Lakini kuna rafiki yangu mmoja kutoka Swaziland, yeye alikuwa anaogopa sana kuitamka Msasani kwa sababu ati kwao ni tusi kubwa. Aliniambia hawezi kutamka neno hilo mbele ya mama yake, maana kufanya hivyo ni kuitamka njia ambayo alitokea kuja duniani kupitia kwa mama yake. Hakuwa straight lakini nadhani nilimuelewa. Yeye mwenyewe majina yake kwa hapa kwetu ni matusi kutamka, lakini alisema ukienda kwao lazima utamke majina hayo kwa sababu ni ya ukoo wao maarufu. Wengi walipenda kumuita jina la kwanza kwa sababu hiyo.
Ni sawa na hapa Tanzania, wewe kama unaitwa NGUMA ukienda Mbeya tafuta jina lingine la kuitwa ukiwa kule, vinginevyo watakutenga wakidhani wewe ni mhuni na huna adabu. Ukienda Moshi naambiwa usiseme KINU kwa maana hiyohiyo. Kuna eneo linaitwa GONJA NDUNGU, ukienda mbeya usiseme hadharani. Ni kama MCHAMBAWIMA ukilitamka Tanzania bara sipati picha palipo na wazee. Kuna watu wanaitwa MBORO kutoka moshi tena ni maarufu hata redioni nawasikia wakitajwa, nadhani wachaga nao wana mambo mwe! Hata bus limeandikwa jina hilo. Nasemaje napanda bus gani kwenda mjini?
Yote haya ni somo kwamba tamaduni zetu zimekaa kama pilau. Inabidi kuheshimu utamaduni wa mwenzio ili naye aheshimu wa kwako. PERIOD!