Katiba ukiibadilisha inaanza kutumika siku ile ilipoanza
Hauwezi kumshtaki mtu kwa katiba mpya wakati aliongoza kwa mfumo wa katiba nyingne.
Hyo tutaiona tz, MUNGU atupe uhai.
Mkuu Katiba ni siasa na matamanio ya kisiasa.
Wengine mlikuwa hamjazaliwa miaka ya Sokoine na vita ya wahujumu uchumi na walanguzi.
Miaka ya 1980-84 kulikuwa na ukosefu wa mahitaji mengi ya kibinadamu kwa maisha ya kawaida.
Wahujumu uchumi walikuwa wengi pamoja na walanguzi.
Mlanguzi anaenda Mtwara ananunua bidhaa zote za RTC(Regional Trading Company) na kuzileta DSM dukani kwake na anauza bidhaa kwa bei zaidi ya mara nne.
Hapakuwepo sheria yoyote kumzuia mtu kununua kwa mfano, sukari yote toka RTC na kuiweka ghalani na kuuza taratibu kwa mwendo wa kuruka.
Sokoine kama wziri mkuu wakati huo aliamuru walanguzi na wahujumu uchumi wote kukamatwa.
Kumbe hakuna sheria ya kuwahukumu katika katiba yetu wakati huo.
Hivyo watu wako ndani kwa miezi mingi, muswada ukapelekwa Bungeni uli kuwahukumu hao wahujumu na walanguzi.
Na hata sheria ilipotengenezwa kukajitokeza tatizo.
Waliokamatwa ni wengi sana hivyo Mahakimu na majaji wakawa hawatoshi hata kidogo kuendehs mahakama.
Ukapelekwa mswaada Bungeni tena ili wateuliwe watu maalum na wawe mahakimu na waweze kuwa hukumu wahujumu na walanguzi.
Hapo unaona Principle iliyokiukwa hapo, unamkamata mtu na baadaye sheria ndiyo inatafutwa kwa yale matakwa yako, alimradi Bunge limetpitisha.
Usiseme hayawezekani.