Unakaaje hapa duniani zaidi ya miaka 80 huna hata nyumba ya kwaachai watoto,serikali iingilie kati

Pain killer

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2017
Posts
14,365
Reaction score
21,747
Habari wakuu

Mimi binafsi linanikela sana hili swala ,mwanaume unazaa watoto zaidi ya watano ,nyumba huna,biashara huna,kazi huna ,kilimo cha mkono huku ukijipa moyo huenda mtoto atakuwa jakaya,au Mandela ,au Obama,ujinga mtupu

Kuwalisha tuu ni shida achana na mavazi ,huduma za mhimu tu ni tabu ,shulen kuwapeleka ni mpaka serikal iingilie kati.

Aisee kama huna uwezo wa kulea ,ni bora tu ukaishi kisela hapa duniani ,sio lazima kuzaa ,ishi kivyako kufa kivyako kuliko kuzalisha watoto ili uwatese na kuiona dunia chungu

Kama wewe ulipata tabu hapa dunian hakuna ulazima wa kuleta viumbe hapa dunian kuwatesa

Mh raisi angalia hili swala ,kama MTU hayupo vizur kiuchumu ni marufuku kuoa ,hana sifa za kuwa na familia,akileta za kuleta weka ndani ni ujinga Mtupu kuendelea kuzalisha watoto ambao wanajuta kuzaliwa hapa dunian .

Uzi tayari
 
Mkuu watu wanapitia mapito sana na siyo kwamba wote wanapenda hayo maisha.

Tunaomba kwa aliyewahi au anayepitia maisha kama hayo awe muwazi kueleza ili tujifunze kupitia yeye/wao.

Moyo wa mtu msitu ila kupitia yako , wengine tutajifunza.
 
Hoja nzuri. Ila kuzaa kwani ni lazima uwe umeoa ukipiga marufuku kuoa watu wataendelea kuzaa tu kama siku zote. Watu wengi waliojenga wamezaliwa ktk nyumba za kupanga au duni ndiyo wamepata uchungu wa kujenga. Waliozaliwa baba zao wana majumba wamebweteka hawajajenga wanazaa hadi kujukuu humo humo nyumba za urithi
 
Jamani mtu maisha ya mpige hata starehe inayopelekea kupata mtoto mnataka mumpangie? Daah kweli mwenye nacho huongezewa aisee
 
Mkuu naunga mkono hoja kwa nguvu zote ,ni upumbavu wa kiwango cha bombardier mtu anazaa watt kibao wakat anahali mbaya kiuchumi
Mtu mpaka anazeeka anawatoto 7 wamepanga

Watoto wanakuja kuwa vibaka kisa kukosa mwelekeo
 
Jamani mtu maisha ya mpige hata starehe inayopelekea kupata mtoto mnataka mumpangie? Daah kweli mwenye nacho huongezewa aisee
Kama yanampiga yeye ,asilete watoto wengine nyuma yake wapate tabu
 
Mkuu watu wanapitia mapito sana na siyo kwamba wote wanapenda hayo maisha.

Tunaomba kwa aliyewahi au anayepitia maisha kama hayo awe muwazi kueleza ili tujifunze kupitia yeye/wao.

Moyo wa mtu msitu ila kupitia yako , wengine tutajifunza.
Mapito unayopita ndio yanakupa tafakari kuwa hapa naweza kuongeza MTU wa kumhudumia (mke na mtoto)?

Kama Milo mitatu kwa siku ni tabu ,unapata wapi ujasir wa kuzaa watoto ,watakula mawe?
 
Hayo ni mambo ya mijini huko, vijijini (zaidi ya 70% tunaishi huku) hakuna mtu hana nyumba... wala hakuna kitu sijui mnaita kupangisha!

Na watoto tunazaa wa kutosha, hata wewe unayelialia ulizaliwa huko kijijini kisha ukakimbilia mjini... endelea kuisoma namba tu.
 
Ukweli mchungu, halafu watu wa dizaini hiyo ni wabishi hakuna mfano...
 
Chukulia huyo mzee ana miaka themini alioa na kuzaa akiwa na miaka 30 kwa hiyo sasa akiwa na miaka 80 mwanawe atakuwa na miaka 50 .Kwa hiyo huyo mzee amwachie mali mwanae wa miaka 50? hilo si ni jitu zima hilo ? mleta mada akili huna
 
Sas KAZI ya mweheshimiwa Rais zitakuwa zimemzid uwez hata hii jamn
 
Mtu mpaka anazeeka anawatoto 7 wamepanga

Watoto wanakuja kuwa vibaka kisa kukosa mwelekeo
kwani kupanga ndiko kunafanya mtu akose mwelekeo? Wahindi mbona wanazeekea na kujukuu wakiwa nyumba za kupanga za NHC mbona watoto wao sio vibaka na hawajakosa mwelekeo?
 
siungi mkono hoja kwani unaweza ukawa na uwezo kulea familia lkn bahati mbaya ukafilisika ama ukatangulia mbele za haki kabla watoto hawajapata haki zao za msingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…