Unajua kuwa Tanzania Haina Admiral wa Navy?

Kwangu mimi huku tuna makuruta tu kulingana na system ya kivita ya sasa.

Vita ya Sasa ni akili naa hesabu na jeshi dogo linalotumia nguvu ndogo na tunakoendea hata infantry itakuwa na robots + autonomous tankers huko angani full drones na missiles.

Kwasasa tunapaswa kujikita sana kuboresha mitaala ya shule huko chekechea, primary na secondary ili tuwe na watalaam wengi wa technolojia ili tuwe capable kwenye softwares, programing, kutengeneza military hardwares kwa speed, haraka, wingi nk.

Hizbollah, Hamas, IS nk wana askari shupavu, wavumilivu, wenye morally ya vita, nk lakini hawana vifaa vya kisasa kwa maana technolojia kama aliyonayo adui matokeo yake adui akiwa na askari 10000 wewe unahitaji askari milioni moja ambao wote ukiwa na fleet ya drones kadhaa na autonomous Hellicopter gun ship unawamaliza kama nzi vile.
 
Mtu kuwa 4 star General wa Army ni rahisi kuliko kuwa Admiral. Kuwa Admiral lazima uwe vizuri kuliko maelezo, jeshi la majini lina changamoto nyingi sana kuliko jeshi la ardhini.

Tanzania hata corvette hatuna, hata missile boats tu hatuna. Sasa Admiral kwetu hana kazi, Tanzania ikilazimika ipeleke task force ya wanajeshi walau 2,000 kwenda Madagascar ndani ya voyage moja haiwezi sasa Admiral wa nini.
Una shule ya sekondari unataka uchague Professor awe Vice Chancellor badala uridhike na Mwalimu Mkuu.

Kwanza Admiral atakaa flagship gani, hizi boti ambazo silaha yake kuu ni heavy machine gun.

Kwa Afrika naona nchi inayostahili Admiral bila kupepesa macho ni Algeria. Ndio wapo serious na Navy.
 
Mboma alitokea Air Force, CMI wa sasa simfahamu.
 
Umesema "Captain wa Army ni sawa na Lieutenant wa Navy". Hii si sahihi. Captain wa Jeshi la Nchi Kavu analingana na Lieutenant Commander wa Jeshi la Wanamaji.
Hapana; Lieutenant Commander wa Navy ni sawa na Major wa Army. Katika majeshi ya nchi nyingine anajulikana pia kama Lieutenant Commodore (LCDR). Commander au Commodore ni sawa na Lieutenant Colonel wakati Navy Captain ni sawa na Colonel
 
Kama wewe ni mwanajeshi ama ni mtu tu unayeelewa mambo ya kijeshi, basi kuna kitu haukielewi sawa sawa.

Kabla ya mabadiliko ya mfumo wa vyeo vya jeshi la Navy miaka ya karibuni, kamandi za majeshi yote zilitumia vyeo vyenye kufanana, yaani vya Army.

Lakini vyeo vya Navy vilipobadilishwa, kuna barua nadhifu ilitolewa kufafanua kila cheo kulinganishwa na vyeo vya Army/Air force.

Kwa hiyo kila cheo cha afisa ama askari wa Navy kina ulinganifu wa cheo cha afisa ama askari wa Army/Air force na equivalent rank huwa haizidi cheo inacholingana nacho.

Chukulia mnapokutanishwa majeshi ya mataifa mbali mbali cha kwanza huwa ni kutafsiri equivalent ranks, yaani cheo hiki ni sawa na cheo kipi kwa jeshi jingine.

Tukija kwenye upandishwaji wa vyeo kutofikia cheo flani, hilo lipo wazi, vyeo vya jeshi hufuata muundo.

Hata mkuu wa majeshi aliyepo sasa, cheo alichonacho hakimstahili, alistahili cheo cha chini yake, kwa wajuzi wa mambo tunaona kama anavaa cheo cha kisiasa.

Jeshi kimuundo, ukishatoka Brigade, kuna Division, baada ya divisheni kuna corps na baada ya hapo kuna Army.

Uhalali wa vyeo kimuundo upo hivii: Brigade inaongozwa na Brigadier general, Division inaongozwa na major general, corp inaongozwa na Lutenant general na Army inaongozwa na General.

Hizi command za majeshi zilizopo Tz zina hadhi ya Divisions na viongozi wake ni major generals ambapo ni sawa.

Baada ya hapo kimuundo inafuata Corp ambapo jeshi letu ndiyo limekomea, na cheo kinachostahili ni Lutenant general na siyo General kama tukifuata muundo.

Kwa hiyo Cdf wa Jwtz alitakiwa awe Lt general.
 
Kijana unajua Admiral wewe.
Flat top tu-Carrier ya kijeshi inayobeba nde hata zaidi ya 50, inaongozwa na Captain.
Sisi tuna viboti vidogo vidogo tu, ambavyo havina uwezo mkubwa.
Admiral ni cheo kikubwa sana.
Admiral ni cheo cha Kijeshi. Hata kama fleet size yetu siyo kubwa na inaongozwa na Rear Admiral kama ilivyo sasa; iwapo mtu huyu atateuliwa kuwa COS asiitwe Lt General bali aitwe Vice Admiral, na akiteuliwa kuwa CDF basi aitwe Admiral siyo General. Lakini ninavyoelewa maafisa wa Navy wanapoteuliwa majukumu mengine makao makuu huvalishwa vyeo vya Army. Mmojawa ni Lt General Yakub Mohammed aliyekuwa COS, huyu alikuwa afisa wa navy kabla ya kuteuliwa kwenye nyadhifa nyingine za makao makuu ya jeshi na kupewa vyeo vya Army.
 
Umezunguka sana lakini hiyo siyo topiki niliyoandika hapa. Kutokuwa na Admiral siyo kosa, ni muundo tu wa jeshi; ni kueleweshana tu kuwa kwenye muundo wetu hatuna Admiral basi. Hata Israel yenye jeshi active sana hawana hata Rear Admiral; mkuu wa Navy Israel ni Commander (Commodore) na mkuu wa majeshi ni Lt General. yaani Israle hakuna General..
 
Hiv navy yenyewe si ni kaji section tu kanako exist hapa fery pekee,, au mpaka mpaka mpanda hukoo na Iringa kuna Navy?? 😂
 
Unajua kuhusu Egypt mzee
 
Hii ndio laha ya kushiba alafu ukalala chini ya mwembe.
 
Israel haijawahi kuwa na General, hata wafanye vizuri vipi vitani huwa hawawapandishi vyeo kufika General. Hata Moshe Dayan alikuwa Major General.

Ila Israel haikuwa na bado haina Navy kubwa ya kulazimika kuwa na Admiral. Total displacement yao ni ndogo ukiachana na Sa'ar series za missile boats na corvettes na hizi diesel subs za Dolphin class hawana major surface combatants.

Nimekumbuka ambavyo ni vigumu kumuona Grand Admiral kwenye majeshi. Ni rahisi kuwaona Field Marshals watano duniani kuliko kumuona Grand Admiral mmoja. Nazi Germany ilikuwa na Field Marshals wengi kina von Manstein, Paulus, Keiter, Jodl, von Rundsdedt, Rommel, Kesserling, n.k.
Alafu ikawa na Grand Admiral wawili napo ni Karl Donitz alishika nafasi ya Erich Raeder.
 
Sahihi. Hata Israel the highest military rank I mean Mkuu wa Majeshi ni Lieutenant General. Najaribu kuwaza CDF akikutana na yule wa Israel equivalent inakuwaje? Ufafanuzi tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…