Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Unajua Kwanini Wachagga Hawali Muhogo? [TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD]
Na Mwandishi Wetu
WACHAGGA ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu wanaoishi au kaskazini mwa Tanzania kandokando ya Mlima Kilimanjaro, huku mkoa wao ukichukua jina la mlima huo mrefu kuliko yote Afrika.
Tafiti zilizowahi kufanywa zinaonyesha kuwa Wachagga ni kabila la tatu kwa ukubwa kati ya makabila zaidi ya 120 yanayotambulika nchini Tanzania.
Waachagga ni mkusanyiko wa makabila madogo madogo yaliyosambaa kijiografia kuuzunguka Mlima Kilimanjaro kuanzia mashariki (Tarakea, Rombo) hadi magharibi ya Mlima Kilimanjaro (Siha, Machame).
Makabila yanayounda Uchagga ni Warombo, Wamarangu, Wa-Old Moshi, Wakibosho na Wamachame bila kuwasahau Wakirua-Vunjo, Wauru na Wasiha.
Lugha yao
Kichagga kwa kawaida hubadilika kulingana na maeneo kutoka mashariki hadi magharibi mwa mlima.
Kutokana na tofauti hizo, Kichagga kimegawanyika katika makundi yanayofahamika kimaeneo kama Kirombo (wanatokea Rombo), Kimarangu (kutoka Marangu) na maeneo mengine.
Lugha zote zinakaribia kufanana hasa maeneo ya mipakani. Kwa mfano, Ki-Old Moshi kinafanana na Kikirua wakati Kikirua kikifanana kidogo na Kimarangu.
Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame, wakati Kimachame pia kinafanana kwa kiasi fulani na Kikibosho.
Inasemekana baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru, Arusha na kuchanganyika na Waarusha. Hapo ndipo lugha yao ikabadilika na kuwa Kimeru. Na kwa sababu hii Wameru wanasikilizana na kuelewana na Wamachame, licha ya kwamba lafudhi zao zinatofautiana kidogo.
Elimu
Wachagga wanajulikana sana kwa uwezo wao mkubwa wa kufanya biashara na kushiriki kwenye kilimo.
Moshi ni miongoni mwa maeneo ya mwanzo Wamisionari walikojenga makanisa na shule. Hii ndiyo sababu iliyowafanya Wachagga kuwa miongoni mwa makabila yaliyopata sana elimu.
Takwimu zinaonyesha kuwa Mkoa wa Kilimanjaro kwa sasa unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya shule za sekondari nchini. Hadi Aprili mwaka huu, kulikuwa na shule za sekondari zaidi ya 320 wakati shule za msingi zikiwa pia katika idadi kubwa kuliko mikoa mingine.
Kilimo
Wachagga pia hujishughulisha na kilimo cha ndizi, mahindi, maharage, viazi, ulezi na mboga mboga. Vile vile wanayo mazao ya biashara kama kahawa, nyanya na vitunguu. Haya huwasaidia kukidhi mahitaji yao ya kila siku kwa kuwapatia kipato.
Chakula chao
Pamoja na kwamba Wachagga wanakula vyakula mbalimbali kama ugali, wali na viazi, lakini ni ukweli usiopingika kuwa chakula chao kikuu ni ndizi. Wana ndizi za aina mbalimbali zinazotayarishwa kwa namna malimbali pia.
Wachagga hupendelea sana ndizi mshale mbichi zinazoandaliwa kwa kukatwakatwa, kisha hupikwa kwa kuchanganywa na nyama ya ngombe, kondoo au mbuzi.
Lakini ndizi hizo zinaweza pia kupikwa kwa kuchanganywa na maharage, choroko, kunde na wakati mwingine maziwa mtindi huku zikiwa katika ladha tofauti kama mtori, machalari na kiburu.
Inaaminika kuwa Mchagga halisi hali muhogo akiamini kuwa akila atakufa. Hii ni kwa mujibu wa historia ya mababu wa Kichagga wanaosemekana kuwahi kupanda mihogo lakini walipokula walikufa.
Inawezekana kuwa ni kweli kwani ipo mihogo yenye sumu aina ya sianidi, ingawaje makabila yaliyozoea kula mihogo huiloweka kwa muda na kuondoa sumu hiyo.
Huenda Wachagga wa zamani hawakuijua mbinu hiyo ingawa watani zao na majirani zao - Wapare, walikuwa wameshaizoea na mihogo ni chakula chao kikuu.
Mbali na kilimo, Wachagga pia ni wafugaji na hupendelea zaidi kufuga nguruwe na mifugo mingine.
Mapenzi ya kufuga nguruwe na kula nyama yake yaliwapa shida sana Wachagga waliohamia maeneo ya pwani, hasa Dar es Salaam, ambako wakazi wengi wa huko ni Waislamu na kwao nguruwe ni haramu (kharam mutlaq)!
Majina
Majina ya kiukoo ya Kichagga huashiria maeneo wanakotoka japokuwa si lazima sana kuwa hivyo. Miongoni mwa familia au koo maarufu za Kichagga ni Kimaro, Swai, Massawe, Mushi, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi na Meena wakitokea Machame.
Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kimambo na Tesha wenye asili ya Old Moshi na Vunjo, wakati Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Lamtey, Mramba na Kauki wanatokea Rombo, bila kusashau akina Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Mtui, Mushi, Meela, Minja, Njau wanaotokea Marangu.
Wachagga hupendelea sana kurudi Moshi kama walikuwa nje ya huko wakati wa Krismasi.
Watu wengi hudhani kuwa Wachagga wameathiriwa sana na Ukristo kwa kuwa wengi wao ni wafuasi wa dini hiyo, lakini ukweli ni kwamba kipindi cha Desemba huwa ni cha mapumziko baada ya kumaliza mwaka uliojaa shughuli za utafutaji pesa (ingawa kuna utani kuwa Mchagga akiona pesa halali hadi azikamate).
Utawala wa jadi
Watawala wa Kichagga waliitwa Mangi. Hawa walihodhi mashamba pamoja na ngombe na waliheshimiwa kama viongozi wa kabila hilo. Akina Mangi walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri.
Mangi Rindi ni miongoni mwa mamangi maarufu hasa kwa kuwa aliwahi kuingia mikataba na wakoloni wa Kijerumani. Mwingine ni Mangi Sina wa Kibosho aliyejulikana kwa uhodari wake kwenye vita dhidi ya Wamachame, alipopora ngombe na mazao yao, wakati Mangi Marealle wa Marangu na Vunjo naye ni maarufu sana hadi leo.
Wakoloni walipofika Kilimanjaro waliingia mikataba na viongozi hawa ili wajiimarishe na kuweka misingi yao ya kikoloni. Ndugu na watoto wa Mangi ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata elimu ya kikoloni, kwa kufanya hivyo walishirikishwa moja kwa moja kwenye serikali za kwanza. Mangi walikuwa mabepari wa kwanza wa kijadi, kwa kuwa walifanyiwa kazi na wengine wakati wao wamekaa tu na kufanya hesabu za mali. Huenda hata ule usemi maarufu wa u mangi-meza ulitokana na tabia za watawala hawa wa Kichagga.
Mila na desturi zao
Haipingiki kuwa ardhi kwa wengi ni msingi wa maendeleo, lakini kwa Wachagga ardhi ni mali kuliko chochote kile, kwa vile wao hutegemea kilimo cha mazao ya kudumu kama kahawa na ndizi.
Kihamba (kipande cha ardhi) ni urithi mkubwa wanaopewa watoto wa Kichagga. Ni hapo mtoto anapotarajiwa kujenga na kuanzisha familia yake, lakini ni bahati mbaya kwamba watoto wa kike walikuwa hawapewi kipaumbele katika ugawaji wa vihamba.
Ni kutokana na uhaba mkubwa wa ardhi Uchaggani ndiyo maana utakuta Wachagga wengi wamehamia mikoa mingine kama Dodoma, Mbeya na Iringa. Huko pia huendeleza shughuli waliyoizoea ya kilimo cha migomba, biashara na ufugaji, hasa wa nguruwe.
Wanaume wa Kichagga hupendelea kufanya shughuli zao mbali na makazi yao, huku wake zao wakiwa nyumbani na kuendeleza shughuli za ufugaji na kilimo. Wanawake wa Kirombo hujulikana kama wafanyakazi hodari na huchangia sana katika kipato cha familia na chakula.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]