ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Mtu utasikia anadai anaenda sehemu kula bata ila akifika anakunywa soda chips labda na kipande cha kuku. Kwani kula kwa tunavyohisi ni kitendo cha starehe yaani yawe mambo yenye utofauti kidogo na unayofanya kila siku.
Wewe kwa upande wako ukisema unaenda kula bata unamaanisha mambo gani haswa.
Kuna mdau katoa mchango wake yeye anasema
kula bata kwangu mimi.
Ni kupata muda wa kufurahi pamoja mimi na familia yangu tukipata neema ya kupata nafasi muda na pesa ya kufanya
1)kubadilisha chakula mfano kutokana na umasikini tulionao sio mara nyingi tunakula vyakula tunavyovipenda ila tunakula vinavyopatikana kadiri ya uwezo wetu kama dagaa,maharage,mboga za majani,ugali
Hatuna financial freedom ya kula tunachokitaka na kwenda outing kila weekend ku enjoy
Na mimi binafsi nikitumia laki moja pembeni nikaila kipembeni peke yangu bila kushare na familia yangu naona nafsi inanisuta kwa u selfish
mfano naagiza kitimoto kilo moja na ndizi nne na soda nikaila pembeni peke yangu nahisi kama nimetenda dhambi wakati najua watoto na familia wanakula dagaa nyumbani.
Sasa watoto nikiwanunulia mbuzi choma,kiti moto,pilau chips,vyakula vizuri ambavyo familia watoto wanavipenda ambavyo hawavipati mara kwa mara huwa wana enjoy kama familia wote tunafurahi sana,wakinywa na juice au soda
2)Au nikipata neema ya kuwatoa out kwenda sehemu za michezo ya watoto,kuogelea kubembea,kula chakula,wakapiga picha ,nikiwanunulia na nguo huwa wanafurahi..
3)Kama sasa hivi wanafunga shule nikipata neema ya wao wakasafiri kusafiri nao hasa nikiwa likizo kwenda mbuga za wanyama,ama mikoani kisalimia wakatembelea mazingira mapya ,wakajifunza kitu kipya
4)nikiwanunulia zawadi au nikijinunulia zawadi au nikinunua .
LAKINI HII YA
Kunywa pombe(situmii kilevi chochote),uzinzi na uasherati sifanyi naheshimu ndoa yangu na nimeamua kukataa na kuacha dhambi ya uzinzi/uasherati ni uchafu na ina madhara kiroho kadiri ya imani yangu dhambi ni mauti,dhambi inakutenga na Mungu.
Miziki ya kidunia ni ibada ya kishetani ile miziki ni ibada kamili zinazolaani maisha ya wasikilizaji ni dhambi,hata filamu movie,series,baadhi ya cartoon na sports michezo ni ya kipagani.
BADALA YA BURUDANI AU ANASA ZA KIDUNIA
Naburudika kwa nyimbo za kwaya za kumsifu na kumshukuru Mungu,badala ya miziki ya kidunia inayosifia violence ,sex ,illegeal issues ,pride kujisifu majigambo
Badala ya pombe nakunywa maziwa ,juice ,maji,
Badala ya kwenda baa ,disco club naenda kwenye ibada nacheza na kuomba nyimbo za kumsifu na kumshukuru Mungu
Na napata muda mwingi wa kulala usiku badala ya kukesha kwwnye ulevi na anasa,na kujisomea,na kuwahi kuamka kwenda ibadani kusali na kusali jumuiya
Natoa sadaka kwa Mungu wangu kanisani kwangu,Pesa ambayo ningeitumia kuhonga ama kulewa au anasa za kidunia na kusaidia matumizi ya familia.
Nawahi kurudi nyumbani tunapata muda wa kula chakula cha usiku pamoja na familia na kusali pamoja kama familia kabla ya kulala ,kifuatilia home work za watoto na kuongea na familia.
HITIMISHO
Siwahukumu walioamua kuishi maisha ya ULEVI(unywaji wa pombe),NGONO/UZINZI,KUBETI,USHABIKI WA MIPIRA hata wasiosali ,na hata wasio amini uwepo wa Mungu.
Kila mtu ana haki na uhuru wa kuishi kwa kuamini na kufanya kile anatochokitaka kama havunji katiba,sheria za nchi ,na havunji na haki na uhuru wa watu wengine.Hata mimi kabla ya kupata neema ya kuokoka nilikuwa mlevi na mzinzi ,lakini vyote hivyo havikunisaidia kitu hasara ni nyingi kuliko faida,na nilikuwa najifariji kuwa nakula bata au naenjoy kuishi maisha ya dhambi.