I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,929
- 10,747
Kunguru ni ndege mwenye sifa za kipekee sana. Mmoja kati ya ndege anayejulikana sana duniani. Je, unafahamu nini au umewahi kusikia jambo gani kumhusu ndege huyu? Ngoja tumpe maua yake.
1. Kunguru wana akili kinoma noma. Ni kama akili walizo nazo watoto wa miaka saba kwa upande wa binadamu. Watu mbalimbali wmeshuhudia hawa jamaa wakiangusha vitu vigumu kulika toka juu hadi chini mfano barabarani kwenye lami au kuvitega njiani magari yakanyaje ili vitu hivyo vivunjike wale vya ndani.
2. Kunguru ni waaminifu kwa wenza wao. Inasemekana; kunguru huzaa na kulea jike au dume moja tu maisha yake yote. Na mmoja kati yao akifa; basi huyo mmoja atabaki single hadi atakapokufa. Kunguru hana baya!.
3. Kunguru ni mzuri katika kukariri. Kunguru wanauwezo wa kukariri sura ya mtu mbaya kwao na kubebelea kinyongo cha kulipiza kisasi hapo baadae.
4. Kunguru wana lugha na lafudhi zinazotofautiana. Kwa kila eneo Kunguru wa eneo hilo husika huwa na lugha yao. Kwa maana kuwa kunguru huwa na sauti moja ila namna ya utoaji wa sauti hizo hutofautiana kati ya Kunguru wa eneo moja hadi jingine. Watu wanaoishi na kunguru maeneo yao wataelewa zaidi point hii.
5. Kunguru huuzunikia na kuaga mwili wa maiti ya Kunguru mwenzao. Jambo hili ni nadra sana kwa viumbe wengine hasa aina nyingine ya ndege. Mara kadhaa Kunguru wameshuhudiwa kukusanyika kwa wingi hadi kwa makumi na mamia katika eneo ambapo kuna mwenzao kafia.
6. Kunguru huchelewa sana kuoza akifa. Na hata kuoza kwao huchukua muda mrefu na taratibu sana tofauti na viumbe wengine. Hapa ndipo huja ile dhana ya wengi kufikiri kunguru hawaozi ila kumbe sivyo!.
7. Hawa jamaa ndiyo ndege pekee mwenye ubongo mkubwa kuliko ndege mwingine yeyote.
8. Wanauwezo na ujuzi mzuri wa utatuzi wa changamoto mbalimbali. Inaelezwa kuwa wanaweza pia kutumia zana tofauti tofauti kufanikisha matakwa yao. Viumbe wengine wanaofaamika kutumia nyezo ni binadamu, Orangutans, Chipanzee na sokwe.