Unakumbuka kazi za hawa wakulungwa wa Uganda

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
UGANDA CENTRAL ( +256)
Hili lilikuwa jina la kipindi cha ngoma za Uganda pale East Africa Radio miaka hiyo (sijajua kama bado kipo maana sisikilizi tena redio).
Umewahi kusikiliza muziki wa Uganda?
Ulivutiwa na kazi za nani?
Wimbo gani unaukumbuka mpaka leo?
Binafsi nawakumbuka wafuatao na kazi zao.

1. BLU3 (JACKIE CHANDIRU, CINDERELLA SANYU AND LILIAN MBABAZI)
Tanzania ilikuwa na WAKILISHA, Kenya ilikuwa na TATUU halafu Uganda ikawa na BLU3.
Kwa pamoja walitoa ngoma kali kama;
HITAJI
HITAJI RMX FT MOSHI
BURN
BURN RMX FT NAVIO
Na ngoma nyingine walizoziimba kwa Kiganda.
Cindy alikuwa wa kwanza kujitoa. Lilian akabaki na Lilian na kumwongeza binti mwingine ili jina lisipoteze maana.
Cindy akasimama na mikwaju kama
TOTAL SATISFACTION
ME AND YOU FT P SQUARE
NATAMANI WEWE
OUT OF MY MIND
BLU3 MPYA ikarudi na ngoma kama;
PRISONER FT NAMELESS
STRONG WOMAN
TOGETHER
na wimbo wa taifa ulioitwa WHERE YOU ARE FT RADIO AND WEASLE.
Jacky ndiye niliyekuwa nikimwelewa zaidi na alitoa kazi binafsi kali kama;
AGASSI, OVERDOSE na GOLD DIGGER

2. WEASLE AND RADIO
Radio alikuwa na sauti ya pekee sana na alifariki angali bado anahitajika kwenye game. KIFO CHAKE KINANIUMIZA MPAKA LEO.
Wawili hawa waliwasha moto na ngoma kama;
EVERYTHING I DO, POTENTIAL, UNANIUMIZA, CAN'T LET YOU GO, NAKUDATA FT OMULANGILA SUUNA ( OS), MAGNETIC, ABILITY, NIPE KIFUNGUO FT WIZKID, DON'T CRY FT WIZKID, NYUMBANI FT VBOYO na magoma mengine mengi Kama ZUWENA.

3. JOSE CHAMELEONE
Jamaa alipamba utoto/ ujana wetu kwa ngoma zake za Kiswahili alizozichanganya na vionjo vya nyimbo za watoto. Kuna ambao walidhani alikuwa Mtanzania mwenzetu.

Daktari huyu wa muziki alisumbua Sana na ngoma kama;
BEI KALI, DOROTIA, MAMA MIA, MAMBO BADO, NAUMIA, SAUTI YA DHAHABU, BAHATI YANGU, NAOMBA UNIAMINI, TOBESIGA, SHIDA ZA DUNIA, MAMA RODA FT BUSHOKE, BOMBOCLAT, TUBONGE, VALUVALU

Chameleone ndiye msanii kutoka UG anayeongoza kwa kufanya Kolabo na Wabongo kama ifuatavyo;

1. Ndivyo sivyo - Prof Jay
2. Kiboko yao - Lady Jay Dee
3. Bounce - Mwana FA
4. Nasema nao - AY
5. Kwa ajili yako - Prof Jay
6. Dance flow - Pig Black
7. Kila siku za wiki - Sir Nature
8. Dhahabu Records - Dully Sykes

JOSE ana stori nyingi Sana kwenye vichwa vya Wabongo ikiwemo; kuzinguana na Shigongo, kurudia beat ya NIKUSAIDIAJE ya Prof Jay/ Majani, kuwa kwenye beef na mdogo wake, kujirusha ghorofani na nyinginezo nyingi kuhusu utajiri wake.

4. KEKO
Nilikuwa nikimwita African EVE kutokana na flow yake na mwonekano wake.
Alijitambulisha kwa HOW WE DO IT, HOW WE DO IT RMX FT RADIO, MAKE YOU DANCE FT MADTRAXX lakini ngoma NINAYOIELEWA Sana kutoka kwake ni ALWOO ( CRY FOR HELP)

5. NAVIO
Mnyamwezi sana huyu mwamba, alikuwemo kwenye lile goma la ONE EIGHT PROJECT, ambapo kwa Bongo aliwakilisha Ally Kiba na kufanya kazi moja na R Kelly.

6. GNL ZAMBA
Mwamba huyu ambaye alijitambulisha kwa kuchana kwa lugha yake ya Kiganda. Alikuwa na msauti fulani hivi.

7. BOBI WINE
Rais huyu!!
TIME BOMB IS THE CLASSIC. KAMA HUJAWAHI KUISIKILIZA ITAFUTE.

8. AZIZ AZION
NKUMILA OMUKWANO au NITUNZIE MAPENZI BABY Kama Wabongo wengi walivyoiita, ndiyo ngoma iliyompaisha sana kwenye ardhi yetu.

9. EDDY KENZO
Kasumbua vijana wa kizazi hiki na MARIA ROSA na hizi kolabo na akina Harmonize lakini KUMBUKUMBU yangu inarudi nyuma mpaka kipindi kile alipotoka na STAMINA na STAMINA RMX.

10. JULIANA KANYOMOZI
Nianzie kwenye Kolabo ya USIENDE MBALI aliyofanya na Bushoke au nianze kwa WOMAN na RIGHT HERE??
Umewahi kuisikia sauti yake alipokuwa jaji kwenye mashindano ya muziki? Ulikosa vingi!!

11. BEBE COOL
The General, alikuwa kwenye beef na GoodLife kisa kuibiwa Zuwena wake, na walivyo washenzi wakamwimba na kumtaja jina kabisa.
Mwamba aliwahi kuunganisha nguvu na NECESSARY NOIZE wa Kenya na kuunda EAST AFRICAN REGGAE. BASHMENT CREW ambapo waliachia mikwaju kama; FIRE na KUBE lakini baadaye kila mmoja akapita hivi na hamsini zake
Goma ninalolielewa kutoka kwake ni NOBODY MOVE. Bonge moja la sound na goma la kuamsha mashetani.

12. NGONI
Walifanya SIRIMBA na LADY JAY DEE lakini pia walifanya MIMI NA WEWE na AY halafu wakafanya MAPINDUZI na PROF JAY.
DIGI, BIGULA na NASIMAGWE zilikuwa ngoma za moto sana kutoka kwao.

13. BENON AND VAMPOS
14. OBSESSION

Hawa walitamba na JANGU

15. SWANGZ AVENUE

Ilikuwa familia kubwa Sana na ilisumbua mno kwa ngoma yao iliyoitwa LOCOMOTIVE.

16. DAVID LUTALO
HELLENA FT RADIO AND WEASLE na NENDA ni ngoma zilizofanya nikamfahamu na kumheshimu sana.

17. MAURICE KIRYA

Wengi tulimsikia kwenye ngoma ya AY, BINADAMU, HAKUNA aliyeyabishia makamuzi aliyoyafanya kwenye ile track.

18. ZIGGY DEE
ENO MIC ft FATMAH ni CLASSIC PIA.

19. BABA LUKU
Huyu ni maarufu sana Bongo lakini kazi zake hazifahamiki kihivyo.
Nakumbuka nimemsikia kwenye ngoma ya AY iitwayo UTAKE ANTHEM.

20. STEVE KABUYE (KAFAYA)
ONE OF THE BEST PRESENTERS I'VE EVER GIVEN THEM MY ATTENTION.
Alikuwa mtangazaji wa East Africa Radio
Alifanya Kolabo na BEN POL linaitwa KILA WAKATI
Lakini pia yumo kwenye ngoma kama;
1. 41 LEGENDARY - KIKOSI
2. ALL YOU WANT - LUFUNYO
3. TANGAZO
4. WAKATI WA MACHIZI - MONA GANGSTER
5. STREET - NCHA KALI
6. WATU WANGU - FID Q
Sijajua kwa Nini hakutaka kuufanya muziki kwa kumaanisha, ni kipaji kilichochukuliwa poa.

Sarkodie kaja baadaye na Moto mkubwa sana lakini ana Ukafaya ndani yake!!

Ongeza waliosahaulika.
TUTUNZE KUMBUKUMBU PAMOJA.
LUAH SANAA MWAMBETA
THE AUTHOR OF HIS OWN KIND.
 
GNL mzee wa kuchana ni kama Sarko D sikuwahi kuelewa ana maanisha nini ila mtu unapenda tu sijamsikia tena ila maisha ya mwisho na kifo cha Zig De vilinisikitisha sana.
 
Daaah umenikumbusha mbali sana nipo zangu Kampala UG. Pande za makelele west,wandege,chikoni,Ntinda view,Kampala mulunginyo.I wish one day kurudi tena na tena. Viwanja vyetu miaka iyo ilikua Club silick,California Hii ilikua inamilikiwa na wakenya,club sex katikati ya JIJI la Kampala. Niliwai kukutana Na msanii mmoja nilimtungiaga wimbo kwa kiswahili Diz nuts. Alikua sio maarufu. Umenikumbusha mbali mnoooo Maisha matamu lakini mafupi
 
Wakati huo nacheza viwanja vya mukono nakula chapati na mayai ya kukaanga
 
Umetisha Sana..waganda walisumbua Sana bongo
Umenikumbusha..Juliana kanyechakalile..bigula..obugenyi..nkumila imukwano..
Umemsahau mwamba Abdu mulasi..empaya shapu..
 
UGANDA CENTRAL ( +256)
Hili lilikuwa jina la kipindi cha ngoma za Uganda pale East Africa Radio miaka hiyo (sijajua kama bado kipo maana sisikilizi tena redio).
Umewahi kusikiliza muziki wa Uganda?
Ulivutiwa na kazi za nani?
Wimbo gani unaukumbuka mpaka leo?
Binafsi nawakumbuka wafuatao na kazi zao.

1. BLU3 (JACKIE CHANDIRU, CINDERELLA SANYU AND LILIAN MBABAZI)
Tanzania ilikuwa na WAKILISHA, Kenya ilikuwa na TATUU halafu Uganda ikawa na BLU3.
Kwa pamoja walitoa ngoma kali kama;
HITAJI
HITAJI RMX FT MOSHI
BURN
BURN RMX FT NAVIO
Na ngoma nyingine walizoziimba kwa Kiganda.
Cindy alikuwa wa kwanza kujitoa. Lilian akabaki na Lilian na kumwongeza binti mwingine ili jina lisipoteze maana.
Cindy akasimama na mikwaju kama
TOTAL SATISFACTION
ME AND YOU FT P SQUARE
NATAMANI WEWE
OUT OF MY MIND
BLU3 MPYA ikarudi na ngoma kama;
PRISONER FT NAMELESS
STRONG WOMAN
TOGETHER
na wimbo wa taifa ulioitwa WHERE YOU ARE FT RADIO AND WEASLE.
Jacky ndiye niliyekuwa nikimwelewa zaidi na alitoa kazi binafsi kali kama;
AGASSI, OVERDOSE na GOLD DIGGER

2. WEASLE AND RADIO
Radio alikuwa na sauti ya pekee sana na alifariki angali bado anahitajika kwenye game. KIFO CHAKE KINANIUMIZA MPAKA LEO.
Wawili hawa waliwasha moto na ngoma kama;
EVERYTHING I DO, POTENTIAL, UNANIUMIZA, CAN'T LET YOU GO, NAKUDATA FT OMULANGILA SUUNA ( OS), MAGNETIC, ABILITY, NIPE KIFUNGUO FT WIZKID, DON'T CRY FT WIZKID, NYUMBANI FT VBOYO na magoma mengine mengi Kama ZUWENA.

3. JOSE CHAMELEONE
Jamaa alipamba utoto/ ujana wetu kwa ngoma zake za Kiswahili alizozichanganya na vionjo vya nyimbo za watoto. Kuna ambao walidhani alikuwa Mtanzania mwenzetu.

Daktari huyu wa muziki alisumbua Sana na ngoma kama;
BEI KALI, DOROTIA, MAMA MIA, MAMBO BADO, NAUMIA, SAUTI YA DHAHABU, BAHATI YANGU, NAOMBA UNIAMINI, TOBESIGA, SHIDA ZA DUNIA, MAMA RODA FT BUSHOKE, BOMBOCLAT, TUBONGE, VALUVALU

Chameleone ndiye msanii kutoka UG anayeongoza kwa kufanya Kolabo na Wabongo kama ifuatavyo;

1. Ndivyo sivyo - Prof Jay
2. Kiboko yao - Lady Jay Dee
3. Bounce - Mwana FA
4. Nasema nao - AY
5. Kwa ajili yako - Prof Jay
6. Dance flow - Pig Black
7. Kila siku za wiki - Sir Nature
8. Dhahabu Records - Dully Sykes

JOSE ana stori nyingi Sana kwenye vichwa vya Wabongo ikiwemo; kuzinguana na Shigongo, kurudia beat ya NIKUSAIDIAJE ya Prof Jay/ Majani, kuwa kwenye beef na mdogo wake, kujirusha ghorofani na nyinginezo nyingi kuhusu utajiri wake.

4. KEKO
Nilikuwa nikimwita African EVE kutokana na flow yake na mwonekano wake.
Alijitambulisha kwa HOW WE DO IT, HOW WE DO IT RMX FT RADIO, MAKE YOU DANCE FT MADTRAXX lakini ngoma NINAYOIELEWA Sana kutoka kwake ni ALWOO ( CRY FOR HELP)

5. NAVIO
Mnyamwezi sana huyu mwamba, alikuwemo kwenye lile goma la ONE EIGHT PROJECT, ambapo kwa Bongo aliwakilisha Ally Kiba na kufanya kazi moja na R Kelly.

6. GNL ZAMBA
Mwamba huyu ambaye alijitambulisha kwa kuchana kwa lugha yake ya Kiganda. Alikuwa na msauti fulani hivi.

7. BOBI WINE
Rais huyu!!
TIME BOMB IS THE CLASSIC. KAMA HUJAWAHI KUISIKILIZA ITAFUTE.

8. AZIZ AZION
NKUMILA OMUKWANO au NITUNZIE MAPENZI BABY Kama Wabongo wengi walivyoiita, ndiyo ngoma iliyompaisha sana kwenye ardhi yetu.

9. EDDY KENZO
Kasumbua vijana wa kizazi hiki na MARIA ROSA na hizi kolabo na akina Harmonize lakini KUMBUKUMBU yangu inarudi nyuma mpaka kipindi kile alipotoka na STAMINA na STAMINA RMX.

10. JULIANA KANYOMOZI
Nianzie kwenye Kolabo ya USIENDE MBALI aliyofanya na Bushoke au nianze kwa WOMAN na RIGHT HERE??
Umewahi kuisikia sauti yake alipokuwa jaji kwenye mashindano ya muziki? Ulikosa vingi!!

11. BEBE COOL
The General, alikuwa kwenye beef na GoodLife kisa kuibiwa Zuwena wake, na walivyo washenzi wakamwimba na kumtaja jina kabisa.
Mwamba aliwahi kuunganisha nguvu na NECESSARY NOIZE wa Kenya na kuunda EAST AFRICAN REGGAE. BASHMENT CREW ambapo waliachia mikwaju kama; FIRE na KUBE lakini baadaye kila mmoja akapita hivi na hamsini zake
Goma ninalolielewa kutoka kwake ni NOBODY MOVE. Bonge moja la sound na goma la kuamsha mashetani.

12. NGONI
Walifanya SIRIMBA na LADY JAY DEE lakini pia walifanya MIMI NA WEWE na AY halafu wakafanya MAPINDUZI na PROF JAY.
DIGI, BIGULA na NASIMAGWE zilikuwa ngoma za moto sana kutoka kwao.

13. BENON AND VAMPOS
14. OBSESSION

Hawa walitamba na JANGU

15. SWANGZ AVENUE
Ilikuwa familia kubwa Sana na ilisumbua mno kwa ngoma yao iliyoitwa LOCOMOTIVE.

16. DAVID LUTALO
HELLENA FT RADIO AND WEASLE na NENDA ni ngoma zilizofanya nikamfahamu na kumheshimu sana.

17. MAURICE KIRYA
Wengi tulimsikia kwenye ngoma ya AY, BINADAMU, HAKUNA aliyeyabishia makamuzi aliyoyafanya kwenye ile track.

18. ZIGGY DEE
ENO MIC ft FATMAH ni CLASSIC PIA.

19. BABA LUKU
Huyu ni maarufu sana Bongo lakini kazi zake hazifahamiki kihivyo.
Nakumbuka nimemsikia kwenye ngoma ya AY iitwayo UTAKE ANTHEM.

20. STEVE KABUYE (KAFAYA)
ONE OF THE BEST PRESENTERS I'VE EVER GIVEN THEM MY ATTENTION.
Alikuwa mtangazaji wa East Africa Radio
Alifanya Kolabo na BEN POL linaitwa KILA WAKATI
Lakini pia yumo kwenye ngoma kama;
1. 41 LEGENDARY - KIKOSI
2. ALL YOU WANT - LUFUNYO
3. TANGAZO
4. WAKATI WA MACHIZI - MONA GANGSTER
5. STREET - NCHA KALI
6. WATU WANGU - FID Q
Sijajua kwa Nini hakutaka kuufanya muziki kwa kumaanisha, ni kipaji kilichochukuliwa poa.

Sarkodie kaja baadaye na Moto mkubwa sana lakini ana Ukafaya ndani yake!!

Ongeza waliosahaulika.
TUTUNZE KUMBUKUMBU PAMOJA.
LUAH SANAA MWAMBETA
THE AUTHOR OF HIS OWN KIND.
Miaka hiyo Kenya ilikuwa na wasanii wakali. Sasa hivi Wakenya wanaukubali sana muziki wa Bongo
 
Halafu kulikuwa na kipindi kinaitwa STRICTLY KENYAN pia. Kilikuwa ni ngoma za Kenya tu.
Kipindi changu pendwa Kilikuwa kile cha jioni The drive

Siku ingine tujadili vipindi vya Kiss Fm ya zamani.
 
Mimi nilikuwaa mutukula kule tulikuwa tunasikiliza zile nyimbo za wasanii wa hadhi ya Best Naso
Mfano

Abdul Mulasi....Swimming Pool, Obugenyi
Mesaki Semakula......first Aid, Ndekka, taliyo
Phil Lutaya
Obssession, wimbo wao Wekuume
Angela Katatumbaa
 
Back
Top Bottom