Unajua madini yana tawaliwa na majoka. Ukweli huu hapa

Fbn

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
15,749
Reaction score
37,420
Picha hii ilipigwa mwaka 1959 na rubani wa helikopta kutoka Ubelgiji, Kanali Remy Van Lierde, wakati akiwa doria juu ya eneo la Congo. Nyoka aliyemuona alikuwa na urefu wa takriban futi 50 (sawa na mita 15), rangi yake ilikuwa kijani au kahawia iliyokolea na tumbo jeupe. Alikuwa na taya lenye umbo la pembetatu na kichwa kilichokadiriwa kuwa na ukubwa wa futi 3 kwa 2.





Picha hiyo ilichunguzwa baadaye na kuthibitishwa kuwa ya kweli. Van Lierde anadai kuwa aliposhuka chini kwa ajili ya kuuangalia kwa karibu, nyoka huyo alijinyanyua hadi urefu wa takriban futi 10 (sawa na mita 3), kana kwamba akitoa onyo kuwa angeishambulia helikopta hiyo kama ingekuwa ndani ya umbali wa kuweza kufikiwa na shambulizi lake.
 
Mh! hii napinga kwa kuandika no reform no nyoka!.
 
Sijaona sehemu yoyote uliyomhusisha nyoka na madini
 
Kwahiyo madini yako wapi hapo?
Au kayameza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…