Unajua maana ya jina Msasani?

hapa Mombo kuna sehemu inaitwa chekereni ukweli ni sehemu ambapo Reli inakatiza na wazungu walisisitiza Check Rail, wasamaba wakaunga chekereni
 
shekilango ni nkumbkumbu ya waziri aliyekufa kwa ajali ya ndege mlima kilimanjaro alikua akiishi mitaa hiyo
 

Duh asanteni nimewapata vzr asante sana mwanzisha huu Uzi..
 

Si kweli huu mtaa ulipewa jina kutokana kama kumbukumbu ya mbunge wa korogwe Mh
Hussein Ramadhani
Shekilango
aliyekuwa
waziri
wa nchi katika ofisi ya
waziri
mkuu. Alifariki kwa ajali ya ndege miaka ya 80 mwanzoni, huko arusha
 
[h=3]HUSSEIN RAMADHANI SHEKILANGO, SHUJAA ALIYEKUFA AKIIJENGA UGANDA[/h]
Jijini Dar es salaam kuna Barabara Mashuhuri kama 'Shekilango Road', ikianzia maungio ya Barabara ya Morogoro eneo la Nyumba za NHC mkabala na Kiwanda cha Urafiki, ikipitia Mitaa yote ya Sinza na kuishia Maungio ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kituo cha Bamaga.

Ni watanzania wachache wajuao kuwa Barabara hiyo ya Shekilango imepewa jina Maalum kwaajili ya heshima ya Ndugu Hussein Ramadhani Shekilango, aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, akishughulika zaidi na mambo ya Utawala, wakati wa Uongozi wa Rais Julius Nyerere na Makamo wake Aboud Jumbe Mwinyi.

Hussein Shekilango alichaguliwa na Wananchi wa kwao kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Jimbo la Korogwe Mjini, Mkoani Tanga katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1975, akiachia nafasi yake ya Zamani ya Meneja Mkuu wa Shirika la Usagishaji Nchini (NATIONAL MILLING CORPORATION).

Mwaka huo huo akachaguliwa na Rais Julius Nyerere kuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Utawala) akiwa chini ya Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu, ndugu Rashid Mfaume Kawawa.

Tarehe 11 Mei, 1980, ndege ya Kijeshi iliyowachukua Shekilango, Balozi Kilumanga pamoja na Wanajeshi wanne wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ilianguka katika vilima vya Jiji la Arusha na Abiria wote kupoteza Maisha, wakiacha huzuni na majonzi mazito kwa Watanzania.

Shekilango alizikwa Kijijini kwao Jitengeni, Korogwe, Mkoani Tanga, huku akisindikizwa na umati mkubwa wa watu, mpaka leo akibaki Mbunge kipenzi cha watu wa Korogwe na akisifika Serikalini kwa hatua yake ya kurudisha Madaraka Mikoani. Kwa kumuenzi kuna Shule yenye jina lake Jimboni Korogwe.

Mamlaka za Uongozi wa Jiji la Dar es salaam kwa kutambua mchango wa Shekilango kwa Taifa, ikaamua kuipa Barabara mpya iliyokuwa inajengwa wakati huo jina la Shekilango ili kumuenzi shujaa huyu.

Mola amlaze Pema Shujaa Hussein Ramadhani Shekilango

Na Luke Evelyne Singano

KOROGWE YETU: HUSSEIN RAMADHANI SHEKILANGO, SHUJAA ALIYEKUFA AKIIJENGA UGANDA
 
Mtoni kwa Aziz ally je hili jina limepatikana Vp?

Unajua Gongo La Mboto?

Palikuwa na mzee mmoja mashuhuri ambaye alipata kuishi katika eneo hilo... Huyu jamaa alikuwa mkulima. Jina lake aliitwa Mboto. Siku moja alijilawa kwenda katika konde lake kwa ajili ya kujipatia riziki. Wakati ule, maeneo yale yalikuwa na giza la mapori na vichaka kadhaa. Jioni yake asirudi nyumbani. kesho yake hadi mchana Mboto haonekani. Mbiu ikapigwa watu wakakusanyika... kilichofuata ni msako mkali wa kumtafuta mzee huyu... baada ya siku kadhaa wakakuta nyayo za mnyama mkubwa mithili ya Simba na ishara ya purukushani kadhaa. Walipochunguza zaidi wakafanikiwa kukuta Gongo ambalo alipenda kutembea nalo mzee huyu. Wakahisi kuwa Mboto huenda amekutwa na maafa ya kuliwa na Simba. Walichokiona pale ni Gongo lake.... Ndipo hilo eneo hadi leo lajulikana kama Gongo la Mboto.
 
AFRICAR..!!! Jina limetokana na wazungu. Walipokuwa wanakuja bara hili hawakukuta usafiri wowote. Na kutokana na ukarimu wa babu zetu waliwabeba wazungu hawa mabegani wakidhani ni watu laini wasioweza kutembea kwa miguu. Wazungu walipokuwa wanarudi kwao walikuwa wanahadithiana kuwa I visited a land of A Free Car, wakiwa na maana kuwa (kiswahili kisicho rasmi) ardhi yenye usafiri/gari huru ama lisilo na gharama. Sisi tukaona isiwe shida na tulitungue lilivyo. Tukaamua kuita AFRICA (A Free Car) mpo wadau wa historia...!!!!???
 
Mtoni kwa Aziz ally je hili jina limepatikana Vp?

Ni mahali alipokuwa anaishi mzee Aziz Ally tajiri wa wakati huo Tanganyika. Ni baba mzaz wa Dossa Aziz tunaemjua katika harakat za kudai Uhuru wa Tanganyika
 

Na Kilumanga je
 

Hongera ndugu nimefurai kujuzwa hilo
 
ILALA- asili ya jina hili ni maneno yaliyokuwa yakitumiwa na wailsamu muda wanapoenda kuzika pale (karume ) kwa wakati huo. laaailaa hailalhaa sasa wenyeji wakabatiza jina ila lhaa( isipokuwa MUNGU) wakaita ilala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…