Waterbender
JF-Expert Member
- Oct 2, 2018
- 7,573
- 10,063
ebu youtube link nisikie akihubiri
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapo sasa...Nabii akitaka mafanikio tumchangie….ila waumini awaombee ili nao wapate
Hakuna manabii mkuu kuna waganga njaa tu wanaotapeli wajinga walokubali kutapeliwa.Nabii ni mjumbe wa Mungu. Hata katika zama hizi tunazoishi mimi na wewe bado kuna manabii, na wataendelea kuwepo mpaka pale Mungu atakapokuwa hana mahusiano na mwanadamu.
Manabii zamani walikuwa wanatengenezwa na Mungu,siku Hz Kuna "self made nabiis"Nabii ni mjumbe wa Mungu. Hata katika zama hizi tunazoishi mimi na wewe bado kuna manabii, na wataendelea kuwepo mpaka pale Mungu atakapokuwa hana mahusiano na mwanadamu.
Ninatamani sana ungefika kwenye kongamano, kuna namna mtazamo wako juu ya watumishi wa Mungu ungebadilika.Manabii zamani walikuwa wanatengenezwa na Mungu,siku Hz Kuna "self made nabiis"
Kuna mtu anaitwa Egbert Angel ni "pastor" kule zimbabwe,ni balozi na ni mjomba wa Raisi Emerson Mnagangwa,huyu amehusika na mtandao wa wizi wa dhahabu Afrika,Kuna mazingaombwe alikuwa anawafanyia waumin wake eti watapokea pesa za ajabu kwa mihamara ya simu,
Tafuta documentary gold ya aljazeera uone jinsi Hawa manabii wa mchongo wanavyoishi,
Na waumini wengi wa haya makanisa Elimu ni form 4 kwenda chini,na haya makanisa huwezi kukuta yamefunguliwa mbezi kunduchi,masaki,ni mbagala,kawe,
Kupata kazi nzuri,kusomesha watoto,ni matatizo ya kiuchumi sio kiroho,kila mtu anatakiwa aende kanisani kumuabudu Mungu,hqijqlishi kiwango Cha Elimu.Ninatamani sana ungefika kwenye kongamano, kuna namna mtazamo wako juu ya watumishi wa Mungu ungebadilika.
Watu wanatakiwa kumjua Mungu, hapo ndipo watajua manabii wa michongo ni wepi na wa kweli ni wepi.
Wafuasi au washiriki wengi wa 'haya' makanisa kuwa na Elimu za form four kushuka chini sina takwimu nalo, ila ni wazi kuwa hawa ni wahitaji zaidi kuliko wenye shahada moja na kuendelea.
Watu wa form four wanataka Mungun awasaidie wapate elimu za juu, wanataka wapate kazi nzuri, wasomeshe watoto wao, wanataka wapate furaha maishani - mtu mwenye vyote hivyo na vimempata kibahati - unaweza usimkute makanisani au katika makanisa 'haya', ingawa wapo wengi tu wana mpaka shahada za uzamivu ni waumini wa 'haya' makanisa.
Hata hivyo Bwana Yesu haangalii elimu ya mtu wala kazi wala kabila, anaangalia moyo. Anataka umuabudu kwa moyo na kweli. Soma Mithali 15:8-9 inasema hivi;
Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.
Tatizo la kiuchumi lililosoviwa kiroho.Kupata kazi nzuri,kusomesha watoto,ni matatizo ya kiuchumi sio kiroho,kila mtu anatakiwa aende kanisani kumuabudu Mungu,hqijqlishi kiwango Cha Elimu.
Hata sie wenye Elimu kubwa tunaenda makanisani,lakini sio kwenda kulala chini ya miti kawe Tanganyika pakers tukisubili miujiza ya Mwamposa,ituondolee umaskini.
Hata hao wenye Elimu kubwa na ukwasi hawakuzaliwa nao,Kuna kipindi walikuwa wahitaji,matatizo yao hayakuisha kwa miujiza,kazi ilifanyika.
Waumini wengi wanaoenda "kuombewa"kulamba chumvi,kunywa maji,kukanyaga mafuta,wanashida za kiuchumi,matatizo yao hayataisha kwa miujiza na kuombewa,mipango ya kisayansi inahitajika,wapate kipato.
Kuhusu kwenda kwenye kongamano,Dunia ipo mikononi,Nina wahubiri wengi ninaowafatilia,Dr Myles Munroe,pastor John hagee,nk.
Hawa wanafundisha,wanaandika vitabu,wanatoa masomo heavy,sio story za kukanyaga mafuta,na kuambiwa una "roho ya kukatawaliwa"
"Manabii"wetu wengi Wana take advantage ya raia wenye shida za kiuchumi,wanaogitaji neno la faraja.
Kama unafatilia Citizen ya Kenya,pastor Mackenzie aliwaaminisha waumini wake wafunge mpqkq wafe Ili wakamuone Yesu,upuuzi mtupu,miili 90 imepaprikana.
Kuna yule pastor wa Agape TV,mtoto wake Fernandez,ndie mvumbuzi wa app ya Nara,inayotumika kuhqmisha pesa duniani,kijana alikataa mshahara wa milioni ,500 Ili aanzishe kampuni yake.
Sasa unafikiri huyu kijana amefikia hapo kwa kwenda kanisani kukanyaga mafuta?,amefanya kazi,amesokeshwa na wazazi wake.
Makanisa Mengi ni miradi ya watu inawafsnya waumini chanzo Cha kipato,hao manabii wenu,wakitaka gari,tunaxhanga,ila muumini akitaka school fees anaambiwa,afunge na kuomba.
Sasa hv makqnisa ya "kilokole"yanaanzishwa kila Kona,ila tajiri nicmmoja tu,nabiis,waumini wengi ni maskini,