Unakumbuka nini kuhusu Redio ya Kaseti

Unakumbuka nini kuhusu Redio ya Kaseti

Rhz4567

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2018
Posts
4,893
Reaction score
6,599
Mimi nakumbuka kipindi hiko kama unakwenda kuchunga mifugo upo nayo mkononi kwenda kulima na kupalilia mazao lazima Kaseti iwe pembeni bila Kaseti kipindi hiko nisawa na kijana wa sasa bila smartphone kaka zetu na baba zetu walifaidi sana ujana
 
Nakumbuka ukitaka kusogeza mbele wimbo unatumia pen na ukitaka kustopisha wimbo ili usikilize baadae unazima kwanza
 
Nakumbuka miaka ya 90 tulikuwa tukienda kulima vibarua mashamba ya tumbaku Tabora. Tukipewa ujira mwisho wa msimu tunanunua kaseti na kurudi home tunafunga kijiji kizima
 
Nakumbuka ikizima unaipiga kibao kimoja inaendelea kufanya kazi
Hiyo ni mkulima ila kaseti zilikuwa na tabia ya kusinzia basi ukiwasha kibao inaendelea

Mkulima yenyewe inazima afu ndo taarifa ya habari RTD basi inawashwa kibao afu inawaka tena
Unaweka mguu juu mambo saafi kabisa
 
Ahahah. Nakumbuka ukitaka ku rewimd unatumia pen ya biki tu. Sema kasheshe ilikua kujua exactly ngoma unayotaka inaanzia wapi.

Ikianza kuliwa sasa ,halaf ukute kanda maza kaazima kwa shougaake..hahhahaaa lzm jicho likutoke
 
Nakumbuka pen ilihusika sana au kijiti chenye pembe ili kutunza battery zisiishe mapema.
Nakumbuka makosa yangu niliharibu wimbo wa pepe kalle haswa pale anapomuimba Lonyamila, nilijaribu button ya kurecord ikafuta weeee niliiweka kwenye mfuko nikaitupa mbali na nyumbani kkkkkkk
 
Back
Top Bottom