Unajua sababu zinazomvutia kachero mbobevu Benard Camilius Membe kwa Rais Samia Suluhu Hassan?

Unajua sababu zinazomvutia kachero mbobevu Benard Camilius Membe kwa Rais Samia Suluhu Hassan?

Jesusie

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2021
Posts
1,466
Reaction score
766
|Haya ndio mambo sita makubwa yanayomvutia zaidi Kachero Benard Membe kwa Utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan,

Kwanza, Mabadiliko
, ni raha ya Watanzania kupokea mabadiliko ya uongozi wa nchi.

Pili ,Uhuru & Usalama, anasema kuingia kwa Rais Samia ambaye ni mwanamke, hewa ya uhuru na usalama nayo ikaingia nchini na kwa sasa hakuna lugha ya watu wasiojulikana kwa kuwa msamiati huo unaanza kufa.

Tatu, Watuwasiojulika, Sasa hivi husikii watu kukamatwa au kuona maiti zinaelea baharini au mtu kafa, husikii upotevu wa binadamu wenzako, wafanyabiashara au watu wa kawaida, kwa Watanzania hii lazima tuithamini,” anasema Membe na kuongeza:
“Nilihuhuria mazungumzo ya Bill Clinton na Jakaya baada ya kustaafu, Jakaya alimuuliza Clinton swali uchaguzi unaendeleaje Marekani kwa sababu Hillary Clinton alikuwa anagombea wakati huo.

“Akajibu uchaguzi unaendelea. Je, kuna matumaini mama anaweza kushinda? Akasema hapana hakuna matumaini hayo kwa sababu wahafidhina wanafanya kosa kubwa kwa kudhani wakimchagua Hillary kuwa Rais wa Marekani atakua ananiiga mimi (Clinton).

“Akasema hakuna marais wanaofanana, asikudanganye mtu, hakuna, wao wana miaka zaidi ya 250 ya uhuru wao na marais wanajuana wote na hakuna rais atayefanana kwa maneno na vitendo na rais mwenzake, kwa sababu kila rais atakutana na changamoto zake ambazo akiangalia nyuma hazijawahi kutokea sasa unaiga nini?“Clinton akasema hata ukimlazimisha Hillary amuige hawezi kwa sababu kila mtu anatawala katika mazingira ambayo ni tofauti na ya jana, akasema kwa hiyo wahafidhina wa Marekani wanafanya kosa tukimchukua huyu atafanya hivi.

“Haiwezekani kwa sababu wewe Kikwete ulikuwa na changamoto zako tofauti na Mkapa, na Mkapa alikutana nazo tofauti na Mwinyi, kwa hiyo wewe haiwezekani changamoto zako zikafanana na Mkapa. Huwezi kusema mimi niliendeleza shughuli za Mkapa, hapana, huwezi kusema hivyo.”

Katika hatua nyingine, anasema pia si sahihi kusema kwamba Rais Samia afanane na Magufuli kwa sababu yeye ana changamoto zake ambazo ni lazima ziende kwa uwiano wa kipekee na mazingira yake anayokutana nayo.

Anasema kwa sasa anachokifanya Samia ni kizuri kwa sababu anaangalia swichi kubwa ya umeme na vitufe vyote vilikuwa vimezimwa, kwa mfano swichi ya mambo ya nje ilikuwa imezimwa na sasa ameiwasha.

Nne, Bunge Live , Swichi ya Bunge live ilikuwa imezimwa nayo akaiwasha, ile ya ya gesi ya Lindi ilizimwa na yeye kaiwasha na sasa kuna mazungumzo na ndiyo utaalamu mzuri.

“Na unaona kabisa huyu mama anajua madhara ya swichi kuzimwa na kuwasha na lazima tumpe heshima yake na huyu ni mama, duniani kuna wanawake sita tu viongozi wa nchi na mmojawapo ni Rais Samia wanaongoza na hiyo ni bahati.

Tano, Utu wa Mtu,Unapopata bahati hii lazima tuiheshimu, tukianza hapa huyu mama hatufai ataondoka. Katika siasa ili ukubalike nchini na duniani kuna mambo lazima yafanyike, haki ya msingi za binadamu kwanza uthamini kwamba umwagaji wa damu ya Mtanzania mmoja itakugharimu, kwamba ni lazima ukiwa kiongozi uhuru wa vyombo mbalimbali, kuwe na uhuru wa wananchi wako kwenda kokote wanapotaka.

Sita, Demokrasia na Utawala wa Sheria ,demkorasia na utawala bora, lazima tuwe na uongozi wa sheria na pia tuwe na demokrasia na unapokuwa hivyo unakuwa na taasisi za kidemokrasia mfano vyama vya upinzani viheshimu kwa hivyo huo ndiyo msingi wa uongozi, kwa hiyo ni lazima utengeneze muundo au mfumo wa kwako unaoutaka wewe, lakini si lazima ufanye hivyo siku hiyo hiyo.”

Membe anasema ukiwa kiongozi lazima ujiulize kwanini fulani alikuwa anapenda mfumo huu au ule na utajifunza na kuna kitu kinaitwa mpito na anaamini kwa sasa bado tuko katika kipindi kifupi cha mpito.

“Sasa mtu mwingine atakwambia kipindi cha mpito cha miezi sita ni kikubwa sana, hapana kumbuka hii ni siasa, kuna mashimo katika njia hiyo hiyo na miba, kwa hiyo lazima uje taratibu kumpa nguvu mama na kumpa muda ili aweze kufanya marekebisho,” anasema na kuongeza:

“Huyu ni mama, mama yeyote yule hata mama yako mzazi ni mtu ambaye hakawii kukata tamaa, nyinyi watoto wote mkienda kinyume naye ataumwa kichwa tofauti na baba yenu ambaye atawachapa. Mama Samia lazima tumpe heshima yake.”
Membe anasema atamuunga mkono Rais Samia mwaka 2025 na hiyo inaeleza tafsiri yake kwamba hapa katikati asiwe na wasiwasi wowote ule.

Anasema ataenda mbali zaidi na Rais Samia kwa sababu kuna nguvu zinapenda aondoke na sasa wanachotakiwa kufanya ni kumpa moyo na kumpa nguvu kwamba wanamuunga na watamuunga mkono.

“Kwamba suala la kumuunga mkono kwake lisiwe tatizo na hivi ndivyo inavyokuwa tutamuunga mkono"

Soure : Dennis Luambano -Jamhuri

photo_2021-11-05_10-00-35.jpg
 
Amesahau kuwa raisi wetu anapenda nchi iwe na haiba ya usafi lakini kuna watu hapo pembeni yake wanamhujumu kwenye swala la kuhamisha machinga. Kwa kuwa wananchi tuko naye kwenye hili basi awadhibiti hao wanaotaka kumhujumu kwa lengo la kujiimarisha kisiasa
 
Amesahau kuwa raisi wetu anapenda nchi iwe na haiba ya usafi lakini kuna watu hapo pembeni yake wanamhujumu kwenye swala la kuhamisha machinga. Kwa kuwa wananchi tuko naye kwenye hili basi awadhibiti hao wanaotaka kumhujumu kwa lengo la kujiimarisha kisiasa
😍😍 Umeongea vitu vizuri Sana
 
Back
Top Bottom