NJIA 7 UNAZOWEZA KUZITUMIA ILI KUEPUKA DHAMBI YA UZINZI.
Imeandikwa...
" Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.."
( 1 Wakorintho 6:18-20)
〰️ Lakini Maandiko hayakuishia hapo yakasema pia..
"Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalo mwangamiza nafsi yake"
( Methali 6:32 )
〰️ Kusudi la mwili wako sii kwa Ajili ya Ngono au kufanya mapenzi, katika hili Maandiko yalitukumbusha kwa kusema .....
" Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, .... Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe"
( Wimbo ulio bora 2:7 )
""Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na MUNGU? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni MUNGU katika miili yenu"
( 1 Wakorintho 6: 19-20)
**** ZIFUATAZO NI NJIA 7 AMBAZO UNAWEZA KUZITUMIA KATIKA KUEPUKA DHAMBI YA NGONO AU KUFANYA MAPENZI KABLA YA NDOA. (Dhambi ya uzinzi)
️⃣ Shinda vita yako akilini kwa kusoma Neno la MUNGU
〰️ Dhambi ya ngono huanzia akilini kwa kuifikiria, Ili uishinde vita yako akilini. Jifunze kuijaza akili yako kwa Neno la MUNGU.Kama kijana Ikiwa akili yako utaijaza kwa neno la MUNGU, Fikra zako wakati wote zitadumu katika kuimarisha uhusiano wako na MUNGU kwa muongozo wa Roho Mtakatifu na wala si kwakufikiria dhambi ya ngono.
Imeaandikwa....
" Nimewaandikia ninyi vijana, kwa Sababu mna nguvu, na neno la MUNGU linakaa ndani yenu nanyi mmemshinda yule muovu.
( 1 Yohane 2:14 )
2️⃣ Uchaguzi wa marafiki wazuri.
Imeandikwa....
" Enenda Pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima, bali rafiki wa wapumbavu ataumia."
( Methali 13:20 )
Kuna usemi unasema nieleze rafiki zako nami nitakwambia tabia yako, usemi huu una maana ya kuwa idadi ya marafiki uliona huwakilisha tabia yako. Ikiwa una marafikia 4 wadangaji, malaya au makahaba nawewe utakuwa mdangaji, Malaya au kahaba wa 5.
Marafiki wana ushawishi mkubwa wa tabia yako, Ikiwa wewe ni Mkristo jifunze kuchagua marafiki watakao kuwa na mchango mkubwa katika mambo ya kiroho au safari yako ya kiimani.
Jifunze kuchagua marafiki ambao fikra zao Wala mawazo yao hayapo katika kuongelea wala kuwaza ngono zembe.
Ikiwa utaishi na marafiki wenye nia na malengo sawa na wewe itakuwa vyepesi kwako kuzishinda tamaa za mwili wako katika dhambi ya kufanya mapenzi kabla ya Ndoa.
3️⃣ Jifunze Kuwa Busy Na Mambo Muhimu.
Kuna usemi mmoja unasema.....
" An idle mind is the devil's workshop".
(Akili isiyo na Kazi ni karakana ya Shetani)
Ikiwa utaishi maisha yako bila ratiba, Ikiwa utaishi maisha yako bila malengo, Ikiwa utaishi maisha yako bila kuwa na kitu Cha kufanya au kazi ya kufanya. Basi, Shetani atakutumia ili utimize kusudi na malengo yake.
Imeandikwa..
"Mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya BWANA"
( Waefeso 5: 16-17)
Kama kijana Ikiwa utakuwa busy kwa kufanya kazi na kwa kufikiria mambo muhimu ya maisha yako, hizo fikra za kuwaza ngono au kufanya mapenzi kabla ya Ndoa huwezi kuzipita. kwa Sababu, akili yako na mwili wako utakuwa umeshachoka tayari, na hautokuwa tayari kufanya Chochote zaidi ya kupumzika au kupata utulivu.
4️⃣ Usijiruhusu kuwa katika maeneo yenye vishawishi au katika maeneo ambayo mawazo ya kufanya ngono yanaongelewa zaidi.
Imeandikwa....
"Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema. Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui MUNGU"
( 1 wakorintho 15: 33-34)
5️⃣ Jiepushe na vitabu, magazeti, picha, au Tovuti na magroup katika mitandao ya kijamii yanayochochea kufanya ngono.
Imeandikwa..
" Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia,......Maana kila kilichomo duniani, yaani tamaa ya mwili, na tamaa ya macho na kiburi cha uzima, havitokani na BABA, bali vyatokana na dunia."
( 1 Yohane 2: 15-16)
6️⃣ Jenga uhusiano wa uwajibikaji na wazazi wako, wazazi wako wakiroho, Watumishi wa MUNGU waaminifu, na marafiki wenye nguvu za Ukristo ndani yao. Unapopitia wakati wa jaribu, wajulishe na uwaombe msaada wa mawazo, ushauri na maombi.
7️⃣ Mtume Paul alishauri kuwa.." Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe...'
( 1 Wakorintho 7 )
Ikiwa umri wako wa kuoa au kuolewa umefika basi Tafuta mtu huku ukimtanguliza MUNGU kwa maombi akuongozee, ili umpate wa kufanana na wewe Kama alivyo ahidi. Ili uepukane na dhambi ya NGONO au kufanya mapenzi kabla ya Ndoa...
MWISHO....
" KAMA VIJANA, MUNGU NA ATUSAIDIE ILI TUISHINDE DHAMBI HII. KUNA NGUVU KUBWA YA USHINDI AMBAYO MUNGU KAIWEKA NDANI YAKO, IKIWA UTAAMINI NA KUIISHI HAKUNA LISILOWEZEKANA KATIKA YEYE ATUTIAYE NGUVU"
Ubarikiwe sana kwa masomo mengine karibu
👇👇
View: https://youtu.be/Im-XnldBVTI
👆👆