Unajua kwanini binadamu hakuumbwa kwa neno moja tu la Mungu?

Unajua kwanini binadamu hakuumbwa kwa neno moja tu la Mungu?

GRAMAA

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2014
Posts
1,241
Reaction score
3,800
Ipo hivi mifugo wezangu, hivi kwanini Mungu hakutamka tu hivi "na awe binadamu mwanaume na mwanamke na wakaishi kwenye bustani ya edeni” ikawa asubui ikawa jioni, siku ya sita?

Mbona vitu vyote Mungu alikuwa anatamka neno tu na vinatokea lakini ilipofika siku ya sita kwenye kipengele cha kumuumba binadamu Mungu hakutamka tu neno NA "AWE BINADAM MWANAUME NA MWANAMKA" ila alianza mchakato wa kuwaumba.

Binadamu ana uspesho gani mpaka Mungu ashindwe kumuumba kwa kutamka tu neno la NA AWE BINADAMU?

Inakuaje mpaka Adam alazwe usingizi mzito ndiyo Hawa atolewe kwenye ubavu wa kushoto wa Adam wakati Mungu alikuwa na uwezo wa kusema tu "NA AWE HAWA MKE WA ADAM"

Wanyama, wadudu, ndege, samaki n.k walitamkwa tu kwa neno na Mungu na wakatokea wakiwa wanauhai wa pumzi. Na wanyama wengi na ndege wengi wa kike ni dhaifu sana kwenye jamii yao wanayoishi dhidi ya jinsia ya kiume. Mfano kuku mwanamke hawezi kumfanya lolote jogoo.

Sasa iliwezekanaje Mungu aweze kutamka tu "na wawe wanyama na ndege wa kike" na wakatokea ila ilishindikana kusema tu "NA AWE HAWA" ila cha ajabu ujio wa Hawa ulimlazimu Adam alazwe usingizi mzito.

Au nyani mwanaume naye alilazwa usingizi mzito ili kumpata nyani wa kike kutoka kwenye ubavu wa kushoto ila mwandishi wa biblia alisahau kutuandikia?

Hivi na sisi binadamu tungeumbwa kwa neno tu kwa kutamkwa na Mungu tungekuwaje?
 
Back
Top Bottom