Unajua kwanini Klabu ya Yanga inaitwa Gongowazi na Ndala? Usikose ukaambiwa

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Ni FlashBackSaturday kuelekea kwa pambano la DSM Derby siku ya Jumapili, Unajua kwanini Klabu ya Yanga wanaitwa Gongowazi na Ndala?

Majina haya kiasili yalianza kuvuma sana mwishoni mwa miaka ya Hamsini kwenye karne iliyopita sababu kuu moja.

Yanga SC hawakuwa wanacheza na jezi wala viatu, ni vibukta na pekupeku huku over 90% ya fans wao mwendo wa malapa.

Sasa yuko mhindi alikuwa na duka lake pale Independence Street (Samora Avenue) akiitwa Jeetu Kumar ambaye ndio mtu wa kwanza kuwanunulia Jezi, huku Klabu ya Sunderland (Simba) ikiwa na Jezi na Viatu.

Siku aliponunua akawaambia haifai timu kucheza 'Mgongo Wazi' bahati mbaya yule mhindi hakuweza kutamka vizuri, akasema Gongowazi.

Na neno Ndala ni kwa Washabiki wao ambao hadi leo kwa sehemu kubwa chini ni ile kitu ya kwendea msalani.

 
Sijui unajua wewe, ila mimi nimesema hakukuwa na club iliyokuuwa inaitwa simba.
Mkuu..mbona unaona uzito kujibu swali langu? Au labda tufanye hivi Sunderland kwa sasa inaitwa Coastal Union..Unaonaje hapo!!!
 
Na Sunderland yenyewe haikuwa ya watu weusi kama wewe.
Mbona katika historia huandikwa Yanga ilianzishwa mwaka mnamo1935

Na Simba mwaka 1936 bila kujali kama hakuna klabu ya Simba kwa wakati huo ya watu weusi? Hii imekaaje?
 
Utakuwa umeichangia Yanga baada ya Vichekesho hivi[emoji3][emoji3][emoji196][emoji196]
 
Miaka 60 baadae zote hazina hata viwanja!!
Exactly mkuu..Wengine tunamiliki vichaka Bunju

Na kuna wengine wanamiliki bwawa la kufungia Vyura na Konokono
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…