Unakumbuka nini ukiona picha za Programu hizi? (Nero, Ashampoo, JetAudio na Window Media Player)

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
Programu kama Nero Burner na Ashampoo Burning zilitumiwa sana nyakati za zamani kwa kuchoma CD na DVD, kujenga na kuhariri video na muziki. Windows Media Player na JetAudio pia zilikuwa maarufu kwa kucheza na kusimamia faili za media.
Hizi zilikuwa sehemu muhimu ya vifaa vya programu za zamani ambazo zilikuwa zinahitajika sana kabla ya teknolojia ya sasa ya kutumia wingu (cloud-based) na huduma za kisasa za media.

Software ya kuchoma CD - nero



Ashampoo Burning Studio 6

Music Player Jet Audio

Window Media Player
 
Naikumbuka window XP, window 2000, window vista , du izi window zinaingia mda mrefu sana yani
 
Hizi ndo takataka gani? Mambo na Adrod, IOS, YouTube spotify AI
 
Like humans do hapo kwa windows media player imenirudisha nyuma miaka 20 hivi.... Miaka inakimbia
 
Dah ahhhhhaah😅😅😅
Window Xp na Vista kabisa hizi
 
ni watu wachache sana walikuwa wana burn cd enzi hizo, nyimbo 18 kwa cd shilingi elf 5, window elf 20, games elf 10, video na muvi nimesahau ila Pilau ilikuwa elf 20 wateja walikuwa wenye uwezo wa kununua redio zenye vcd, Hapo zamani miaka ya 2000 hadi 2006 hata account ikisoma elf 20 ni sawa na laki ya sasa,

vijana walinunua magari, walivaa vizuri na wenye akili waliweza kujenga, kujisomesha, kufungua biashara, kunuua mashamba, n.k.

jirani yangu aliendekeza starehe pombe na kufunua vyupi, Mapinduzi ya teknolojia yakaharibu biashara, kwa sasa umri umeenda sana anatia huruma
 
Hasa hiyo Nero burner inanikumbusha 2005 hivi wakati nipo na desktop yangu used.
 
Nimepiga hela sana kwa hizo software

Ila VLC mbona hujaiweka japo yenyewe ilikuja mwishoni mwishoni
 
Kuna mwanangu bado ana vimba na jet audio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…