Unakula mpaka Sadaka aisee? Bodi ya Wasabato Tanzania Yavunjwa kwa Ubadhirifu wa Mali za Kanisa

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
62,101
Reaction score
38,487
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imeivunja rasmi Bodi ya Wadhamini ya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania kufuatia kubainika kwa mapungufu makubwa katika usimamizi wa mali na utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya ripoti ya ukaguzi maalum ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kubaini kuwa bodi hiyo ilishindwa kusimamia ipasavyo mali na rasilimali za kanisa, pamoja na kutotekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.

Akizungumza Februari 24, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa kupokea ripoti ya ukaguzi huo wa kiuchunguzi, Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Frank Kanyusi amesema kuwa kuvunjwa kwa bodi hiyo ni hatua ya kisheria inayolenga kulinda mali za taasisi na kurejesha nidhamu ya uongozi ndani ya kanisa hilo.

Amesema, pamoja na kuvunjwa kwa bodi, uongozi wa kanisa umepewa siku saba kuwasilisha majina kumi (10) ya waumini watakaopendekezwa kuwa wajumbe wa kamati ya mpito.
Amesema kuwa Kamati hiyo itasimamia mali na shughuli za kanisa hadi pale Bodi mpya ya Wadhamini itakapoundwa kwa mujibu wa sheria.

Kanyusi alieleza kuwa ukaguzi huo maalum ulifanyika kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na baadhi ya waumini wa kanisa hilo katika Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu na kwa Msajili wa Jumuiya za Kiraia chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakilalamikia tuhuma za ubadhirifu wa mali za kanisa na matumizi mabaya ya madaraka.

Alibainisha kuwa hatua ya kufanya ukaguzi maalum ilitokana na mashauriano kati ya ofisi yake na Msajili wa Jumuiya za Kiraia katika Wizara ya Mambo ya Ndani, Emmanuel Kihampa, ili kujiridhisha na ukweli wa malalamiko hayo.

“Taarifa hii ya CAG ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha ukweli unajulikana na hatua stahiki zinachukuliwa. Tutaiwasilisha kwa vyombo vingine vya uchunguzi ili wote watakaobainika kuhusika na ubadhirifu au matumizi mabaya ya madaraka wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria,” alisema Kanyusi.

1772012799062.jpg
 
Nilijuaa kondooo tu kumbe hadi saadaka mpwa wanapita nazooo bodies nyokooo
 
Halafu wasabato ukiwaambia tukale kitimoto wanaruka kimanga na kukupa vifungu vya Kumbukumbu la Torati eti Mussa alikataza.

Lakini hela za kujengea nyumba ya Mungu wanazitafuna kama mchwa. Ipi mbaya kati ya kula nguruwe na kula hela za waumini za kujengea kanisa?
 
na ipi mbaya na kuwala kondoo wenyewe 😛 😛 😛
 
Ripoti ya CAG haijatoa ufafanuzi kwa asilimia mia moja ni ubadhirifu gani umefanyika ndani ya kanisa, the report is too shallow to discuss japo ni kweli kwamba kuna irregularities nyingi ndani ya kanisa, kama ilivyo kwenye taasisi nyingine za kidini.
 
Halafu wasabato ukiwaambia tukale kitimoto wanaruka kimanga na kukupa vifungu vya Kumbukumbu la Torati eti Mussa alikataza.

Lakini hela za kujengea nyumba ya Mungu wanazitafuna kama mchwa. Ipi mbaya kati ya kula nguruwe na kula hela za waumini za kujengea kanisa?
Tena Waumini Oheahe Kishenzi Mnoo....
 
Kwahiyo ndugu mtoa mada wewe ulikuwa unadhania kwamba sadaka ni kwaajili ya Nini !? 😁😁😁

Hiyo ni mifumo imewekwa kwaajili ya wajanja wachache kuwapiga wasio nauelewa wa jinsi mambo yanayo kwenda Duniani ,

So hizo sadaka zilikuwa zinatumika Kwa maamuzi sahihi kabisa ,

Wamewaonea itakuwa wana ugomvi nao , Mbona serikali Huwa inakutwa na hatia na CAG lakini Huwa haiwajibishwi!!!!!
 
Dini ya kweli ni kuwasaidia wajane ,yatima ,wagonjwa ,masikini na wasiojiweza.

Fuata amri 10 za Mungu.

Mungu anasisitiza Upendo.

Kwasasa Dini ni Biashara.
 
Tunaomba special audit iendelee kwa manabii na mitume ili kazi zilizojificha ziwekwe waaz
 
Back
Top Bottom