyo ya kutoa complement ya umependeza hata kwa mwenzi wako wengi huwa tunajisahau kusema ukweli. Kuna wale ambao wanafanya kusudi kuishusha thamani ya mwenzake kwa maneno na visa vya kukukatisha tamaa sasa hapa inakuwaje?
Maneno kama....unajifanya unajua, ni hivyo videgree vyako ambavyo any tdh can have it....LOL
 
Mwanajamiione hiyo tunasema ni inferiority complex yaani jamaa anashindwa kukudefeat kwenye hoja anaishia kukuambia unaringia degree yako. Mwambie aje kwa hoja na sio kwamba unaringa.
 
Mr Rocky za siku nyingi? Gud to have you back!

Eti eh! Ah kweli binadamu tupo wa aina nyingi! Mwenzako hiyo ndo anaiona hoja baab kubwa!

Mbu kuhusu kuchukua hatua pale unapohisi kutumiwa kwa faida ya wengine mh kweli wengine tunahitaji therapy.....huwa tuna ile ya namwachia Mungu ...sasa sijui hatujiamini au kujithamini!?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Hiyo ya kutoa complement ya umependeza hata kwa mwenzi wako wengi huwa tunajisahau kusema ukweli. Kuna wale ambao wanafanya kusudi kuishusha thamani ya mwenzake kwa maneno na visa vya kukukatisha tamaa sasa hapa inakuwaje?
Maneno kama....unajifanya unajua, ni hivyo videgree vyako ambavyo any tdh can have it....LOL

Mwj1....mtu wa aina hiyo hajiamini, ana low level ya self esteem. Kwakuwa hajiamini, anakupiga vitofali upate kunyong'onyea ujisheshe kwenye level yake. BTW, hili neno kujishusha kuna watu wanaipotezea maana yake. Being Humble inatokana na utu/haiba ya mtu...
sio almuradi mtu anahitajio/kusudio lake ndio utamuona anajifanya mdogo kama piriton.

The coice is yours kuwa offended na comments za aina hiyo ewe Mwj1.
Ushauri wangu, hata kama utakuwa offended, usizionyeshe hisia zako wazi wazi..mfano kulia mbele yake, nk...
Self Control inayotokana na kujitambua thamani yako itakuwezesha kumnyamazisha mtu wa aina hiyo.

LOL, eti hivyo vidigeree vyako,...ha ha ha! Asipokuliza na hilo, atakusimanga na nyumba yako, gari lako, chako, chako chako...yaani kila kilicho chako kwake yeye kinamsuta! Kosa utalofanya ni kujishusha ili kum please anavyotaka yeye.
Namsikitikia mno mtu anayejishusha kwa aina hii! Hajitendei haki ya uthamani wake...
 
Mbu aksante lol saasaaaa hata sijui niulizeje!! Kama iko hivyo na wewe huna hulka ya kugomba, kufoka au kukemea! Mtu anakufanyia hayo na mambo mengine mengi je ni vema kumkalia kimya au unajipangaje ?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mwanajamiione asante sana sana.
Sio wala swala la kufoka nae mpuuze na mwache aongee ya kwake maana hajui thamani yako na thamani yako wala haiko kwenye degree uliyo nayo bali jamii yenyewe ishakupa thamani ya kutosha. Hutakiwi hata kujali maana degree yako sio inayokupa thamani yako bali wewe tayari ushapokea thamani ya kukutosha kutoka kwenye jamii inayokuzunguka.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

Mwj1...wazee wa busara wana ushauri wao juu ya hilo,...wanasema "mdharau tu!"....
Kumdharau mtu haina maana umuonyeshe kwa vitendo unamzomea la hasha!...
Hata kama yanakuuma, waweza either mjibu hoja kwa hoja, au msubirie siku maruhani yake
yamemtoka umwambie a piece of your mind!
 
Lol Mr Rocky na Mbu mbona mnajibu kama vile ni mimi nlofikwa lol

Hahah hii thread inanifumbua mengi.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mbu, usipojithaminisha mwenyewe ni vigumu mtu mwingine kukuthamini, kujithamini kuanzia ndani ya roho na mwili wako na hadhi yako kama binadamu kamili, hapo hata wengine wanaweza kukuthamini

Ni kweli kujithamini au kuthamini wengine kunatokana na kujitambua wewe binafsi. Na hili kujitambua wewe binafsi inabidi ujue tamaduni za jamii inayokuzunguka iwe kazini, familia au hata Pub. Kwa kujua hilo ndio utaweza kushusha au kupandisha vigezo kutokana na maisha ya jamii hiyo.

Mara nyingi ukijishusha kwa kiasi fulani utakuwa na uwezo mzuri wa kujitambua na kujichaganya na kukubalika na jamii sehemu yeyote hile..hata pale nyumbani kwako jaribu kujishusha na kuthamini kazi za House girl au Houseboy wako..jaribu kumfanya kama mdogo wako na uone matokeo yake.... Pia tukumbuke hakuna kipimo cha thamani..sio cheo, wala hela, wala mavazi, wala mikogo..wala kutoa misaada..vyote hivyo havisaidii kupandisha thamani yako ..Thamani ni kukubalika..na kuheshimika kwa kujishusha kwako albeit ilibidi uwe juu... Hata walevi wanathamani na kuthaminiwa wakikutana kwenye jamii za walevi wenzao..ni utamaduni na vigezo vyao. Hapo utaona thamani inakuja yenyewe na wala sio wewe unayeiweka au kuilazimisha... kikubwa.. Jitambue..jishushe ili wale wanaokuzunguka ndio wakupandishe..
 
Mr Rocky za siku nyingi? Gud to have you back!

Eti eh! Ah kweli binadamu tupo wa aina nyingi! Mwenzako hiyo ndo anaiona hoja baab kubwa!

Mbu kuhusu kuchukua hatua pale unapohisi kutumiwa kwa faida ya wengine mh kweli wengine tunahitaji therapy.....huwa tuna ile ya namwachia Mungu ...sasa sijui hatujiamini au kujithamini!?

...lol, mwj1 hii ni topik yake inayojitegemea.
Kwa kifupi, jichunguze hao wanaokutumia wanakutumia kwa mambo gani?

Kama ni kazini, jichunguze kwanini wewe ndio uelemewe na majukumu ya hizo kazi
kama ni nyumbani, jichunguze kwanini wewe ndio uelemewe na majukumu ya ulezi
kama ni familia, jichunguze, nini mtazamo wa wazazi, nduguzo kuhusiana na majukumu yako kwao
nk,...nk...

Kumbuka, sio kila jukumu lina shari nawe. Kuna majukumu yanakusaidia kukupima uwezo wako,
yanakupa challenges za kazi, maisha nk...Be positive kwa challenges hizi. Zipokee kwa mikono miwili.

Ila kuna Challenges za 'kijinga,'...mfano, kuachiwa watoto uwalee, nduguzo uwasomeshe,...eehhh?
 
Ni kweli kujithamini au kuthamini wengine kunatokana na kujitambua wewe binafsi. Na hili kujitambua wewe binafsi inabidi ujue tamaduni za jamii inayokuzunguka iwe kazini, familia au hata Pub. Kwa kujua hilo ndio utaweza kushusha au kupandisha vigezo kutokana na maisha ya jamii hiyo.

Mara nyingi ukijishusha kwa kiasi fulani utakuwa na uwezo mzuri wa kujitambua na kujichaganya na kukubalika na jamii sehemu yeyote hile..hata pale nyumbani kwako jaribu kujishusha na kuthamini kazi za House girl au Houseboy wako..jaribu kumfanya kama mdogo wako na uone matokeo yake.... Pia tukumbuke hakuna kipimo cha thamani..sio cheo, wala hela, wala mavazi, wala mikogo..wala kutoa misaada..vyote hivyo havisaidii kupandisha thamani yako ..Thamani ni kukubalika..na kuheshimika kwa kujishusha kwako albeit ilibidi uwe juu... Hata walevi wanathamani na kuthaminiwa wakikutana kwenye jamii za walevi wenzao..ni utamaduni na vigezo vyao. Hapo utaona thamani inakuja yenyewe na wala sio wewe unayeiweka au kuilazimisha... kikubwa.. Jitambue..jishushe ili wale wanaokuzunguka ndio wakupandishe..
Kweli kabisa Tulizo, ila sie waafrica hapo bold huwa ngumu sana, wengi wetu kujishusha ili tupate faida fulani hatuwezi, natokeo yake kila mtu kichwa juu hata kwenye jambo anaona kabisa anatakiwa aje chini lakini hakuna
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kwa nini najithamini? ni hivi, dunia nzima kuna watu zaidi ya bn. ngapi? and who will give a damn about me other than myself??!..nobody!

Vyovyote ulivyo lazima mtu ujithamini, ukisubiri kuthaminiwa itakula kwako. yes, kuna muda mwingine mtu ukikutana na matatizo unaweza kujiona huna thamani lakini maisha ni pande zote na ukifahamu hili unatakiwa kutatua matatizo kwa kadiri ya uwezo wako.

Sijui aisee, najithamini na kujijali sana katika haya maisha!!..
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom