Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna kamtaa kamoja utapoelekea sinza au ubungo Kinaitwa Sheklango.
Hii imetokana na mzee mmoja alikuwa SheKhe na jina lake akiitwa Kilango
Basi walitamka Shekhe Kilango.
Vilevile Mikocheni imetokana na Miti fulani inaitwa Mikochi. Sasa kwa kiswahili kwenye mikochi una sema Mikochini
Basi watu wakamodifai tu ikawa Mikocheni.
KARIAKOO
Pale ambapo pamejengwa soko, wakati wa vita ya pili ilikuwa kambi ya wapagazi [wabeba vifaa na mizigo ya jeshi] ambao waliitwa 'Carrier Corps'
lakini wenyeji walitohoa jina hilo na kuita kariakoo.
KAWE
Enzi hizo za mkoloni ng'ombe walioletwa toka mikoani walikuwa wakipita njia maalum zilizotayarishwa kwa ajili hiyo njia hiyo iliishia kiwandani tanganyika packers. Wenyeji katika matamshi badala ya kuita COW WAY wao waliita kawe
Kuna kamtaa kamoja utapoelekea sinza au ubungo Kinaitwa Sheklango.
Hii imetokana na mzee mmoja alikuwa SheKhe na jina lake akiitwa Kilango
Basi walitamka Shekhe Kilango.
Vilevile Mikocheni imetokana na Miti fulani inaitwa Mikochi. Sasa kwa kiswahili kwenye mikochi una sema Mikochini
Basi watu wakamodifai tu ikawa Mikocheni.
Mtoni kwa Aziz ally je hili jina limepatikana Vp?
ni jina la mzee Aziz Ally aliyekuwa landlord maeneo hayo kipindi cha zamani
Mtoni kwa Aziz ally je hili jina limepatikana Vp?
Mtoni kwa Aziz ally je hili jina limepatikana Vp?
[h=3]HUSSEIN RAMADHANI SHEKILANGO, SHUJAA ALIYEKUFA AKIIJENGA UGANDA[/h]
Jijini Dar es salaam kuna Barabara Mashuhuri kama 'Shekilango Road', ikianzia maungio ya Barabara ya Morogoro eneo la Nyumba za NHC mkabala na Kiwanda cha Urafiki, ikipitia Mitaa yote ya Sinza na kuishia Maungio ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kituo cha Bamaga.
Ni watanzania wachache wajuao kuwa Barabara hiyo ya Shekilango imepewa jina Maalum kwaajili ya heshima ya Ndugu Hussein Ramadhani Shekilango, aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, akishughulika zaidi na mambo ya Utawala, wakati wa Uongozi wa Rais Julius Nyerere na Makamo wake Aboud Jumbe Mwinyi.
Hussein Shekilango alichaguliwa na Wananchi wa kwao kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Jimbo la Korogwe Mjini, Mkoani Tanga katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1975, akiachia nafasi yake ya Zamani ya Meneja Mkuu wa Shirika la Usagishaji Nchini (NATIONAL MILLING CORPORATION).
Mwaka huo huo akachaguliwa na Rais Julius Nyerere kuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Utawala) akiwa chini ya Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu, ndugu Rashid Mfaume Kawawa.
Tarehe 11 Mei, 1980, ndege ya Kijeshi iliyowachukua Shekilango, Balozi Kilumanga pamoja na Wanajeshi wanne wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ilianguka katika vilima vya Jiji la Arusha na Abiria wote kupoteza Maisha, wakiacha huzuni na majonzi mazito kwa Watanzania.
Shekilango alizikwa Kijijini kwao Jitengeni, Korogwe, Mkoani Tanga, huku akisindikizwa na umati mkubwa wa watu, mpaka leo akibaki Mbunge kipenzi cha watu wa Korogwe na akisifika Serikalini kwa hatua yake ya kurudisha Madaraka Mikoani. Kwa kumuenzi kuna Shule yenye jina lake Jimboni Korogwe.
Mamlaka za Uongozi wa Jiji la Dar es salaam kwa kutambua mchango wa Shekilango kwa Taifa, ikaamua kuipa Barabara mpya iliyokuwa inajengwa wakati huo jina la Shekilango ili kumuenzi shujaa huyu.
Mola amlaze Pema Shujaa Hussein Ramadhani Shekilango
Na Luke Evelyne Singano
KOROGWE YETU: HUSSEIN RAMADHANI SHEKILANGO, SHUJAA ALIYEKUFA AKIIJENGA UGANDA
AFRICAR..!!! Jina limetokana na wazungu. Walipokuwa wanakuja bara hili hawakukuta usafiri wowote. Na kutokana na ukarimu wa babu zetu waliwabeba wazungu hawa mabegani wakidhani ni watu laini wasioweza kutembea kwa miguu. Wazungu walipokuwa wanarudi kwao walikuwa wanahadithiana kuwa I visited a land of A Free Car, wakiwa na maana kuwa (kiswahili kisicho rasmi) ardhi yenye usafiri/gari huru ama lisilo na gharama. Sisi tukaona isiwe shida na tulitungue lilivyo. Tukaamua kuita AFRICA (A Free Car) mpo wadau wa historia...!!!!???
kibororoni- keep rolling
chekeleli- check rail
wonderful- ndafu
Wamarekani wawili walikuwa wanapita maeneo ya Manzese na mmoja awao akashangaa warembo wa kizaramo akasema '' Man....these?''........:baby::baby::baby: