MView attachment 3633730View attachment 3633731View attachment 3633732eno ya utotoni – yana umuhimu mkubwa kuliko unavyofikiri.
Wazazi wengi hudhani kuwa meno ya utotoni hayana umuhimu kwa sababu baadaye yatang'oka na kuota meno ya ukubwani. Kutokana na imani hiyo, wengine husubiri meno yakioza kabisa ndipo wampeleke mtoto kwa daktari wa kinywa na meno ili yatolewe.
Ukweli ni kwamba, meno ya utotoni yana muda maalum wa kung'oka na kuota meno ya ukubwani, na muda huo hutofautiana kulingana na aina ya jino (meno ya mbele, machonge au magego). Kuyatoa kabla ya muda wake kunaweza kusababisha madhara mbalimbali, ikiwemo:
1. Kusababisha mpangilio usio sahihi wa meno ya ukubwani.
2. Kuathiri ukuaji wa taya.
3. Kumfanya mtoto ashindwe kutafuna chakula vizuri.
4. Kusababisha maumivu, maambukizi na majipu ya meno.
5. Kuathiri umakini na maendeleo ya mtoto shuleni.
6. Kumuathiri mtoto kisaikolojia na kujiamini.
Mtoto akianza kuoza meno, usikimbilie kuyatoa. Mpeleke kwa daktari wa kinywa na meno mapema ili yafanyiwe matibabu stahiki, kama vile kuzibwa, na yahifadhiwe hadi yatapofikisha umri wa kutoka mdomoni
Tunatoa huduma za Afya Kinywa na meno ikiwepo
-Kuziba meno
-Huduma ya Meno bandia ya aina zote
- Kusafisha meno
- Kung’arisha meno
- Kupanga meno yaliyo kaa katika mpangilio usio sahihi
- matibabu ya mzizi wa jino ( RCT )
-matibabu ya Kuondoa maumivu& Ganzi kwenye meno
- Kufunga Taya lililoteguka / Kuvunjika
- Kuondoa jino lililo haribika sana
Tunapatikana
📍Temeke - Dar es salaam, Kibaha - Pwani
📞0658 950 085
Karibu Tukuhudumie 🦷✅
Asante kwa ushauri mzuri sanaMView attachment 3633730View attachment 3633731View attachment 3633732eno ya utotoni – yana umuhimu mkubwa kuliko unavyofikiri.
Wazazi wengi hudhani kuwa meno ya utotoni hayana umuhimu kwa sababu baadaye yatang'oka na kuota meno ya ukubwani. Kutokana na imani hiyo, wengine husubiri meno yakioza kabisa ndipo wampeleke mtoto kwa daktari wa kinywa na meno ili yatolewe.
Ukweli ni kwamba, meno ya utotoni yana muda maalum wa kung'oka na kuota meno ya ukubwani, na muda huo hutofautiana kulingana na aina ya jino (meno ya mbele, machonge au magego). Kuyatoa kabla ya muda wake kunaweza kusababisha madhara mbalimbali, ikiwemo:
1. Kusababisha mpangilio usio sahihi wa meno ya ukubwani.
2. Kuathiri ukuaji wa taya.
3. Kumfanya mtoto ashindwe kutafuna chakula vizuri.
4. Kusababisha maumivu, maambukizi na majipu ya meno.
5. Kuathiri umakini na maendeleo ya mtoto shuleni.
6. Kumuathiri mtoto kisaikolojia na kujiamini.
Mtoto akianza kuoza meno, usikimbilie kuyatoa. Mpeleke kwa daktari wa kinywa na meno mapema ili yafanyiwe matibabu stahiki, kama vile kuzibwa, na yahifadhiwe hadi yatapofikisha umri wa kutoka mdomoni
Tunatoa huduma za Afya Kinywa na meno ikiwepo
-Kuziba meno
-Huduma ya Meno bandia ya aina zote
- Kusafisha meno
- Kung’arisha meno
- Kupanga meno yaliyo kaa katika mpangilio usio sahihi
- matibabu ya mzizi wa jino ( RCT )
-matibabu ya Kuondoa maumivu& Ganzi kwenye meno
- Kufunga Taya lililoteguka / Kuvunjika
- Kuondoa jino lililo haribika sana
Tunapatikana
📍Temeke - Dar es salaam, Kibaha - Pwani
📞0658 950 085
Karibu Tukuhudumie 🦷✅
Toa elimu kwanza maana hata kula nyama siwezi juzi kati nilienda ukweni nyama zote zilinishinda ni kwamba haliumi ila ni kama lina hali ya uchachuFika Clinic kwetu tuweze kukuchunguza kwa kina tujue tatizo haswa ni lipi linapelekea hiyo Ganzi , Pia unaweza nitafuta PM Au whatsApp 0658950085 niweze kukudadisi kwa kina 🙏
Haya Ngoja Tujadili Kidogo ,Toa elimu kwanza maana hata kula nyama siwezi juzi kati nilienda ukweni nyama zote zilinishinda ni kwamba haliumi ila ni kama lina hali ya uchachu
Haya Ngoja Tujadili Kidogo ,
Sababu za meno kuwa Ganzi ( hypersensitivity ) 👇
• Kusafisha meno kwa kutumia nguvu kubwa hii husababisha kuondoka kwa gamba gumu la nje la meno , ikiwa ni pamoja na aina ya mswaki ukiwa na brush ngumu sana hupelekea kuondoa tabaka la juu la jino hivyo jino kuwa exposed unashuauriwa kutumia mswaki laini na usio na usitumie nguvu kusafisha meno yako ( njia ya kiduara inafaa zaidi / rotatory )
•Kusagika kwa fizi ( Gum recession ) hii ni tissue ambazo zimelizunguka jino hivyo ikiwa imelika kutokana na magonjwa ya fizi au kwa upigaji usio sahihi wa mswaki hupelekea kwa kiini cha jino kuwa nje hivyo ukigusa kitu cha moto / baridi lazima usikie maumivu
•Matumizi ya vyakula vyenye Tindikali hapa tunazungumzia soda , citrus, wine huwa vinasababisha tabaka la nje la meno ( Enamel ) kuyeyuka pia na kufanya tabaka la kati la jino ( dentin) kuwa haliko protective ukikutana na vitu vya baridi lazima meno yapate ganzi
•Kusaga au kutafuna meno nyakati za usiku ( Bruxism ) hupelekea kusagika kwa sehemu ya juu ya jino ( enamel) hivyo Dentin au pulp kuwa nje iwapo utatumia vyakula vya baridi lazima upitie changamoto
•Kutoboka kwa meno / kuoza .. iwapo jino limetoboka , au kuoza na kufika kwenye tabaka la pili la jino Dentin / pulp hupelekea maumivu na na ganzi kwenye meno ushauri fanya uchunguzi wa kinywa na meno angalau mara mbili kwa mwaka
• Baadhi ya huduma za kinywa na meno ulizopata hivi karibuni ikiwepo kungarisha meno. Iwapo zilihusisha kukwangua kwa jino hupelekea ganzi na maumivu kwenye meno
Je hiyo hali umeanza kuipata mda gani !? , Unapata maumivu wakati wa kula !? Ukipiga mswaki kuna chembe chembe za damu kwenye Fizi ?
Ni wakati gani sahihi wa kuwekA meno baada ya kung'oa meno??Meno yote mazuri kulingana na Uwezo wako , Lakini ya Kudumu zaidi ndyo suluhisho la Kudumu karibub