Unakumbuka kilichokufanya ukaacha/ukaachwa...??

Unakumbuka kilichokufanya ukaacha/ukaachwa...??

Ligogoma

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2010
Posts
3,503
Reaction score
6,415
Habari wana JF??

Kuna mapenzi yamevunjika hivi karibuni na wasuluhishi walijaribu kuyaokoa ikashindikana!! Mwanamke alikuwa na madai yake lukuki na mwanaume vilevile kiasi kwamba kila mmoja alikwishamchoka mwenzie kabisaa!!!

Nikapata wazo moja tuli-share hapa jamvini!!!

Kipi kilikufanya ukaachwa au ukaamuacha mpenzi wako ambaye ulimpenda sana, ukampa kila kitu, mkapanga mengi, mkaruka ruka na kufurahi pamoja lakini mwisho wa siku ukamuona hafai!!!

Naanza na mie, wangu wa awali ni umbali na kukosa mawasiliano kulitutenganisha kabisaa (miaka ya tisini simu kulikuwa hakuna)

Wa pili alinimwaga sababu ya kipato, nilikuwa ndo kwanza naanza maisha so sikuwa na kipato cha kujitosheleza kutokana na kuwa na majukumu ya kujijenga.

Nawe mwana JF, tupe yako tupate kujua kinachovunja mapenzi ya wengi nini....???
 
hao wapenzi wako ulikua huwapendi ki ukweli ulikua unacheza nao tuu... mi ninaamini kama kweli umempenda mtu yaani deeply madly in love...then huwezi kuwaacha...ukiwaacha lazima udate...upelekwe muhimbili ukachekiwe akili...usifanye mchezo na kipenda roho...
 
sina uzoefu cuz cwahai kuachwa wala kuacha,nilieanza nae ndo huyo ninae mapaka sasa.ngoja waje
 
1. Shinikizo la wazazi wake - walichukua mahali wakamlazimisha aolewe na Bwana Mwenye mafedha kipindi mi niko shule.
2. Alikuwa na mtoto - kwetu BK mwanamke mwenye mtoto huwezi kumuoa wakamthamini.
3. Alihama kikazi, aliporudi akarudi na mtoto na kusingizia kuwa ni wa kwangu - nikam-mwaga kwa sababu ya uongo wake.
4. ....... bado niko naye na sina mpango wa kumuacha kwa kuwa tumedumu miaka zaidi ya 10 sasa!
 
1. Alikuwa kicheche alikuwa anapenda sana kudo, nikamkatalia kumpa mpaka tufunge ndoa akasepa
2. Sijui sababu zilizomfanya aniacha ingawa yeye huwa anasema umbali ulichangia na huwa hajui ilikuwaje mpaka sasa. Hana sababu ya msingi
3. Nkamgundua ni mme wa mtu nikatupilia mbali.
4. Ndo niko nae na hapa ndo nimefika.
 
1: Alifariki dunia
2: Alikwenda kusoma china japo tunawacliana lakini moyo ulishahama,its ten years now ever since.
3: Alinenepa kupita kiasi...mpaka akawa kero.
4: Nilikuwa nikimpiga bao moja tu,anasema kachoka na mie ndo inasimika vibaya.
5: Nilikuwa sina malengo nae,tumeachana kwa amani japo bado ananitext every night.
 
mwanamke ambae sitakuja kumsahau kamwe,na ndio mwanamke pekee aliyowai kuniacha....alikuwa demu wangu haswa tena zaidi ya demu alikuwa ni rafiki na msela wangu...nilianza nae chuoni mwaka wa kwanza hadi wa tatu...tulikula happy za kutosha,2liendana.. yani uyu demu ni kama tulikuwa damu moja...tulikuja kuachana baada ya kumaliza shule kama utani vile...nakumbuka siku moja aliniambia uku yuko siriaz sana,nitamuoa lini?mie nikachukulia poa tu nikamwambia sasa ivi mapema sana ngoja nijipange kidogo ndo twaweza lekebisha..akaitikia nyie wanaume ndio zenu...hapa ndio mtiti ukaanza sms wala simu azijibiwi nikimuuliza tatizo nini anasema sipo siriaz..watoto wa mjini tukawa tushaelewa 'ugali ushaungua'.

Baada ya muda kidogo hatujaonana wala kuwasiliana,akaniibukia geto kipindi bado nakaa kino...akaniambia samahani nimeona haupo siriaz na mimi nimepata mtu wa kunioa kwaio naolewa soon..basi tuliongea sana siku iyo na tukawa 2meachana kiivo bila kinyongo...demu sasa ivi ameolewa na mtoto wa kizito mwenzake na nifamily friend wao pia.

Kitu ambacho nilijifunza kupitia uyu demu ni kwamba wanawake sio waaminifu,na wana tamaa za kupata haraka...kama ishu ilikuwa ni chapaa sasa ivi najua ananifatilia anaona nilipo fika,tena bado nasonga na ni self made..
 
  1. Kipato
  2. Baba yake alitaka kunisomea albadil
  3. Alianza kutembea na baba yake wa kambo baada ya mama yake kufariki
  4. Race (ilikuwa haiwezekani kuoana)
  5. Dini
  6. Rafiki yake
  7. Tamaa
  8. Alikuwa njia panda
  9. Tumeoana na tunapendana sana na tuna watoto sasa maisha yanasonga
 
Nteko Vano, hiyo namba 2 imenichekesha.

Hizo sababu zote ni kwa mtu mmoja au tofauti?
 
Last edited by a moderator:
1. Mapenzi yaliisha? Dini tofauti na nilipata mali mpya......
2.mali mpya hii niliipoteza kwenye ajali ya gari
3. Huyu 'tumeWOWAna'
 
Nteko Vano, hiyo namba 2 imenichekesha.

Hizo sababu zote ni kwa mtu mmoja au tofauti?

Hahaaaa, mkuu Kongosho we acha tu.

Sure, yamenipata kwa hao 8 kabla sijaoa. Nakumbuka baada ya kuachana na wa 8 ilinibidi nikae miaka 2 bila kuwa na uhusiano mwingine ili nijipe muda wa kutafakari.
 
Back
Top Bottom