Unakumbuka nini ukisikia jina la Adam Simbeye kwenye THIS WEEK IN PERSPECTIVE

Unakumbuka nini ukisikia jina la Adam Simbeye kwenye THIS WEEK IN PERSPECTIVE

View attachment 3561776

Leo kwenye urejeo wa fikra zangu nikapata kukumbuka kipindi maridhawa kilichokuwa kikiruka hewani kupitia chaneli ya TBC ,THIS WEEK IN PERSPECTIVE kikiongozwa na mtangazaji mahiri enzi hizo bwana Adam Simbeye.

Mule kulikuwa na wazee wanachapa ngeli ya mambele kama wanakunywa supu ya kongoro tu 😂.
Mimi na ngeli ya kuunga nilikuwa naangalia bila kuambulia kitu.

Hivi jamaa yuko wapi sikuhizi Mr Adam Simbeye maana sasahivi hskuna vipindi vya kariba yake

Unakumbuka nini mdau kupitia kipindi hicho wakati huo .
View attachment 3561777
Hapo ina tembea lugha mwanzo mwisho ila tisa kumi kingereza cha maprofesa 😀🙌
 
Nakumbuka mzee Wilson mukama nahisi alikua katibu au makamo ndani ya CCM kila akiongea ni may be, may be na actually ndio zilikua starting point yake ya kila kitu.
Well come to this week in perspective with me Adam simbeye🤣🤣🤗 . Kilikua siku ya ijumaa saa tatu usiku
😂😂😂 Ewaa ilikuwa kila ikifika ijumaa mida ya saa 3 ,
 
Mzee nilikuwa najua hajui kiswahili harafu ni ijumaa mnasubiri tamthilia mnakesha harafu mbu nyingi nimekumbuka mbali 🤣
 
Back
Top Bottom