Ligogoma
JF-Expert Member
- Aug 27, 2010
- 3,503
- 6,415
Habari wana JF??
Kuna mapenzi yamevunjika hivi karibuni na wasuluhishi walijaribu kuyaokoa ikashindikana!! Mwanamke alikuwa na madai yake lukuki na mwanaume vilevile kiasi kwamba kila mmoja alikwishamchoka mwenzie kabisaa!!!
Nikapata wazo moja tuli-share hapa jamvini!!!
Kipi kilikufanya ukaachwa au ukaamuacha mpenzi wako ambaye ulimpenda sana, ukampa kila kitu, mkapanga mengi, mkaruka ruka na kufurahi pamoja lakini mwisho wa siku ukamuona hafai!!!
Naanza na mie, wangu wa awali ni umbali na kukosa mawasiliano kulitutenganisha kabisaa (miaka ya tisini simu kulikuwa hakuna)
Wa pili alinimwaga sababu ya kipato, nilikuwa ndo kwanza naanza maisha so sikuwa na kipato cha kujitosheleza kutokana na kuwa na majukumu ya kujijenga.
Nawe mwana JF, tupe yako tupate kujua kinachovunja mapenzi ya wengi nini....???