unajua IQ ya mtu inatafutwaje?

unajua IQ ya mtu inatafutwaje?

chronological age: huu ni umri wa mtu alio nao, kama una miaka 20 basi chronological age yako ni 20 years

mental age: huu ni umri wa akili ya mtu, kama una miaka 10 na unaweza kufanya vitu ambavyo tunategemea afanye mtu wa miaka 15 basi mental age yako ni 15 years

IQ=(mental age/chronological age) x 100

mfano: ukiwa na miaka kumi unafanya vitu vya mtu wa miaka kumi

10/10 x100=100 hii ndio IQ ya mtu wa kawaida
umri unapoongezeka vigezo vinachange kwa sababu reference ya mental age inakosekana.
nowander sex ingekuwa kigezo wabongo tungekuwa magenius !

sijakuelewa kabisa, na hivyo vitu vya kufanya ni vitu gani cause naona ndio vinabeba IQ, miaka kila mtu anayo.
 
Rule of thumb formula for IQ -fool me once shame on you, fool me twice shame on me.
 
maana yake kuambizana iq kubwa na nini ni kudanganyana bila test kufanyika au una maanisha nini??
 
Deepness, speed and acuracy of thinking in relation tu ur age ndo vitu vinavyotumiwa kupima iq mkuu kiasi kuwa hata mtoto wa miaka 8 anaweza mshinda mtu wa 20 year. Kuna free test ya iq online unaweza jaribu.
 
Mkuu Red Giant, inaelekea umeanzisha kitu bila kutoa ufafanuzi wa kutosha. Wengine tunalearn hapa jamvini mambo kibao. kama IQ huwa inakuwa na kuboreka basi na yangu iko njema sasa, lakini ukianzisha kitu si dhambi ukadefine na kutoa maelezo ya kina, km ulivyoshauriwa.Mkuu Kiranga, nakufurahia sana, infact you are genius, kila comment zako zina mantiki, saidia basi kutuelimisha mana mleta uzi ni full mizaha, na anafikiri intelligence tu ndo wana haki ya kuelewa, then hata kutafuta IQ wangejua isingewekwa hapa jukwaani. I'm eager to learn, give me more.
 
Pamoja na hayo,IQ ya mtu hupimwa kwa muda mrefu,kupitia shughuli mbalimbali anazopewa afanye chini ya uangalizi wa siri.
 
Ningeomba mtu anikalukuletie IQ ya Ritz wa JF na Mwigulu Nchemba wa Magambaz
 
je iko effective kwa adult???
kwa adults mara nyingi haiko effective. sababu kadri umri unavyoongezeka ewezo wa akili wa watu unapungua,mtu mwenye miaka hamsini mara nyingi huwa nauelewa mkubwa kuliko mtu mwenye miaka sitini au sabini. tofauti na watoto ambao tunategemea mabadiliko ya akili huenda sambamba na umri. kama sijasahau limit ya formula ni miaka 16. kwa watu wazima huwa inakuwa modified na zinatumika mbinu zingine bila kuingiza kipengele cha mental age.
 
Deepness, speed and acuracy of thinking in relation tu ur age ndo vitu vinavyotumiwa kupima iq mkuu kiasi kuwa hata mtoto wa miaka 8 anaweza mshinda mtu wa 20 year. Kuna free test ya iq online unaweza jaribu.

iko wap hyo?
 
Nahis IQ yangu ilikuwa kubwa sana sema tu hakupatikana mtu wa kunipima mfano; nilikuwa wa kwanza kuwaandikia majina wanafunzi wenzangu kwenye madaftari turipoanza darasa la kwanza. Niliweza kubuni mbinu ya kuchagua ng'ombe yupi atoke kwenye zizi bila ya kutoa amri ya saut,(NIMEKULIA USUKUMAN) yaan nikiangalia tu anajua anatakiwa atoke, mpaka kufikia darasa la tatu nilikuwa nimeishasoma vitabu vyote vya kiada mpaka vya darasa la saba na vingine ambavyo nilikuja kugundua nilipofika form 3 nilipoambiwa vinatumika kujbia maswali ya fasih. Baadhi ya Maswali niliyokuwa najiuliza pindi nilipokuwa darasa la tano nimetafuta majibu yake mpaka leo inaonekana hayan majibu halafu ni ya kisayans sio ya kiiman so na mpango wa kujaribu kufanya research siku zijazo.
HAYA KOKOTOA HAPO IQ YANGU NI NGAPI
 
Mental age/Umri wa Akili hupimwa kwa uwezo wa kiutendaji wa ubongo wa mtu. Kama mtu wa miaka 15 anaweza kufikiri, kutatua tatizo na kutenda kazi ambayo ingefanywa na mtu wa miaka 20 basi Umri wake wa akili/ Mental age ni miaka 20 na Umri wake wa kuzaliwa/ Chronological age ni miaka 15. Kiurahisi zaidi mtoto wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka 7 (chronological age) akipewa hesabu za mtoto wa darasa la tatu mwenye miaka 9 na akaziweza vizuri basi mtoto huyu wa miaka 7 atapewa daraja la Umri wa akili/mental age ya miaka 9. Hivyo Ukichukua Mental age (Umri wa akili) ukagawa kwa Umri wa Kuzaliwa (Chronological age) kisha ukazidisha kwa 100 jibu lako litakuwa kati ya makundi haya hapa chini: Jipime
Grade Range Percent
Genius/Kipaji maalumu/Uwezo usio wa kawaida:144 >.
Gifted/Uwezo wa juu sana:130-144.
Above average/Uwezo wa juu: 115-129.
Higher average/Wastani: 100-114.
Lower average/Wastani wa chini: 85-99.
Below average/uwezo duni: 70-84
Borderline low/Taahira kiasi: 55-69.
Low/mtindio wa ubongo <55
 
Je ni IQ pekee ndio inamfanya mtu aonekane mahiri au kumudu mambo yanayofanya maisha yake kwa ujumla?
Vipi kuhusu Quotient nyingine zinazojumuishwa na IQ kumfanya mtu kuwa bora na sahihi kwenye maisha? Quotient kama IQ (Intelligence Quotient), SQ (Spiritual Quotient); PQ (Physique Quotient); EQ (Emotional Quotient); and name it ...
 
iNAWEZAJE kuleta tofauti kama data ni ya chronological age?! akiwa na 10yrs unaweka 10, akiwa na 20yrs unaweka 20; huoni kwamba kwa formula yako watu wote wenye umri sawa watakuwa na IQ moja something which is necessary as along as hata wa umri mmoja IQ zinaweza kuwa tofauti.......
 
Anaziwezaje bila ya kufundishwa? Kwani ukimfundisha mtoto wako wa miaka mitano kuwa maji ni oxygen na hydrogen na akaulizwa na akajibu hivyo kwa kuwa ni swali la form one basi tutamwona kuwa ana akili za mtoto wa form one?!
 
Nahis IQ yangu ilikuwa kubwa sana sema tu hakupatikana mtu wa kunipima mfano; nilikuwa wa kwanza kuwaandikia majina wanafunzi wenzangu kwenye madaftari turipoanza darasa la kwanza. Niliweza kubuni mbinu ya kuchagua ng'ombe yupi atoke kwenye zizi bila ya kutoa amri ya saut,(NIMEKULIA USUKUMAN) yaan nikiangalia tu anajua anatakiwa atoke, mpaka kufikia darasa la tatu nilikuwa nimeishasoma vitabu vyote vya kiada mpaka vya darasa la saba na vingine ambavyo nilikuja kugundua nilipofika form 3 nilipoambiwa vinatumika kujbia maswali ya fasih. Baadhi ya Maswali niliyokuwa najiuliza pindi nilipokuwa darasa la tano nimetafuta majibu yake mpaka leo inaonekana hayan majibu halafu ni ya kisayans sio ya kiiman so na mpango wa kujaribu kufanya research siku zijazo.
HAYA KOKOTOA HAPO IQ YANGU NI NGAPI

ni 70 80
 
Back
Top Bottom